Kuna wimbo mpya umetoka. Si mwingine ni kijana wetu, Roma Mkatoliki.
Wimbo unaitwa "Nipeni Maua Yangu" humo ndani kuna madini ya kutosha. Roma Mkatoliki kama kawaida yake katoa ya moyoni yanayoendelea katika utawala huu wa awamu ya 6. Kama kawaida kanyoosha maelezo hajapindapinda.
Hakika baada ya kuusikiliza nampa maua yake ayanuse angali akiwa hai.
Ni mstari upi umekuvutia zaidi? Tushirikishe hapa...
1. Jeshi gani mpaka leo Mmeshindwa kumjua Kigogo
2. Mbona vyuma vimekaza halafu mama anaificha grisi
3. Tulihoji mkajibu kwa dharau tuhamie Burundi
4. Iringa tuna msitu lakini stick tunaagiza China
5. Mnatuambia tujiajiri mbona nyie hamkujiajiri? Ok nikupe boda yangu unipe uwaziri. Nikukabidhi vyeti vyangu hangaika navyo mwezi mmoja, niko pale nakungoja uje tuzungumze lugha moja😂😂
"Mnatuambia tujiajiri mbona nyinyi hamkujiajiri nikupe boda yangu nawe unipe uwaziri? Nikukabidhi vyeti vyangu uangaike navyo mwezi mmoja niko pale nakungoja uje tuongee lugha moja."
Anakwambia "mi sio CCM sio Chadema, ila ukiweka CCM na andazi ntachgua andazi".[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
haya sikilizeni na nyinyi Ngoma
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]