Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 42,525
- 74,605
Nakuelewa Sana kaka, sasa sisi tunafanya kazi ngapi, shambani niende Mimi, Daladala nayo niendeshe Mimi, Maguta pia niwepo na bado ofsini paliponipa yoote haya niende ndivyo unamanisha kwamba lazima nisimamie mwenyewe na kuendesha mwenyewe?Mkuu nilishamiliki daladala, simaanishi kila mtu atapitia njia niliyopitia. Kuna kitu inaitwa return on investment, umewekeza milioni 10/20/30/40 au zaidi zitarudi baada ya muda gani kwa hizo vurugu nilizizitaja hapo juu!?,. Utafiti niliofanya, waliofanikiwa hasa kwenye daladala hawakai na daladala muda mrefu, kwa mfano akinunua coaster baada ya mwaka mmoja na nusu au zaidi kidogo, analiuza likiwa kwenye hali nzuri sana. Hii biashara kama mmiliki ni dereva utakuwa road mwenyewe hata sasa hivi nakushauri nunua gari hata used anza kazi, lakini kama utakaa nyumbani au ofisini ukisubiri hesabu sikushauri. Changamoto ni nyingi mno. Haina tofauti na kilimo cha pdf, upo Dar mashamba yapo Ifakara unahudumia shamba kupitia watu kwa njia ya simu na Whatsapp ππ
Hapana sio lazima, lakini usicheze mbali. Uwe mtu usiyetabirika, ukifanya biashara ya daladala uwe mtu wa machale hata saa 8 za usiku unashtuka. Kwa mfano nilikuwa na daladala linafanya route ya Mwenge - Tazara kabla daladala(hiace-dungu) hazijaondolewa mjini, ilikuwa mwisho saa 3 usiku, dereva anapaki sheli fulani anaamsha saa 11 na nusu alfajiri, siku moja saa 8 za usiku natoka airport kumpokea mgeni nikalikuta Buguruni linapakia, kuchungulia hata dereva anayeendesha simjui, nayeye hanijui na nilikuwa bwana mdogo. Ni mfano mdogo, lakini ku deal na watu wenye shida ambao ni vigumu kujua kichwani wanawaza nini ni shida. Kuna madereva ukiwabana sana wanakubadilishia hadi gear box kwa malipo ya laki 5/6 hadi milioni, hadi engine ukikaa vibaya kutokana na shida zilizowazunguka kwenye familia zao. Mkuu usione kama negative sana na biashara ya vyombo vya moto, ila ina changamoto nyingi sana. Hata hivyo ukikomaa waweza kuwa kwenye hizo % chache za waliofanikiwa, hatukatishani tamaa, tunabadilishana uzoefu. Kila la heri.Nakuelewa Sana kaka, sasa sisi tunafanya kazi ngapi, shambani niende Mimi, Daladala nayo niendeshe Mimi, Maguta pia niwepo na bado ofsini paliponipa yoote haya niende ndivyo unamanisha kwamba lazima nisimamie mwenyewe na kuendesha mwenyewe?
Asante Sana Mkuu, hapa unatufunulia Pandora box, hii ya kufanya kazi usiku inawezekana kabisa na ndio inachosha gari kwa sababu gari haipumui na wanapeana madereva wanaojuana mwisho linakufa, hizi Ziada za kushtukiza nitakuwa nazifanya sanaHapana sio lazima, lakini usicheze mbali. Uwe mtu usiyetabirika, ukifanya biashara ya daladala uwe mtu wa machale hata saa 8 za usiku unashtuka. Kwa mfano nilikuwa na daladala linafanya route ya Mwenge - Tazara kabla daladala(hiace-dungu) hazijaondolewa mjini, ilikuwa mwisho saa 3 usiku, dereva anapaki sheli fulani anaamsha saa 11 na nusu alfajiri, siku moja saa 8 za usiku natoka airport kumpokea mgeni nikalikuta Buguruni linapakia, kuchungulia hata dereva anayeendesha simjui, nayeye hanijui na nilikuwa bwana mdogo. Ni mfano mdogo, lakini ku deal na watu wenye shida ambao ni vigumu kujua kichwani wanawaza nini ni shida. Kuna madereva ukiwabana sana wanakubadilishia hadi gear box kwa malipo ya laki 5/6 hadi milioni, hadi engine ukikaa vibaya kutokana na shida zilizowazunguka kwenye familia zao. Mkuu usione kama negative sana na biashara ya vyombo vya moto, ila ina changamoto nyingi sana. Hata hivyo ukikomaa waweza kuwa kwenye hizo % chache za waliofanikiwa, hatukatishani tamaa, tunabadilishana uzoefu. Kila la heri.
Mkuu hizi mambo za kuroga riga huwa zipo kwenye hii biashara?Hii biashara ukikaa wewe mwenyewe hela utaiona vizuri kabisa. Lakini ukikabidhi mtu asiye muaminifu awe ndiye msimamizi kwisha habari kila mara ni simu za majanga na excuses zisizo na msingi.
Nina uzoefu nayo niliifanya kati ya mwaka 2016 na 2024. Nilipobanwa na majukumu mengine nikamkabidhi mtu ndipo nilipoona ugumu na hasara.
