Nipo tayari kulumbana (Debate) na yeyote kuhusu chochote

Harmonize mwaka huu lazima apitwe na AI? Na mange kimambi lazima tumuuzie fake porn bongo artists musicians Aya tubishane sasa
Kama kichwa cha habari kinavyosema. yeyote yule, anzisha mada yoyote tulianzishe, wakati wowote.

Karibuni sana. Uwanja wa wazi huu, yeyote anaweza kuchangia na kuingilia mada. Hakuna kanuni rasmi isipokuwa kanuni za JF na za dola ziheshimiwe.
 
Mada ni nini hapo? Harmonize au AI au Mange Kimambi au Fake porn au Bongo artists au Musicians au Aya au tubishane au sasa?
 
MADA: ELIMU , AKILI, & UJINGA

Madam FaizaFoxy. Nikusalimu kwa heshima unayostahili. Kwa Muda mrefu sana kumekua na mkanganyiko katika jamii kuhusu AKILI &ELIMU. Wapo baadhi ambao wamekua wakizitumia terminologies hizi wakifikiri wanamaanisha kitu kimoja lakini baadhi ya wachache wamekua wamekua wakiziona terminologies hizi kuwa tofauti! Kwa uelewa wa kawaida tunaweza kusema kwamba Ili kitu kiitwe ELIMU lazima kwa namna Moja ama nyingine kihusiane na MAFUNDISHO apatiwayo mtu aidha darasani, kanisani, msikitini, madrasa, nyumbani n.k n.k. Lakini Kwa msingi wa AKILI tunaweza kueleza Kwa uelewa wa kawaida kwamba ni uwezo wa binafsi wa asili alio nao mtu pasi na kuihusisha elimu yake!

Madam FaizaFoxy mara nyingi nimekuona hapa jukwaani ukitumia msemo mfupi "huko shuleni ulienda kusomea UJINGA" hasa pale unapotofautiana na member(s) huku. Swali langu ni je mtu anaweza Kwa AKILI yake kabisa kwenda kusomea ELIMU(MAFUNDISHO) ya UJINGA? Ama Mimi nashindwa kukuelewa?

Asante.
 
Kwanza kabisa elewa ukisema elimu mimi nachukulia nini:

Elimu = maarifa ya msingi yanayozingatia ushahidi (Evidence based knowledge).

Akili =Ni kitu tunachozaliwa tunacho, Kiislaam tunakiita "fitrah". Na sote tumepewa na muumba wetu sawa kwa sawa bila mmoja kupendelewa zaidi ya mwengine. Kinachofatia ni sisi tunaifundisha nini akili yetu.

Ndipo linapokuja swali langu maarufu "hivi huko shule mlienda kusomea ujinga?". Nikimaanisha kuwa ujinga tunausomea au tunafundishwa (brain washed) bila kujuwa kuwa unafundishwa ujinga. Ni akili zako za kuzaliwa nazo tu zinaweza kukuokowa kutoka kwenye huo ujinga uliosomeshwa.
 
Kama kichwa cha habari kinavyosema. yeyote yule, anzisha mada yoyote tulianzishe, wakati wowote.

Karibuni sana. Uwanja wa wazi huu, yeyote anaweza kuchangia na kuingilia mada. Hakuna kanuni rasmi isipokuwa kanuni za JF na za dola ziheshimiwe.
Hapo majuzi tumeambiwa sasa Figo za nguruwe unaweza kupandikiza kwa binadamu, Je kina Mohammed wapo tayari kupandikizwa endapo watapata mushkel, hili ni swali
 
tujadilli goli la aziz ki kukataliwa na refa kwenye caf
Mwamuzi ndiye mwenye hukumu ya mwisho uwanjani. Hata tukijadili haisaidii kitu.

Nakumbuka zamani sana, Maradona aliwahi kufunga goli la mkono likawa maarufu sana "hand of God". Mwamuzi akaamuwa ni goli, ikawa ni hivyo.

Kwa wengine chungu, kwa wengine tamu.
 
MADA; TEUZI

Nini mtazamo wako kuhusu teuzi za mama, rais SAMIA SULUHU HASSAN. Je, zina tija kwa taifa? Na ukichukulia gharama nyingi zinatumika kwenye kupanga na kupangua na kuwahamisha mara kwa mara watu wale wale, na gharama za kuwaita mara kwa mara viongozi wa kiserikali kuhudhuria hafla hizo huoni kama kodi za wananchi zinatumika vibaya?
 
Naamini mama Samia yupo kwenye mageuzi (reforms) na kujenga upya (rebuild) mfumo wa serikali namna alioukuta ukiendeshwa.

Mageuzi (reforms) na kujenga upya (rebuild) kokote kule kuna gharama zake lakini zinazotarajiwa ni faida za kudumu kuliko alivyokuta.
 
Kama kichwa cha habari kinavyosema. yeyote yule, anzisha mada yoyote tulianzishe, wakati wowote.

Karibuni sana. Uwanja wa wazi huu, yeyote anaweza kuchangia na kuingilia mada. Hakuna kanuni rasmi isipokuwa kanuni za JF na za dola ziheshimiwe.
Afrika ni TAJIRI sana sana.....lakini watu wake ni MASIKINI sana sana...tatizo liko wapi?
 
Tatizo ni ujinga. Bofya chini ujisomee, nilishawahi kuandika kuhusu hilo:

Back
Top Bottom