Nisaidieni kwa wote waliooa na kuolewa

Nisaidieni kwa wote waliooa na kuolewa

Una ndoto gani binti ambazo unataka kuzitimiza nje ya ndoa?
Labda kuwainua wadogo zake kiuchumi, mfano mimi nilikuaga na demu wangu sasa yeye alikua na sijui Malengo au uelewa mdogo au Wazazi wake wajinga sasa yeye alikua anafanya kazi Mshahara wake 250k nikashangaa anacheza mchezo ili kumjengea Nyumba Mama yake, na wakati huo Mama yake yupo ndani ya ndoa na Mama nikajifunza kitu ndiyo Maana Wanawake wengi wanajiuza.
 
Habari zenu,

Naomba kuuliza swali:

Hivi mdada aliye na malengo na ndoto za kutimiza maishani mwake je, akiolewa anaweza kuzitimiza ndoto zake au ndo milango itakuwa imefungwa mazima ya kufikia ndoto zake na kubadilishwa kuwa mke na mama wa watoto
Unaolewa ili utimize ndoto ya kuwa mama kwa watoto wako, mke kwa mume wako na mlezi. Ndoto nyingine yoyote nje ya hapo ni UTAPELI KWA MUMEO NA JAMII.

Lolote ufanyalo linapaswa kulenga kutimiza hilo nililolisema, Bahati mbaya sana wanaume tumekuwa dhaifu kusimamia hili matokeo yake tumewaachia nyinyi mjiamulie ndoto zenu huku tukitegemea huruma na misimamo yenu ndo ilinde ndoa.
 
Tujitafute kwanza au unasemaje😂tusije kuwa mama wa ndani
Kwani ukiwa ndani ya ndoa utakatazwa kujitafuta? Yani ukijaribu kujitafuta kwanza ndiyo utake kuolewa ndoa utaikosa ila utaipata kwa kufosi au kuishia kuzaa na mume wa mtu au utakuja kuwa mshangazi na kulea Vijana, Kwa Tanzania ya sasa hivi Binti ukichelewa sana kuolewa kumpata mtu wa vingezo vyako ni ngumu, mfano una umefikisha miaka 34 unazani mumeo utakae mpata ni wa umri gani ?
 
Muhimu nikupata mtu ambae ataku-support ndoto zako na malengo .
Na pia tabia yako ni muhimu usije ukatumia njia hiyo kuharibu ndoa.

Kama huyo mwanaume wa kusupport kwenye malengo yako humuoni na umewia kutimiza ndoto zako ni bora usiolewe kwanza.

Haya mambo ndio yakujadili kipindi cha uchumba au urafiki.
SIo kuwaza kunyanduana tuu.
Mwanaume anaweza kuchangia kipi kwenye kufikisha malengo Yangu?!
 
Unaolewa ili utimize ndoto ya kuwa mama kwa watoto wako, mke kwa mume wako na mlezi. Ndoto nyingine yoyote nje ya hapo ni UTAPELI KWA MUMEO NA JAMII.

Lolote ufanyalo linapaswa kulenga kutimiza hilo nililolisema, Bahati mbaya sana wanaume tumekuwa dhaifu kusimamia hili matokeo yake tumewaachia nyinyi mjiamulie ndoto zenu huku tukitegemea huruma na misimamo yenu ndo ilinde ndoa.
Vipi kama nikitimiza ndoto na baadae nije kumsaidia majukumu huoni ntakuwa namnufaisha pia
 
Kuolewa si kikwazo kwa mwanamke kufanikisha ndoto zake, bali inategemea aina ya mwenza alionaye, juhudi zake binafsi, na jinsi anavyosimamia majukumu ya ndoa na maisha yake.

Mwenza anayemuunga mkono, mawasiliano mazuri, na mipango thabiti vinaweza kumwezesha mwanamke kufanikisha ndoto zake hata akiwa mke na mama.
Ni ngumu kufanikisha ukiwa mama tyr
 
What's makes think they are great thinkers?!
Maswali unayouliza yana utoto mwingi .

Unaonekana. Wewe haujui nini maana ya ndoto

Utaishia kuzalishwa au Kuwa abortion mothers.

Take time to think is the source of power .
 
Maswali unayouliza yana utoto mwingi .

Unaonekana. Wewe haujui nini maana ya ndoto

Utaishia kuzalishwa au Kuwa abortion mothers.

Take time to think is the source of power .
Then you don't know what great thinkers are🤌
 
Vipi kama nikitimiza ndoto na baadae nije kumsaidia majukumu huoni ntakuwa namnufaisha pia
Ndoa za nyakati hizi ni watu wawili waliokutana katikati mmoja alikuwa anaelekea mashariki mwingine magharibi, katika hali ya kawaida walipaswa kupishana lakini wakaamua waunganishe safari.

Sasa hawawezi kwenda magharibi na mashariki pamoja, lazima kuna mmoja wapo akubali kuhairisha safari yake na kuongeza nguvu kwenye safari ya mwenzake.

Wewe hii safari ya ndoto yako inaongeza nguvu kwenye safari ya ndoto ya mumeo mtarajiwa au inaigharimu safari yake?
 
Back
Top Bottom