Nipo Dar, biashara ipi inalipa kati ya kukaanga miguu ya kuku na kukaanga mihogo?

Nipo Dar, biashara ipi inalipa kati ya kukaanga miguu ya kuku na kukaanga mihogo?

Nina laki MBILI
Mihogo iwe asubuhi, na ununue ile laini ambapo utaanza Kwa kuichemsha kidogo iive iwe laini ndio uiweke kwenye mafuta, jioni kama walivosema wadau ndio udeal na bando za mazao ya kuku, usisahau dagaa mchele kuanzia asubuhi pilipili chachandu iwepo ya kutosha, na Kwa asubuhi ungekua kona ya wanaopika supu au maharage ni safi zaidi, tafuta kona moja matata yenye watu wengi na uwe msafi, kila chakula usishike na mikono yako uwe na vifaa maalumu au gloves za nylon,
 
Binadamu bana si Bora mm nna wazo kama Hilo? Kuomba ushauri nimekosea?
Wasomi wangapi wapo mtaani hata wazo la biashara hawana wanategemea kuajiliwa!
Wengine wanakuja hapa jukwaanikuomba msaada wapate kula najua ww ni shahidi

Hupaswi kuninanga mkuu haya maisha tu!
Ndio maana hao wasomi walioko mitaani tuna washangaa. Na ndio maana wewe umekuja kuomba ushauri Kwa akina sisi tusipo soma mkuu.

Hapa hatukunangi Bali tunakuambia ukweli mjue elimu yenu mnayoisomea haiwasaidii mkija mtaaani mnaanza upya kutegemea wasio soma.

Ukweli mchungu huu mdogo wangu pambana na hongera Kwa kujitambua.
 
Kwamba waliosoma hata kabla ya kufa wake zao wanaolewa?
 
Baadae ukikaa vizuri asubuhi kwenye mihogo, unatafuta dada unaweka meza yako ya alminium unatengeneza mboga mboga kwanza unapika maharage ya kupima, unakua na vidagaa mchele vya kupima, unakua na kipimo umekatakata mbogamboga kama kabichi, chines, hapo Kwa siku utapata pesa tu kikubwa location yako, usafi na lugha njema Kwa wateja vitakubeba, kwenye maharage usiweke chumvi na uwe na kifriza kidogo kitakusaidia, wasaidizi wako waeleze usafi usafi,
 
Good idea

Kukaanga mihongo na kuuza makusanyo ya kuku

Kwa kuanza waweza kuanza na mihogo na makusanyo ya kuku

Ila target yako iweke ktk kuuza kuku wa kukaanga .

Kuku faida yake ni kubwa Sana waweza pata 20-30-50K faida kutegemea na mtaji wako.

Wapi utapata location?

Tafuta dalali ongea naye atakupatia location ya kufanya biashara.

Maeneo (location)

Lenga eneo lenye bodaboda hao ndo wateja wakubwa.
 
Kingine usione aibu kabisa wewe chakarika, Kwa nguvu sahau mambo ya kozi uliyosomea,
 
Back
Top Bottom