Pre GE2025 Nipo kwenye hatua za mwisho za kusajili chama kipya cha siasa kitakachoing'oa CCM kabla 2025. Nahitaji vijana 10 tu kutoka kila mkoa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Umedai hakuna kada wa ccm atayeanzisha chama Cha maana,ndiyo nikamtaja mtei na chadema yake,hoja haikua promo jf
Huyo niliyempa hilo jibu, limeendana na mada yake, au unataka majibu yanayobeba mtazamo wako?
 
Mimi sio mtei Kila mtu na njia zake ,na je aliwahi hata kutikisa sharubu za ccm au kushika Dola?
Atatikisaje sharubu za ccm wakati, ccm haishindani kisiasa bali mbeleko ya vyombo vya Dola?
 
Kila aliyezaliwa kabla ya vyama vingi alikuwa ccm hata hao viongozi wa upinzani waliopo sasa walikuwa ccm
Walikuwepo ccm kwa hiari yao, au ilikuwa ni automatic membership?
 
Sina utani kabisa kwenye hili jambo nimedhamilia , kama vijana wa nchi hii ,tuliweka Imani kubwa sana kwa vyama vya siasa vilivyopo ,tangu mwaka 1995 mpaka sasa ,hakuna chama hata kimoja ambacho kimethubutu kuiondoa ccm na kushika Dola! Zaidi tu tunaona ni vyama vyenye malengo ya kujikimu kimaisha kupitia ruzuku wanayopata !! Hakuna kipya Cha kujifunza kwenye vyama vilivyopo kwa sasa ,kwa sababu vimetawaliwa na uoga ,ubinafsi na ukanda 😭vyama vilivyopo sasa haviwezi kushika Dola abadani! Sera za vyama vyetu vya siasa vilivyopo ni ama kujipatia kipato na kung'ang'ana ili kulinda maslahi binafsi ,ndio maana ni wale wale hakuna rotation ya kimfumo ,nenda uendako Kila ukirudi utawakuta ni wale wale ! Tunahitaji chama kipya kitakachotatua mtanzuko huu holela wa vyama siasa! Marehemu sengondo mvungi aliwahi kuonya umajumui wa vyama vyetu hasa uchaguzi ukikaribia kufeli kwa mikakati na usaliti . Sisi ni vijana na hii ni nchi yetu twendeni kifua mbele tuibebe Tanzania kuipeleka nchi ya ahadi ! Mimi naamini Kila mkoa wapo vijana wanaotamani mageuzi na nafasi ya kuonyesha karama zao katika siasa ! Majukwaa ya kisiasa yaliyopo sasa Yana wenyewe ! Ni yao na watoto wao ! Tuundeni chama kipya kama alivyofanya mwanamziki bobi wine pale Uganda! Ni kijana mdogo lakini amefanikiwa kuunganisha vijana nchi nzima na sasa chama chake Cha NUP ,kinaelekea kushika Dola! Tunao vijana bukoba ! Mbeya ,rukwa ,tabora ,ruvuma ,lindi ,mwanza na mikoa mingine yote ambao kwa pamoja tunaweza kuunda chama chenye nguvu sana na kikawashangaza watu! Tuache kukesha mitandaoni tukisubili eti vyama vilivyopo kwamba vinaweza kutuletea mabadiliko yoyote ! Tutakuwa wafu tunaosubili kuangua embe kwa miti ya michongoma ! Tuamke ,tuliamshe taifa letu !kama ni hivyo basi kwa mujibu wa Sheria na kanuni tunaanza kuelekea 2025 tukiwa na chama kipya Cha kisiasa!
Soma kuhusu ostracism, usije ukaondolewa mwenyewe
 
Tatizo walilonalo wa-Tanzania siyo vyama vya Siasa.

Aidha, CCM kuendelea kubaki madarakani haitegemei kupigiwa Kura na mtu yoyote yule ktk Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha !
Usikubali kukatishwa tamaa na wanufaika wa mifumo iliyopo !!

Keep it up ! Chama chenu kikipata usajili hata sisi baadhi ya wazee tutawaunga mkono !🙏🙏🙏
 
Chama kikuu cha upinzani CHADEMA kimeshindwa kuking'oa CCM madarakani itawezekana vipi kwa chama chako kisichojulikana? Unaleta mzaha kana kwamba hujui nguvu ilizonazo CCM
 
Mbona hujasema unahitaji vijana wa aina gani na wenye elimu gani?
Harakati za ukombozi zinamhitaji kijana yeyote wa kitanzania awe amesoma ama lah! Mengine tutaelekezana kwenye vikao pindi tutakapo Anza rasmi
 
Chama kikuu cha upinzani CHADEMA kimeshindwa kuking'oa CCM madarakani itawezekana vipi kwa chama chako kisichojulikana? Unaleta mzaha kana kwamba hujui nguvu ilizonazo CCM
Umenena vema kwamba chama kinachojulikana kimeshindwa ,kwa maana hiyo ukongwe wa chama sio hoja ! Bobi wine alisajili chama chake mwezi mmoja kabla ya uchaguzi na akapata nusu ya viti bungeni !rais wa sasa wa Senegal diomaye Faye alikuwa hajulikani popote na amesajili chama chake mwezi mmoja kabla ya uchaguzi na ameshinda uchaguzi hivyo mikakati na ubora wa mipango ndio itatusaidia sio ukongwe
 
Harakati za ukombozi zinamhitaji kijana yeyote wa kitanzania awe amesoma ama lah! Mengine tutaelekezana kwenye vikao pindi tutakapo Anza rasmi
Basi mimi nipo kigoma nilijaribu mpaka leo ni mwanachama wa act wazalendo lakini sikielewi hichi chama changu kinasimamia kitu gani
 
Kwani tusikinunue chama kimoja mamluki kinachotumiwa na CCM,kama vile TADEA,NRA au chochote kati ya vile 22.
Kuanza upya ni kazi sana,tupindue tu wapumbavu kwenye chama kimoja mamluki,tuamshe umma.
 
vijana wachukue nchi bila kupitia jeshini? Ushakuwa na wenge sasa
 
Bila backup ya kiulinzi na usalama ni ngumu.
Kingine unahitaji vyombo vya habari kama radio,tv na magazeti kwa sababu kaa mkao wa hotuba zenu kupigwa marufuku kwenye vyombo vya habari.
Tafuta wanasheria nondo watakaoweza kukupambania hasa pale unapobablmbikwa kesi za kutunga.
 
Watu makini hawaingii kwenye vyama kinyumbunyumbu bila ya kujua falsafra yake,itikadi,misimamo,sera,malengo na dira yake.
 
Basi mimi nipo kigoma nilijaribu mpaka leo ni mwanachama wa act wazalendo lakini sikielewi hichi chama changu kinasimamia kitu gani
Nikuombe tu lazima uwe na jukwaa huru litakako kupa nafasi ya kutumia karama zako zote kuijenga nchi yetu karibu sana njoo dm tuwasiliane
 
Watu makini hawaingii kwenye vyama kinyumbunyumbu bila ya kujua falsafra yake,itikadi,misimamo,sera,malengo na dira yake.
Hivyo vitu ni andiko huwezi kuvikuta hapa ,ukivitaka njoo ofisini au ingia dm tupe email yako tutakutumia ,Bado haujafika muda wa kuweka hapa jf
 
Back
Top Bottom