Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Npashe la leo.
Kwa wengi wa waliozaliwa mijini, hawaijui adha ya kupika kwa kuni mamilioni ya akina mama, wanawake, mabibi zetu, mashangazi zetu, wake zetu, watoto wetu, wapenzi wetu, au kwa kifupi wanawake wa Tanzania, wanaoteseka kwa kupikia kuni.
Kufuatia kupikia kuni kwa muda mrefu, wakinamama hawa wanaathirika, kutokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa inayoitwa, tungomotaka, kwa macho yao kuwa mekundu kama yamevia damu. Kule Mwanza ni Shinyanga, mwaka 1976, wabibi hao wakatuhumiwa kuwa huo wekundu wa macho yao ni wachawi, hivyo wengi waliuliwa kikatili.
Serikali ya Mwalimu Nyerere ikaingilia kati, kukomesha mauaji hayo, hivyo washukiwa wa mauaji ya vikongwe walikamatwa na kuhojiwa kwa mbinu za mateso sana, matokeo yake, watuhumiwa wawili wa mauaji hayo wa Mwanza Masaga Makhula Mazenganuka, na Isaack Ngw’anaMkoboko, walipoteza maisha, hivyo Mwalimu Nyerere akakasirika sana, kwanini watu wafe mikononi mwa polisi?. Siku hizi nobody cares!.
Nyerere alisafisha kuanzia kwa msaidizi wake mkuu Rashidi Kawawa, Mawaziri akiwemo Mwinyi walijiuzulu. Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama walistaafishwa. Watendaji wa Mkoa wa Mwanza, RPC, RSO, OCD na DSO, wote wakapandishwa kizimbani, kesi ya Mauaji Mwanza ilipoanza kuunguruma, ndipo nikajua kumbe Baba alikuwa nani!.
Huo ndio ulikuwa uwajibikaji enzi za Nyerere, siku hizi watu wanakufa mikononi mwa polisi na sio tuu hakuna hatua zinazochukuliwa, bali hakuna hata uchunguzi!. Kuna mtu amewahi kusikia maendeleo yoyote ya uchunguzi shambulio la Tundu Lissu?, yaani Tundu Lissu yupo hata kuitwa polisi kuandika tuu maelezo, hajawahi kuitwa!, kigugumizi hiki kinawaambia wenye akili, wahusika ni kina nani!, sasa uchunguze nini ili iweje?.
Tulirudishwa kijijini usiku usiku kwa Landrover Defenda 109 na hapo sasa ndipo nikashuhudia adha ya kupikia kwa kuni aliyokutana nayo Bibi yangu. Kiukweli ni mateso!.
Hali ya nishati ya nchini Tanzania, sio nzuri, watu 22,000 wanapoteza maisha, kila mwaka kutokana na magojwa ya upumuaji yanayosababishwa na moshi wa kupikia kwa kuni na mkaa, hivyo kufuatia hali hiyo, kipaumbele cha kwanza kwenye sekta ya nishati, ni kuhakikisha gesi inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu na inafika kwenye kila nyumba, hivyo kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Kitendo cha Rais Samia, kulivalia njunga hili jambo la nishati safi ya kupikia, ni ukombozi mkubwa sana kwa wanawake wa Tanzania, japo kupika kibiashara sio kazi ya wanawake ni kazi ya wote na haswa wanaume hivyo ukombozi huu pia unawahusu.
Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, imeamua kumuunga mkono Rais Samia, kwenye kampeni ya nishati bora ya kupikia, kwa kuanza kusambaza gesi ya kupikia, katika vituo vyake vyote zaidi ya 100 nchini kote, ili kufanikisha ndoto ya Rais Samia, kufikia mwaka 2030, Watanzania wote wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
Uamuzi huo, umetangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Mamadou Ngom wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza wiki hii kwa uzinduzi wa kituo cha mafuta cha TotalEnergies Magomeni Makanya, ile njia ya Tandale Uzuri.
Mamadou Ngom amesema, kufuatia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais Samia, kuhamasisha matumizi ya nishati salama ya kupikia, kwa vile TotalEnergies, ndio kampuni inayoongoza Tanzania kwa idadi ya vituo vya mafuta, TotalEnergies, imeamua kumuunga mkono Rais Samia kwenye suala la nishati bora ya kupikia, hivyo sasa itasambaza gesi ya majumbani, katika kampeni iitwayo “Jiko Bomba, Pishi Pambe”.