Upo sahihi na ndicho hata mimi nilichosema hapo juu.Hii biashara kama mmiliki ni dereva utakuwa road mwenyewe hata sasa hivi nakushauri nunua gari hata used anza kazi, lakini kama utakaa nyumbani au ofisini ukisubiri hesabu sikushauri.
Nadhani tunaelewana sasa vizuri, kwamba kunahitaji tahadhari, regular service/maintenanceUpo sahihi na ndicho hata mimi nilichosema hapo juu.
Ukikaa mwenyewe kama dereva aise biashara ni nzuri na faida utaiona kwasababu utaendesha gari lako kwa tahadhari zote na regular services/maintenance utazifanya vizuri.
Dah! Umenimumbusha mbali sana Enzi za kutaabika, mie ilikuwa nikisikia simu inaita nashtuka kama kichaa ππBiashara yoyote ya chombo cha moto kama hutegemei kuendesha wewe achana nayo. Kuanzia bodaboda, bajaji, toyo, coaster, Yutong, fuso, malori(truck) etc. Ndo maana zaidi ya 95%, wamiliki wanabadilika kila baada ya miaka michache, wanakuja wapya kama wewe, hizo % zilizobaki ndo wakongwe akina Abood e.t.c. Kuna watu watanipinga lakini naongea hili nina uzoefu nalo wa miaka mingi, tatizo linaanzia kwa utakao wakabidhi chombo. Kila mmoja anaona kama amepata nafasi ya kujikwamua na umaskini, kama watumishi wa serikali wanavyoichukulia serikali ili waipige, konda na dereva pia wanakuona kama serikali, bado latra, traffic, fundi gereji, bima, sheli,. Kuna wakati dereva akipiga simu unatamani usipokee. Fanya research kabla ya kujilipua.
Hiyo sentensi ni sahihi kabisa!!!!!! Mfano wangu hai, boss wangu alianza na Tax Bubu mambo yalikuwa safi enzi za 80s, baadaye akaenda Daladala wakati Tax Bubu zilipocharuka. Daladala zilikuwa safi kwenye 90s miaka ya 2,000 nazo kirusi kikaziingia. Akakimbilia Malori, baadaye meneja wake akanishauri ayauze mamende mwaka 2017. Cha ajabu la mwisho akadai atamlipa kidogo kidogo! Hapo ndipo hata uhusiano uliharibika. Wewe umeshauri kuuza maana ni biashara kichaa, lakini la mwisho unadai utalipa taratibu!! Kama hayakuwa na matatizo kwanini ushauri yauzwe?Biashara yoyote ya chombo cha moto kama hutegemei kuendesha wewe achana nayo. Kuanzia bodaboda, bajaji, toyo, coaster, Yutong, fuso, malori(truck) etc. Ndo maana zaidi ya 95%, wamiliki wanabadilika kila baada ya miaka michache, wanakuja wapya kama wewe, hizo % zilizobaki ndo wakongwe akina Abood e.t.c. Kuna watu watanipinga lakini naongea hili nina uzoefu nalo wa miaka mingi, tatizo linaanzia kwa utakao wakabidhi chombo. Kila mmoja anaona kama amepata nafasi ya kujikwamua na umaskini, kama watumishi wa serikali wanavyoichukulia serikali ili waipige, konda na dereva pia wanakuona kama serikali, bado latra, traffic, fundi gereji, bima, sheli,. Kuna wakati dereva akipiga simu unatamani usipokee. Fanya research kabla ya kujilipua.
Nunua mpya,Nataka kuingia kwenye biashara ya daladala, lakini nahitaji ushauri wa wazoefu.
Kwa walio kwenye biashara hii, ni mambo gani muhimu ninayopaswa kuzingatia kabla ya kuanza?
HahahaDah! Umenimumbusha mbali sana Enzi za kutaabika, mie ilikuwa nikisikia simu inaita nashtuka kama kichaa ππ
Hili nimeshaliona kwa Mujibu wa hadith nilizopewa, watu waliozifanya kwa moyo na kuzipenda wamefika mbali. Hii biashara hatua za mwanzo ni ngumuHakuna biashara nyepesi. Hizo gari zinazowashinda watu zilizokosa matunzo na uchakavu wengine ndio wanaanzia kama starting point na zinawalipa na zinawafanya wapige hatua.
Biashara ya usafirishaji wa magari inataka mmiliki uipende kwanza usifanye kwa kufata faida za makaratasi na mwingine anavyofanya.
Mpya TZ sio Mpya japan, na zenyewe bado zina vipengere japo sio sanaNunua mpya,
Usinunue used
Ni ushauri mzuri lakini huu kila mtu anajua na hizo route fupi zenye hela zilishajaa kitambo sanaChangua route fupi yenye barabara nzima na Abiria wa kutosha kurudisha pesa yako
Umesema hujawahi kuwaza biashara kama hii lakini tayari unajua kuwa ni Pasua kichwa? Umejuaje? Kwa kusikia?Sijui ni kwa nini siwahi kuwaza biashara ya kumiliki chombo cha moto... the likes of boda, bajaji, gari ! Hii ni pasua kichwa... presha muda wote, chombo kinachoka pesa huioni .... mara ajali na majanga mengine
Kuna namna ya kuzipata mkuuπππNi ushauri mzuri lakini huu kila mtu anajua na hizo route fupi zenye hela zilishajaa kitambo sana