Nisaidieni kwa wote waliooa na kuolewa

Nisaidieni kwa wote waliooa na kuolewa

Well, una point ila sasa hii ni kwa cluster ya binadamu wachache ambao wana upekee na hata mambo ya ndoa si ya maana au umuhimu kwao, upekee wao unawatenganisha na binadamu wengine, Sasa hawa watanganyika na nishati ya nuclear wapi na wapi? Kwamba aachane na ndoto ya kuvumbua nuclear ili aolewe? Huku ndoto za wengi ni usumbufu tu kwa jamii, kuolewa kunaondoa shida ya kutafuta mume uzeeni akiwa na watoto wasio na baba.
🤣🤣Mkuu usichukulie poa mbona kabinti kangu ni kakimatumbi ila nakapika kaje kugundua kitu🤣
 
Muhimu ni kujua hi yu o ndoto ikitimia inaenda kuwafanya imara pamoja au kiwatenganisha. Aidha, ni muhimu kuzungumza pamoja namna bora ya kutimiza ndoto husika. Mwisho never forget nafasi yako kama mke = kumtii mume
 
Kiukweli akipenda kuolewa ni sawa , asipo penda ni sawa pia ila namfundisha zaidi kujitegemea yeye kama yeye na kujiamini.
Hilo ni la lazima mkuu.

Vijana wengi weshakuwa mlenda mlenda, watu wa kutafuta lawama na visingizio vya kukwepa nafasi zao za maamuzi na majukumu.

Hakuna option ya kumlinda binti na jamii ya vijana aina hii zaidi ya kuhakikisha kuwa anaweza kujitegemea ila asisahau, yeye sio mwanaume, ni mwanamke, mama ajae na mlezi. Nakuelewa maana ninao mabinti.
 
Hilo ni la lazima mkuu.

Vijana wengi weshakuwa mlenda mlenda, watu wa kutafuta lawama na visingizio vya kukwepa nafasi zao za maamuzi na majukumu.

Hakuna option ya kumlinda binti na jamii ya vijana aina hii zaidi ya kuhakikisha kuwa anaweza kujitegemea ila asisahau, yeye sio mwanaume, ni mwanamke, mama ajae na mlezi. Nakuelewa maana ninao mabinti.
Na binti asipo pikwa na baba kimbinu atakuja kuwa mpira wa kona
 
Kuna vijana washenzi mno. Usisahau kumtumia mama yake pia. Mkimlea kwa pamoja na kwa utulivu anavuka salama mpaka anajitambua.
Huyo atalelewa kijeshi tu hakuna cha mama wala nini , maisha ya sasa ni vita vita 😁
 
Huyo atalelewa kijeshi tu hakuna cha mama wala nini , maisha ya sasa ni vita vita 😁
Ok mkuu, kama mama hapatikani nakuelewa. Binafsi nina bahati moja, mama watoto ni mkali yule wa kupiga mpaka mateke mtoto akifanya ujinga, mm naongea mara chache mno ila sasa ikitokea jambo serious tukamchangia mtoto ananyooka kama rula.
 
Ok mkuu, kama mama hapatikani nakuelewa. Binafsi nina bahati moja, mama watoto ni mkali yule wa kupiga mpaka mateke mtoto akifanya ujinga, mm naongea mara chache mno ila sasa ikitokea jambo serious tukamchangia mtoto mbona wananyooka kama rula.
Sipigi mtoto mkuu na mwanangu anajua kibaya na kizuri kwa mipaka yake , ukikaa nae mwenyewe utafurahia tu anatakavyojiamini mbele yako kwa mipaka.
 
Inategemeana!. Unajua watu wengi wanakosea Sana kwenye kufanya maamuzi Hasa nyakati za uchumba, Ndoa ni Maisha nje ya mapenzi. Na Ndoa ni makubiliano Kati ya watu wawili. Hayo malengo yako yanapaswa kujulikana na mwenzie wako Kwanza kabla hamjaoana, Mkashirikishana Uone atasemaje!!!!
 