Hatua hii ya TotalEnergies, sio tuu inapaswa kupongezwa, bali kuungwa mkono na wadau wengine wote wenye mapenzi mema na taifa letu, mdau mkuu nambari moja akiwa ni serikali yenyewe.
Japo Kenya wana Bandari ya Mombasa na wanaweza kuagiza gesi ya kutosha, lakini ukisimama mpaka wa Namanga, ukashuhudia idadi ya malori ya gesi kutoka Tanzania kupeleka gesi Kenya utashangaa na kujiuliza kama wenzetu wana uhaba!, jibu ni hapana, Wakenya wengi zaidi wanatumia gesi hivyo demand ni kubwa, wakati Watanzania wengi zaidi wanatumia kuni na mkaa!.
Mfanyabiashara wa Tanzania, mwenye Taifa Gas, akaiona fursa ya gesi Kenya, sasa amejenga kiwanda cha Taifa Gas Kenya na kuwahudumia jirani zetu Wakenya, huku Watanzania tukiendelea kuhangaika na kuni na mkaa!. Fursa, zina utaratibu wa kuwa grabbed, usipo changamkia wewe, wenzetu wanazichukua, sasa Wakenya wengi zaidi wanatumia gesi yetu wakati sisi wenyewe wenye gesi, tunapikia kuni na mkaa!.
Sababu ni moja tuu, majiko ya gesi ni gharama na gesi ni ghali kuliko mkaa, kuni ni bure, ughali huu unachangiwa na kodi na tozo mbalimbali, hivyo kama serikali yetu iko serious Watanzania watumie gesi, ifanye yafuatayo….
Mungu Ibariki Tanzania
Jumapili Njema
Paskali

- Serikali ifute kodi zote kwenye majiko ya gesi, mitungi ya gesi na gesi yenyewe. Kuna ubaya gani serikali ya Mama Samia, ikaondoa kodi zote kwenye ikiwemo VAT kwenye majiko ya gesi na gesi ya kupikia?. Mbona kwenye computes tumeondoa kodi?!. Hawa Watanzania wenzetu elfu 22, wanaokufa kila mwaka kwa matatatizo yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, maisha yao yangeokolewa kwa matumizi ya gesi na umeme
- Serikali itambulishe ruzuku ya majiko ya gesi na mitungi ya gesi, kama ruzuku kwenye zana za kilimo na pembejeo ikiwemo mbolea. Enzi za Mwalimu, baadhi ya bidhaa muhimu zikiwemo, mbegu, mbole na pembejeo za kilimo, zilifanywa bei nafuu kuliko hata bei halisi kwa kupewa ruzuku ya serikali ili wananchi wamudu gharama. Kuna wakati wa uhaba wa maji, Tanesco ilikuwa inatumia gharama kubwa kuzalisha umeme wa gesi na mafuta na kuuza kwa bei ndogo kama ya umeme wa maji ili kutowabebesha wananchi mzigo mkubwa wa gharama
- Wafadhili mbalimbali wahamasishwe kujitolea kufadhili majiko na mitungi ya gesi kwa wasio na uwezo, wakiwemo TASAF iingize program ya kufadhili majiko, mitungi na ruzuku ya gesi kwa kaya masikini katika program yao ya kunusuru kaya masikini.
- Tutunge sheria ndogo, by laws, kulazimisha taasisi zote za watu wengi, mashule, vyuo vya kati, vyuo vikuu, na mahoteli ni lazima kutumia gesi ili kuokoa mazingira na sheria za ujenzi zijumuishe njia za kesi kama ilivyo kwa mabomba ya maji, umeme na mawasiliano, watu walipe bili za gesi kama maji na umeme.
- Ziwekwe tozo maalum kwa vibali vya mkaa, na ziwekwe faini kali kwa uharibifu wa misitu kutafuta kuni na uchomaji mkaa bila vibali. Kama Tanesco iliweza kuuza umeme kwa bei ya chini, na enzi za Mwalimu kulitolewa ruzuku kwenye bidhaa muhimu, na enzi za JPM, gharama za kuunganishwa umeme wa REA, zilikuwa ni Shilingi 27,000 tuu, na tumeshuhudia hadi vijumba vya nyasi, vimeunganishwa na umeme, hili linashindikana vipi kwenye gesi?.
Mungu Ibariki Tanzania
Jumapili Njema
Paskali