Mtunisia mweusi
Member
- Oct 19, 2023
- 95
- 91
Nipo njia panda, je huyu mtoto ni wangu ?
Habari za siku nyingi JamiiAfrica!
Akili yangu imechanganyikiwa sana hapa nashindwa kuelewa cha kuamua juu ya mkasa huu uliyo nitokea.
Miaka mitatu iliyopita nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke sehemu x,baadae tukaacha bila sababu za kueleweka katika huo mwaka.
Sasa mwaka huu wiki moja iliyopita(baada ya miaka mitatu iliyopita) akiwa kwenye bodaboda akanipita sehemu Y na mimi nilimuona.
Punde alirudi pale aliponiona,tukasalimiana na kujuliana hali kidogo.akachukua namba zangu akaenda zake.
Usiku wake alinitafuta kunieleza yafuatayo!
Kwamba miaka mitatu iliyopita alipata mimba yangu,na alishindwa kuniambia kwasababu aliona sina uwezo wa kuihudumia.
Pili:Anasema alikuwa na kansa ya kizazi tangu kipindi hiko kabla sijawa nae katika mahusiano,hivyo hata mimba aliambiwa hatoweza kushika kabisa.Hata hivyo akaniambia alipata mimba na alijijua kuwa na mimba ikiwa na miezi 5(hii inawezekana kweli au napigwa?)
Tatu:Anasema yeye hataki chochote kutoka kwangu ila amenipa taarifa nijue tu kama nina mtoto nae na yeye muda si mrefu anaweza kuondoka duniani kwamba kansa imefikia pabaya.
Nne:anasema nikapime DNA na dogo ili nijihakikishie kama kweli mtoto wangu na gharama atagharamia yeye mwenyewe.
Ajabu maswali ninayo muuliza ajibu kwa ufasaha.
Kwanini hakuniambia kama ana mimba yangu?
Nani alimwambia siwezi kuhudumia mimba? Na sikumwambia kama siwezi?
Mtu anaweza kujigundua kuwa ana mimba baada ya miezi 5? Kwamba mwezi wa 1,2,3,4 hakujijua kama anamimba? Inawezekana hii?
Je wazazi wake hawamjui mwenye mtoto? Mtoto hakuwa na baba na hakusema?
Je huyu mtoto anaweza kuwa wangu kweli au napigwa?
Nikimuuliza maswali muhimu yeye anasema hataki kujua yaliopita anataka nikapime Dna tu na anasema hata ikijulikana mtoto ni wangu hayupo tayari kuniachia dogo na anasema sitompata apoteze maisha.
Samahani kwa uandishi mbovu.Naomba kuwasilisha