Nipo kwenye mahusiano ila mwanaume wangu ana kipato kidogo. Naombeni ushauri nifanyaje?

Nipo kwenye mahusiano ila mwanaume wangu ana kipato kidogo. Naombeni ushauri nifanyaje?

Wewe ndo hauna akili. Unahisi kisa unamzidi kipato ndo unamzidi kila kitu mpka maono na akili. Umetaja changamoto ya ufugaji lakini umesahau mpesa pia inachangamoto zake na unaweza amka tajiri ukalala maskini.
Msapot katika mawazo yake uone itakuaje so kumkatisha tamaa, otherwise muache ukutane na mabrothermen wakufirisi
Mkuu umenena vyema sana
 
Njia nzuri ya kufanikiwa pia ni kufanya kile upendacho Cha msingi support juhudi zake za ufugaji naamini mtafika mbali
 
Daah, pole sana kwa experience yangu na ujuzi wangu wa biashara kusema ukweli biashara ya ufugaji sio biashara ya kufanya, kwa kifupi huyo mshakaji hana akili ya maisha, hii inaweza kuwa mbaya kwenye mahusiano yenu ya baadae katika uhalisia jamaa anazingua hana dira.
Biashara ya ufugaji sio ya kufanya?. Unazungumzia ufugaji wa aina gani?. Na biashara ipi yakufanya ambayo imekutajirisha?.
 
Vyakula kipengele.
Naongea kama mfugaji mwenye uzoefu wa kufuga kuku chotara.
Nimefuga kuku chotara, na mpaka sasa nafuga kuku wa mayai.

Fuga kuku wa nyama au mayai hao chotara wanunuzi wa jumla wanataka kwa bei ya elfu 10, labda ufuge hao chotara ukiwa na oda maalumu.
 
Cold H2O.....,

ufugaji ni ushamba!!
Mshahara unawapa baadhi ya watu ujivuni sana! Moja ya sekta zenye mpunga ni agri- business! Ifanywe on larger scale, hata ukikufa watoto wanasoma!
 
Mimi pia nimfugaji naona kabisa utanifaa wewe.

Kwamba ufugaji ni issue ambayo haina pesa kama mpesa imebidi tu niishie hapo, niseme maneno machache tu kwako. "wewe hujitambui na kama unajitambua basi huna akili."
🤣Njomba mbona unamchoma kwa maneno makalio hivo
 
Kuna mwanaume, tuna mahusiano tuna miaka miwili Sasa kwenye mahusiano, nampenda natamani tuanze familia.

Kila nikiwaza kipato chake kinanikatisha tamaa mimi. Nina kipato Kwa Sasa hata kusomesha hao watoto tutakaopata lakini nikiwaza vipi kama nikifa ataweza kuwasomesha wanangu?

Au wataishia kayumba tu, nampa mawazo ya biashara hataki anasema yeye interest yake kufuga kwakweli Kwa muonekano wangu na wadhifa wangu sitaki haya mambo yake ya ufugaji Yana Fanya azidi kuwa underground, though kaanzisha.

M-Pesa, binafsi M pesa napenda lakini mambo ya kufuga Fuga sitaki labda ufuge kwaajili ya kula na Sio kuifanya biashara kuu ya kuingiza kipato.

Nikamwambia mimi naku support kwenye upande wa Mpesa na Sio kufuga nunua machine 2 ya NMB na CRDB tengeneza mazingira ya kupiga pesa anasema machine ni bei ghali, tumegombana hadi akaamua anikatie simu.

Yaani yeye anapenda kufuga kuku, mbuzi na ng'ombe mimi nitamuacha jamani!!!

Sasa tutapata fedha kweli dah namuambia mifugo usipokua makini itakufa basi ndo akazidi kukasirika akidai namkatisha Sana tamaa.

Natamani ajue kutafuta pesa kupitia biashara hiyo ya wakala akifungua branch anaweza ku make pesa lakini amekazania mifugo!!!!! Yaani ananichosha na sipendi mawazo yake.
Nenda mapumzikoni Equatorial Guinea ukirudi utakua sawa na mtashauriana vizuri kabisa
 
Lolote laweza tokea wasi wasi ndio akili wanangu nahitaji wasome nahitaji nae awe na kipato Cha kutosha watoto wasiangaike namuona yupo slowly Sana kwenye kutafuta pesa ata saizi nikimpigia nimwanbie tu Nina shida atakuambia pesa Hana Sasa kama tu anashindwa kunisaidia mimi shida ndogo ndogo vipi hao watoto labda hatumi Kwa sababu anaona Kuna kitu ambacho kinaniingizia pesa anaona Nina pesa lakini akiwa kama mwanaume hatakiwi kuangalia kipato changu inabidi a play part yake kama mwanaume.
Wewe ni mjuaji, hayo maisha unayoyaona kwa wenzio kwako hayatakusaidia. Kaa nafasi yako wewe kama mwanamke kwa jamaa na tamani uwe na ndoa yako isiyofanana na wengine. Kaa chini mchunguze kama anafaaa kuwa mume bora kwako, baada ya hapo angalia namna ya kuziba mapungufu yake.
 
Huyu kijana wa kiume angekuwepo humu tungemwambia akae mbali na huyu mwanamke la sivyo ajiandae kufa mapema au ndoa kuvunjika mapema.
 
[
Ndiyo Hawa wanaolewa kila siku baada ya miezi mwezi wapo mitaani wanadanga na kusambaza propaganda za ndoa ngumu.

Very interesting 😎
Huyo kijana wa kiume tumuombee apate mtu amfungue akili amwambie hapo mwanamke amekosa la sivyo ajiandae na mateso.
 
[
Ndiyo Hawa wanaolewa kila siku baada ya miezi mwezi wapo mitaani wanadanga na kusambaza propaganda za ndoa ngumu.

Very interesting 😎
Huyo kijana wa kiume tumuombee apate mtu amfungue akili amwambie hapo mwanamke amekosa la sivyo ajiandae na mateso
 
Mwanamke ambae hana akili kama wewe ni wa kukimbiwa mapema sana! Nashauri jamaa atafute mwanamke mwenye akili na maono ya mbali.

Nipe namba ya huyo jamaa yako nimwambie kabisa bado hajapata mke atafute mwenye maono.
Jamaa atanyanyasika saaana akiingia ndoani na mwanamke kama huyu aloharibiwa akili na life style ya maisha ya wenzie.
 
Jamaa atanyanyasika saaana akiingia ndoani na mwanamke kama huyu aloharibiwa akili na life style ya maisha ya wenzie.
Kabisa! Mwanamke anadhani maono ni kufungua wakala mpesa na tigopesa,..e.tc! Hizi mpesa tigo pesa sijui crdb, nmb wakala zilikua zamani sahizi watu wameshakaba maeneo yenye sehemu inayoweza kukupa nafasi ya watu kufanya transactions za mara kwa mara. Ila kama anataka kufungua na kwenda kupumzika sawa!
 
Back
Top Bottom