Nipeni ushauri, nataka kufanya biashara ya daladala. Wazoefu naomba ushauri

Kuna namna ya kuzipata mkuuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mpaka upenyeze Rupia.
Kama Ruti ya Makumbusho Stesheni via mwananyamala na Makumbusho Posta via Bagamoyo Road gari zote ni zile mnazoponda zimechoka lakini kuna wamiliki wapo route hiyo zaidi ya miaka 10 na route ikiwa fupi hesabu itakuwa chini
 
Kwanza tafuta njia nzuri yenye barabara bora,dereva au konda uwe mwenyewe mwisho chuma nunua ambayo haijatumika apa bongo maana hua atupendan huwez uziwa chombo nzima mkoni
 
Nami nlikuwa na plan ya kuanza na bajaji ambayo nitaitoa kwa mkataba kwa mtu/ hesabu za siku kwa Dar es Salaam.

Sijawahi fanya,lakini nishawahi kufanya ya pikipiki miaka ya nyuma mkoani Mbeya, nlimpa dereva jamaa wa heshima tu na familia. Haikuenda vizuri, lakini tukaja fikishana polisi mara moja ndiyo mambo yakanyooka.

Japo jamaa alikuja kunyooka sana baada ya kufikishana polis,ile biashara haikunipa hata faida ya 100 sababu sikuwa na chanzo kingine cha mapato,hela inakuja na kupitiliza.

Mkataba uliisha,na sina hata 100 ya ile pikipiki nami jamaa nikampa kadi yake kiroho safi.

Ninavyoona bajaji mjini ni kama zinakuja kuja hivi kwa watu wanaopiga bolt.

Kama kuna mtu ana uhalisia wa hii biashara amwage details zote. Changamoto za dereva najua ni kubahatisha, ikiniridhisha kuna faida nitafanya jambo.

Biashara nyingi zina changamoto sana ni kujilipua litalonipata inakuwa part ya maisha😁😁😁
 
Nataka kuingia kwenye biashara ya daladala, lakini nahitaji ushauri wa wazoefu.

Kwa walio kwenye biashara hii, ni mambo gani muhimu ninayopaswa kuzingatia kabla ya kuanza?
Ukifanikiwa kuanzisha hiyo biashara usisahau kununua vifaa vya kupimia magonjwa yasiyo ya kuambukiza mfano kisukari na shinikizo la damu. Lakini pia uhakikishe unakuwa na akiba ya kutosha ya dawa za kutuliza maumivu kama vile panadol, nk.
 
Hakikisha unakuwa na moyo mgumu kama wakamaria, yan uwe mtu ambaye ukiambiwa sahv mwanao anaumwa amekimbizwa hospital hushtuki wala nini basi ndio utaiweza hiyo biashara
 
Piki pili ya Mkataba nin zero profit, watu wanafurahi kale ka elfu 10 Ka kila siku lakini Kihasibu after 10-12 months hakuna kitu unaambulia
 
Ukifanikiwa kuanzisha hiyo biashara usisahau kununua vifaa vya kupimia magonjwa yasiyo ya kuambukiza mfano kisukari na shinikizo la damu. Lakini pia uhakikishe unakuwa na akiba ya kutosha ya dawa za kutuliza maumivu kama vile panadol, nk.
Watu mnatishana jamani daah
 
Nataka kuingia kwenye biashara ya daladala, lakini nahitaji ushauri wa wazoefu.

Kwa walio kwenye biashara hii, ni mambo gani muhimu ninayopaswa kuzingatia kabla ya kuanza?
Niliwahi ifanya hii biashara miaka 7/8 iliyopita zilikuwa 3, mbili coaster na moja Eicher kwa sasa hata sijui zipo wapi, ninachojua nilikuwa na fundi wangu Msambaa, fala sana huyu na dereva Tall huyu ndio nilikuwa namwelewa kati ya wote. Changamoto za wakati ule na sasa zinaweza kuwa tofauti ila kama upo serious na hela kweli unayo nenda mahali penye utulivu upige kwanza smirnoff spirt vodka...utakuja kushukuru!
 
Ushauri wako haujanyoka
 
Tafuta interview aliyofanya Sumry wakati anatundika daluga na kwenda shamba kulima.

Usimamizi ndiyo mchawi na zaidi aliwaangushia lawama madereva hawajali wala kuheshimu kazi zao.
 
UTAKAPO NUNUA MABASI ANZISHA ROUTE YA SEGEREA -KINYEREZI-MBEZI-KIBAHA-MLANDIZI-CHALINZE.
NAULI -2500/-
 
Haya ni maoni yangu.
Fundi ni adui namba moja w boss. Fundi anasema nimebadilisha spare kumbe HAPANA na pesa kachukua y ufundi na spare. Na fundi akijua hujui magari n spare ndio Wana maneno yao kua tajiri sio ndugu yako mwibie sana ipo cku atahama tu.
Dereva ndio nuksi kabisa wala hafai ikifika mda w Hesabu utackia kazi mbovu leo utapewa nusu. Akiona anataka kukuama anaiba spare kwa kuuza Diffu,Gear box au ukifanya makosa hadi injini. Hii wanaita change cotta wao. Kuna Dereva mmoja uyo alikua asubuhi hadi ucku Hesabu ya boss. Kisha anajifanya amepaki sheri ucku mnene anacheza dili na mlizi w anaamsha gari kutafuta Hesabu zake. Kwa maana fupi gari lilikua alipumziki kwa cku.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Hii comment hadi nimeogopa nikatetemeka
 
Route zinaanzishwa na LATRA siyo kuamka na kujiamria tu.
Toka zamani,unaweza kuomba njia na ikarasimishwa rasmi./ Route nyingi sana zilianzishwa na daladala then latra wanazirasimisha na kuzipa mkanda wa rangi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…