Nisaidieni kwa wote waliooa na kuolewa

Nisaidieni kwa wote waliooa na kuolewa

Ndoa za nyakati hizi ni watu wawili waliokutana katikati mmoja alikuwa anaelekea mashariki mwingine magharibi, katika hali ya kawaida walipaswa kupishana lakini wakaamua waunganishe safari.

Sasa hawawezi kwenda magharibi na mashariki pamoja, lazima kuna mmoja wapo akubali kuhairisha safari yake na kuongeza nguvu kwenye safari ya mwenzake.

Wewe hii safari ya ndoto yako inaongeza nguvu kwenye safari ya ndoto ya mumeo mtarajiwa au inaigharimu safari yake?
Nmekuelewa shukrani
 
Habari zenu,

Naomba kuuliza swali:

Hivi mdada aliye na malengo na ndoto za kutimiza maishani mwake je, akiolewa anaweza kuzitimiza ndoto zake au ndo milango itakuwa imefungwa mazima ya kufikia ndoto zake na kubadilishwa kuwa mke na mama wa watoto
Habari zenu,

Naomba kuuliza swali:

Hivi mdada aliye na malengo na ndoto za kutimiza maishani mwake je, akiolewa anaweza kuzitimiza ndoto zake au ndo milango itakuwa imefungwa mazima ya kufikia ndoto zake na kubadilishwa kuwa mke na mama wa
Mbavu mbili haziingii kwenye mdomo mmoja, chagua kimoja kuolewa au kupambania ndotozako,
 
Sio kweli, kila mtu anamalengo yake tofauti na kuoa au kuolewa , mwanaume mwenye busara husaidia mke wake kufikia malengo yake kama ambavyo mke mwenye busara anavyoweza kufanya tu🤔
Familia ni conservative institute, ambayo kikawaida mwanamke anaolewa ili kushiriki kwenye kutimiza maono ya mwanaume. Maono ya mwanaume ndio yanatakiwa kuwa maono ya familia.

Moja ya sababu zinazofanya ndoa zisidumu ni hiki ulichokiandika wewe. Tumeifanya familia kuwa liberalism institute., hapa lazima taasisi ya ndoa itaanguka tu.

Mfume dume ndio perfect kwa maisha ya ndoa. Kama tumeamua kwemda kwenye hizi mambo za 50/50 sijui feminism basi lazima tukubaliane na ukweli kwamba ndoa ni taasisi ambayo ishapitwa na wakati
 
Ndoto za binti yangu zije zikatishwe na kiazi mmoja 😅😅 hayo mambo yalishapitwa na wakati mkuu, ndio maana leo hii raisi wako ni mwanamke na unabaki kununa tu😄
 
Ndoto za binti yangu zije zikatishwe na kiazi mmoja 😅😅 hayo mambo yalishapitwa na wakati mkuu, ndio maana leo hii raisi wako ni mwanamke na unabaki kununa tu😄
Nafikiri haujanielewa mkuu. Ni hivi ndoa ni taasisi ambayo imesukwa kwenda sambamba na mfumo dume. Maono ya mwanaume ndio maono ya familia.

Kwaiyo lazima mwanamke achague kimoja kama anataka ndoa aachane na mambo ya 50/50 au feminism na kama anataka 50/50 aachanr na suala la ndoa

Uzuri ni kwamba kuoa/kuolewa sio lazima, kwaiyp mwanamke anaweza kuchagua kimoja. Abaki single kupambania ndoto zake au aolewe na kuwa mshirika kwenye ndoto za mwanaume.

Marriage is not for all women, if you think your daughter's dream is too big to sacrifice it for marriage then you can advice her to be single.
 
Asante
 
Ndoto za binti yangu zije zikatishwe na kiazi mmoja 😅😅 hayo mambo yalishapitwa na wakati mkuu, ndio maana leo hii raisi wako ni mwanamke na unabaki kununa tu😄
Mkuu, sasa hivi mabinti zetu wana ndoto, ila kama tunataka jamii yenye amani, maadili na utulivu katika ndoa hizi ndoto zao ni lazima zisiwahamishe kwenye nafasi zao. Kama binti yako ni daktari, udaktari wake usimbadili akawa mwanaume, maana hili ndo tatizo lililopo. Wanawake wanageuka wanaume.
 
