Niskilizeni mimi, wachezaji hawa yanga waachwe/wabaki

Niskilizeni mimi, wachezaji hawa yanga waachwe/wabaki

Nitashangaa Skudu akiendelea kubaki Yanga msimu ujao.Jezi no.6 apewe Pacome.

Metacha Mnata hatakiwi tena kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga.

Denis Nkane ni mchezaji wa timu ndogo,hana mentality ya kupigania namba timu kubwa.

Zawadi Mauya namkubali sana but imekuwa bahati mbaya hajaweza kukidhi mahitaji ya Yanga.

Kama itatokea timu nje ya nchi na kumuhitaji Nondo napendekeza auzwe.Sivyo,basi abaki lakini bila kuwa regular starter kama ilivyo sasa.Ana makosa mengi ya hatari ingawa ndo beki anayeweza kupiga pasi zenye macho zinazo vuka mstari wa ulinzi.Pia anauwezo wa kukokota mpira umbali mrefu.

Lomalisa pia no problem akiondoka.Ameshatumika sana nadhani pia umri unafanya aumie mara kwa mara.
 
Wachezaji wa kuachwa kutokana na viwango vyao kutoridhisha ni Skudu, Kibwana, Mauya, Sureboy (Namkubali sana lakini aende), Mzize yani huyu ndio sitaki hata kumsikia.
Nkane pia atuache imetosha.

Wa kujirekebisha ni
1. Mwamnyeto (Huyu namkubali mno ila wenge limezidi, atatugharimu at this rate)

2. Musonda, siku hizi anajitahidi ila hayuko aggressive kama stiker, aongeze juhudi.

3. Kibabage, hana utulivu. Aache kutafuta sifa binafsi acheze kama timu, huku mwishoni naona kajirekebisha kiasi.
Mzize unanikosea sana bibie hakuna striker mzawa zaidi ya Mzize hapa Tanzania
 
Dada yangu Nifah najua unajua Kuna kitu inaitwa long term plan tuna invest kwa Mzinze utakuja kuelewa baadae kama viongozi watamtunza Mzinze.
Akija kuwa dhahabu akasaidia timu pakubwa au akauzwa pesa ndefu ya kuwanunulia tusiowaweza kuwamudu kwa sasa hutaelewa hili somo.

Hao unaowataka kwa sasa hatuna pesa hiyo tusijidanganye.
GSM hawezi kujenga uwanja na kununua wachezaji wa mmoja bilioni 2. I'm talking about clinical striker, yule Mayele ilitokea bahati mchezaji bei rahisi kuwa kiwango kile. It's one in a million in life time.

Yanga sio chuo cha malezi, ndio maana nimesema hana hadhi ya kucheza Yanga. Tunahitaji wachezaji wa kuleta mchango wa makombe kwenye timu.

Unafikiri angekuwa Mayele pale si tungekuwa nusu fainali?
Tunakumbushana tu.
Sasa Mzinze anatakiwa Wydad Casablanca na Kaizer Chiefs kwa bei gani?
Umemuona kijana fainal ya ngao ya jamii na mechi ya CAF CL dhidi ya Vital O?

View: https://youtu.be/BuTeLHQniS8?si=5nOTnjunPigAZ8vl
CC: Kosugi ngara23 Its Pancho Dr Matola PhD
 
Kwa maoni yangu mimi,
Wachezaji wa kuondolewa pale ni hawa wafuatao,
1. Sureboy
2. Mauya
3. Skudu
4. Kibwana
5. Kibabage (huyu wenge ni kubwa sana)
6. Metacha( yaani huyu ndo hafai kabisa)
7. Farid
8. Nkane
9. Lomalisa

Wachezaji ambao nadhani tuwape muda ni hawa wafuatao;-
1. Mzize
2. Mwamnyeto
3.Guede
4. Musonda

Wachezaji wa ndani wa kuwaleta msimu ujao pale Jangwani ni hawa;-
1. Yahaya Mbegu
2. Awesu Awesu
3. Lameck Lawi
4. Kelvin Kijili
5. Matheo Anthony
Katika hii list, Simba alipita na watatu, haha
 
Back
Top Bottom