Nami nlikuwa na plan ya kuanza na bajaji ambayo nitaitoa kwa mkataba kwa mtu/ hesabu za siku kwa Dar es Salaam.
Sijawahi fanya,lakini nishawahi kufanya ya pikipiki miaka ya nyuma mkoani Mbeya, nlimpa dereva jamaa wa heshima tu na familia. Haikuenda vizuri, lakini tukaja fikishana polisi mara moja ndiyo mambo yakanyooka.
Japo jamaa alikuja kunyooka sana baada ya kufikishana polis,ile biashara haikunipa hata faida ya 100 sababu sikuwa na chanzo kingine cha mapato,hela inakuja na kupitiliza.
Mkataba uliisha,na sina hata 100 ya ile pikipiki nami jamaa nikampa kadi yake kiroho safi.
Ninavyoona bajaji mjini ni kama zinakuja kuja hivi kwa watu wanaopiga bolt.
Kama kuna mtu ana uhalisia wa hii biashara amwage details zote. Changamoto za dereva najua ni kubahatisha, ikiniridhisha kuna faida nitafanya jambo.
Biashara nyingi zina changamoto sana ni kujilipua litalonipata inakuwa part ya maisha😁😁😁