Tulia Kwanza umri huo bado una mihemko mingi Sanaa..
Labda Kama una bahati mtu wako ni 40+yrs anaweza kukucontrol Kama wewe hutakuwa msumbufu..lakini Kama ni kijana mwenzio tulia utapoteana
Kuhusu kutimiza ndoto labda Kama ndoto gani maana Afrika kutimiza ndoto ni mlolongo mrefu saana.
Umetoa maelezo mazuri kabisa.💪
 
Ukishamuoa tu hizo ndoto atataka umtimizie wewe ndugu yangu we mwache atimize kwanza kama ataweza si wanasema haki sawa yani wanaweza kila kitu we msapoti kwa kummiminia mishahawa tu mzee baba maana huo pia ni mchango tosha
 
Sio kweli, kila mtu anamalengo yake tofauti na kuoa au kuolewa , mwanaume mwenye busara husaidia mke wake kufikia malengo yake kama ambavyo mke mwenye busara anavyoweza kufanya tu🤔
Tatizo tukiwasaidia wake zetu kutimiza ndoto zao baadae hutugeuka na kusema sisi sio type zao na wanaanza kutembea na co-workers wao
 
Asikudanganye mtu, kuolewa ni kwenda kutimiza ndoto za mwanaume. Which is very understandable, kuwa Mume ndio kichwa cha familia, ndoto zake ni ndoto za familia hivyo anatakiwa kupewa support.

Sasa kwakuwa una ndoto zako, omba Mungu na ujitahidi kuchagua mume ambaye ndoto zake ni pamoja na kutimiza ndoto za mkewe, au ambaye ameshatimiza ndoto zake amebaki kutimiza za wengine, au yuko mwishoni kutimiza ndoto zake.

Ushauri wangu, olewa na mwanamume mkubwa 40+ Mara nyingi hawa wanakuwa wameshafahamu muelekeo wa ndoto zao au wengine wametimiza au wanaelekea kutimiza. In return, mpende, mheshimu and be there for him forever, sio ujipata uanze kusumbua.

Yes, namaanisha kuna watu shida yao pekee duniani iliyobaki ni kupata mtu wa kumpenda tu.
 
Unaolewa ili utimize ndoto ya kuwa mama kwa watoto wako, mke kwa mume wako na mlezi. Ndoto nyingine yoyote nje ya hapo ni UTAPELI KWA MUMEO NA JAMII.

Lolote ufanyalo linapaswa kulenga kutimiza hilo nililolisema, Bahati mbaya sana wanaume tumekuwa dhaifu kusimamia hili matokeo yake tumewaachia nyinyi mjiamulie ndoto zenu huku tukitegemea huruma na misimamo yenu ndo ilinde ndoa.
Marie curie ,leo hii ungekuta angechagua kupuuzia ndoto zake ,nishati ya nuclear na matibabu ya saratani kupitia mionzi ingekua ni ndoto🤔
 
Habari zenu,

Naomba kuuliza swali:

Hivi mdada aliye na malengo na ndoto za kutimiza maishani mwake je, akiolewa anaweza kuzitimiza ndoto zake au ndo milango itakuwa imefungwa mazima ya kufikia ndoto zake na kubadilishwa kuwa mke na mama wa watoto
Naam. Waweza timiza ndoto zako ila zingine zaweza kuweka ndoa yako matatani.
 
Marie curie ,leo hii ungekuta angechagua kupuuzia ndoto zake ,nishati ya nuclear na matibabu ya saratani kupitia mionzi ingekua ni ndoto🤔
Well, una point ila sasa hii ni kwa cluster ya binadamu wachache ambao wana upekee na hata mambo ya ndoa si ya maana au umuhimu kwao, upekee wao unawatenganisha na binadamu wengine, Sasa hawa watanganyika na nishati ya nuclear wapi na wapi? Kwamba asiolewe ili asiachane na ndoto ya kuvumbua nuclear? Huku ndoto za wengi ni usumbufu tu kwa jamii, kuolewa kunaondoa shida ya kutafuta mume uzeeni akiwa na watoto wasio na baba.
 
Back
Top Bottom