Biashara yoyote ya chombo cha moto kama hutegemei kuendesha wewe achana nayo. Kuanzia bodaboda, bajaji, toyo, coaster, Yutong, fuso, malori(truck) etc. Ndo maana zaidi ya 95%, wamiliki wanabadilika kila baada ya miaka michache, wanakuja wapya kama wewe, hizo % zilizobaki ndo wakongwe akina Abood e.t.c. Kuna watu watanipinga lakini naongea hili nina uzoefu nalo wa miaka mingi, tatizo linaanzia kwa utakao wakabidhi chombo. Kila mmoja anaona kama amepata nafasi ya kujikwamua na umaskini, kama watumishi wa serikali wanavyoichukulia serikali ili waipige, konda na dereva pia wanakuona kama serikali, bado latra, traffic, fundi gereji, bima, sheli,. Kuna wakati dereva akipiga simu unatamani usipokee. Fanya research kabla ya kujilipua.