Niskilizeni mimi, wachezaji hawa yanga waachwe/wabaki

Niskilizeni mimi, wachezaji hawa yanga waachwe/wabaki

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu binafsi nimeskia sana swala la mashabiki kudai wachezaji wetu baadhi waachwe na wengine wabaki .

Ni sawa ..
Lakini shida tunasahau sana na kukurupuka sana bila kukumbuka na kufuatilia kwa umakini .
Well wafuatao yanga tunapaswa kuwaacha ..!

1. Skudu Makudubela
Huyu ni mfanyakazi hewa na hana anachofanya. Sio vibaya akiachwa sababu ni mgeni na nafasi yake ikajazwa na wings mwengine wakigeni au striker kuliko kumuacha musonda, tutaumia.

2. Zawadi Mauya
Katusaidia sana kipindi kile yanga inajitafuta lakini lazima tukubali huyu muda wake umeisha, ameshapewa nafasi sana na ameshindwa kuitumia, amekuja Mkude na amemkuta na ameingia kwenye mfumo

Huyu zawadi yeye bado tu!
Aachwe na nafasi yake tupate kiungo mzawa, kama yule wa coastal Gwalala ooh boy! Hata kagoma anatufaa.

3: Metacha Mnata
Huyu muda wake anaupoteza bure na atafute team nyingine kwa sasa sidhani kama atabaki. Amepewa sana nafasi na kocha lakini tumeishia kuambulia maumivu tu, hafai aende tupate kipa mwengine mzawa wa kumsaidia diarra na msheli. Kipa wa prison yona Amos anafaa sana sidhani kama kuna ugumu kumpata!

5. Joyce Lomalisa Mutambala

Huyu umri umesogea na amekuwa ni injury prone! amechoka kwa sasa! Yeye mwenyewe hataki kuongeza mkataba na ameomba mwishoni wa msimu aende! Sioni sababu ha kubembelezwa aende, uwezo wake pia umeshuka siku nyingi tu katusaidia sana lakini goodbye! Lamine imoro (something like that) anafaa sana na hana team kwa sasa yupo tu kotoko pale kwao Ghana anapasha pasha , tuchukue mali hiyo..!

WA KUBAKI

Kennedy Musonda
Huyu bado tunamuhitaji sana hasa kimataifa , wanaosema aachwe wamepotoka hata Gamondi mwenyewe atawashangaa! Kwa maelezo zaidi aulizwe beki Khuliso Mudau..!

Clement Mzize
Huyu bado ana msaada mkubwa kwetu, itachukua muda kupata mchezaji mzawa kama Mzize. Tukumbuke yeye ametoka mtaani kijiweni (bodaboda) na kwenda straight Yanga! Its not easy boy, hata kama alianza Yanga B bado sio rahisi. Naskia kaongeza mkataba japo sina uhakika

DANGER ZONE (WA KUJITAFAKARI)

1. Kibwana Shomari
Bwana mdogo akaze sana sana, upande wake mgumu sana .
Kama hata pengo la yao lilizibwa na Fred ambaye wore tunajua ni CB basi ni warning sign kwa kibwana , akaze sana hasa mazoezini nadhani jeraha lake alishapona..

2; Gift Fred
Huyu naye kwa sasa angalau amekuwa akipata nafasi kama beki wa kulia lakini yeye siyo RB Bali aliletwa kama CB , kwahiyo ajitafakari Licha ya kwamba upande ule wa kulia aliziba vizuri sana wakati wa pengo ..

3; FARID MUSSA MALICK
Kipenzi cha wanayanga kwa sasa amepotea! Kipenzi cha Nabi kwa sasa amepotea kwenye zama za Gamondi!
Nadhani quality ya kikosi ndiyo inamuhukumu kijana! Faridi ajitahidi vinginevyo itakuwa ngumu kumvumilia sana pale Yanga.

4; BAKARI NONDO MWAMNYETO
Ndiyo huyu naye amekuwa akifanya makosa ya Mara kwa Mara Captain wetu amekuwa mzito kwenye maamuzi sehemu za hatari, Kiwango chake kimekuwa cha kutabirika sana. Haishangazi sana kwa sasa Job na Bacca wakicheza Mara nyingi dhidi yake.!

Ushahidi mzuri kwa siku za hivi karibuni ni match ya juzi dhidi ya Simba, captain alizembea kwa kweli na kusababisha goli.

Its Pancho
 
Scudu ni mfanyakazi hewa.
Huyu nadhani walituletea ili kutuburudisha
They nicknamed him waziri wa raga sio kucheza ,
Na huyu okra ilibidi aanze leo ila game ndio hivyo wameghairi.

Nimeskia yanga wanafikiria kumleta lilepo huko ufaransa team ipo hatarini kushuka daraja.
 
Huyu nadhani walituletea ili kutuburudisha
They nicknamed him waziri wa raga sio kucheza ,
Na huyu okra ilibidi aanze leo ila game ndio hivyo wameghairi.

Nimeskia yanga wanafikiria kumleta lilepo huko ufaransa team ipo hatarini kushuka daraja.
Mechi wamecancel?
 
Wachezaji wa kuondoshwa haraka Yanga bila kujali na sitatoa sababu ni Jonas Mkude pamoja na Lomalisa Mutambala.

Jonas ni kirusi, hafai kubaki la sivyo tutakuja kulaumiana.
Bila shaka nyie wa dar mnawajua vizuri
Hebu tuambie kwanini aachwe bwana mkude?

Au ni pandikizi?
 
Wachezaji wa kuachwa kutokana na viwango vyao kutoridhisha ni Skudu, Kibwana, Mauya, Sureboy (Namkubali sana lakini aende), Mzize yani huyu ndio sitaki hata kumsikia.
Nkane pia atuache imetosha.

Wa kujirekebisha ni
1. Mwamnyeto (Huyu namkubali mno ila wenge limezidi, atatugharimu at this rate)

2. Musonda, siku hizi anajitahidi ila hayuko aggressive kama stiker, aongeze juhudi.

3. Kibabage, hana utulivu. Aache kutafuta sifa binafsi acheze kama timu, huku mwishoni naona kajirekebisha kiasi.
 
Wachezaji wa kuachwa kutokana na viwango vyao kutoridhisha ni Skudu, Kibwana, Mauya, Sureboy (Namkubali sana lakini aende), Mzize yani huyu ndio sitaki hata kumsikia.
Nkane pia atuache imetosha.

Wa kujirekebisha ni
1. Mwamnyeto (Huyu namkubali mno ila wenge limezidi, atatugharimu at this rate)

2. Musonda, siku hizi anajitahidi ila hayuko aggressive kama stiker, aongeze juhudi.

3. Kibabage, hana utulivu. Aache kutafuta sifa binafsi acheze kama timu, huku mwishoni naona kajirekebisha kiasi.
Mzize Aendelee Kuwepo Ana Improve Kwa Kasi.
 
Back
Top Bottom