Mkuu mm nimekulia mjini ni mwembamba sana ila ninakula sana, mkate mzima nafuta, chapati nakula NNE kwa kujibana sana, Kuna mgahawa Fulani nakulaga mchana chakula ni expensive ila wananifahamu nauziwa plate mbili za wali au pilau kwa bei ya plate moja ugali nakula plate mbili ndo nishibe, wanaiita msukuma, nameza dawa za minyoo kila mwezi lakini kula kupo palepale, cha ajabu sinenepi hata kidogo nazidi kukonda mpaka najiuliza chakula ninachokula kinaendaga wapi?, mwaka 2012 nilihudhuria semina flan ya mambo HIV njombe wakati wa msosi niliweka mlima wa wali na viazi ndizi Kuna wazungu wakawa wanabishana kama nitamaliza nikasema moyoni hawa hawanijui, nilifuta plate nikanyanyuka nikaongeza plate ya pili nikafuta nikala matunda na maji juu, hahahaha