Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

God bless
 
Ugenini noma asee nilimtembelea jamaa angu asee yan chakula cha usiku wanakula saa tano usiku...

Siku ya kwanza nilijua labda jion hawali naona chele saa tatu tatu ndio linachambuliwa mama anawasha moto
Haha au walikua wanasubiri ulale
 
Ukweli au niseme nilivyokuwa naona nyumbani. Mara nyingi watu wa Dar hawali sana kama wapo ni wachache sana ambai watakuja kwako na njaa ya tangu asubuhi au ya tangu mchana akiwa anakuja jioni.

Sasa kwa watu wa kijijini au mazingira ya kijijini ni tofauti. Mtu wa kijijini kutokunywa chai ni kawaida ila mchana atakula sana na jioni atakula sana. Mjini mtu akija kukutembelea anaweza akiwa njiani akanywa soda, akala keki nk.

Lakini mtu wa kijijini hawezi kufanya matumizi madogomadogo ya chakula hii inawafanya kutegemea msosi wa mezani. Pia kazi wanazofanya zinawafanya wale sana na wala waspate mavitambi yenu ya mjini.

Nyumbani nilikuwa naona akija mgeni kutoka kijijini mama anahusika ktk kuwawekea chakula yeye mwenyewe Tena alikuwa anawawekea kila mtu ktk sahani yake. Alikuwa hawaamini watoto wake wa kike.

Hii ni moja ya sababu iliyomfanya apendwe na apokee wageni wengi kutoka kijijini kwao.
 

Eee we kiboko [emoji23][emoji23][emoji23] sasa ukienda ugenin unafanyaje?unaigiza au unakula share za watu watatu huo uroho sasa
 
Anaweza kula ubuyu na maji akalala.
Ukikaa nao sana karibu au ukashare rrom na mpare anaweza kukuambukiza ubahiri. Shida ubahiri wao unaenda mpka ktk kula hapo tu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nasikia hawaungi mboga
 
Hayo ndo maisha ya daslam🤣🤣njaa tupu,watu wanakula kuepuka kufa sio kushiba,life gumu sana daslam
 
Kweli kabisa,tatizo maisha ya daslam ni magumu sana,wengi nanaexist hawaishi 🤔
Nyumba yenye furaha ni yenye chakula cha kusaza. Sasa unakuta watu wanapika wali kwenye sufuria za kuchemshia chai! Kweli!!? Unakula hata ukienda toi unatoa kama mbuzi au mtoto!! Nyumba isiyo na chakula cha kutosha haina furaha hata kidogo.
 
Mimi nikienda Shy kutembelea ndugu hua wananiuliza kwanini nakula kwa kuogopa? (hapo utakuta nimejilazimisha kula karibu mara 2 ya kawaida ya uwezo wa tumbo langu)
Watu wa vijijini wanakula share kubwa kuliko wa town nahisi.
 
[emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…