Mdogo wangu, ukweli mchungu ni huu,kama ni mtu anayekuelewa ama mnaeendana, utatimiza, ila kama hamuendani SAHAU.dadako nilikuwa na ndoto za kuwa mwanasiasa zilizimwa ziii
 
Sipigi mtoto mkuu na mwanangu anajua kibaya na kizuri kwa mipaka yake , ukikaa nae mwenyewe utafurahia tu anatakavyojiamini mbele yako kwa mipaka.
Basi una bahati. Hawa wabantu bila viboko sometimes wanasumbua, hawakupi unachotegemea kutoka kwao. Mm naadhibu mara chache ila mama yao anapiga. Amuachie task arudi akute haijafanywa halafu maelezo hayaeleweki eleweki mtoto anaisoma namba. Ila sasa hivi wamekua, tunaonana nao mara chache.
 
Basi una bahati. Hawa wabantu bila viboko sometimes wanasumbua, hawakupi unachotegemea kutoka kwao. Mm naadhibu mara chache ila mama yao anapiga. Amuachie task arudi akute haijafanywa halafu maelezo hayaeleweki eleweki mtoto anaisoma namba. Ila sasa hivi wamekua, tunaonana nao mara chache.
Mtoto ukimfundisha toka mdogo anaelewa tu , sema mara nyingi wazazi wanakosa mda na watoto wao .
 
“Kila mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke,” msemo huu unaonyesha umuhimu wa mshirika wa maisha katika safari ya mafanikio.

Hali hii pia inatumika kwa mwanamke, kwani nyuma ya mwanamke mwenye mafanikio mara nyingi kuna mume mwenye kuelewa, kumuunga mkono, na kumheshimu.

Ndoa siyo mwisho wa ndoto za mwanamke, bali ni nafasi ya kushirikiana na mwenza ambaye anaelewa thamani ya malengo yake.

Katika ushirikiano wa ndoa, mawasiliano mazuri, kuheshimiana, na kupanga maisha kwa umakini huweza kuleta mafanikio kwa pande zote mbili.

Mwanamke anayetamani kufanikisha ndoto zake anahitaji mume mwenye maono yanayofanana na yake, ambaye atakuwa mshirika wa kweli wa safari yake.

Mume anayejitahidi kumsaidia mkewe, kumtia moyo, na kushirikiana naye katika kugawanya majukumu ya familia na maisha binafsi, huchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yake.

Vivyo hivyo, mwanamke mwenye busara anaweza kuwa chanzo cha nguvu kwa mumewe kufanikisha malengo yake. Kwa hiyo, mafanikio bora katika ndoa hutokana na kushirikiana, kuheshimiana, na kuthamini ndoto za kila mmoja. Ndoa yenye msingi wa upendo na uelewa ni kama daraja la kupita kuelekea mafanikio ya kweli.
Mkuu umetema madini ya uhakika Sana
 
Pole sana, Ukweli mchungu ni kwamba Kwa jinsi jamii yetu ilivyo Hilo unalotaka basi ni kama kubahatisha, ni 1 Kwa 100... Ni aidha uolewe huku unatimiza ndoto zako zozote unazozitaka lakini ukiwa na migogoro mingi isiyokwisha ya ndoa yako au ubahatishe hiyo 1 Kwa 100 niliosema au ukubali kulea watoto peke yako na Kila mmoja na baba yake, ubakie single milele na mwisho ukubali kuwa mchepuko au mke wa pili tena mke mdogo. Nakwambia Ukweli ndugu yangu, jamii yetu Bado au haiko kwenye hiyo hatua ya kufukuzia Kila ndoto unayoitaka.

By the way, umesema ndoto zozote unazozitaka, hapo napo Kuna ukakasi, nachelea kusema kuwa usije kuwa mtu wa ndoto nyingi au kuibua ndoto nyingi zisizo kufanya ubalansi mambo yako.
 
Back
Top Bottom