Asante mwananchi kwa bandiko lako ya kuhusu maboresho ya timu, binafsi naona kwa hatua iliyofikia Yanga kwasasa inatakiwa isiwe na wachezaji wanaopishana sana viwango. Yanga msimu ujao wanataka kuprove watu kuwa walioonewa kuishia robo fainali ya klabu bingwa, wanatakiwa kushiriki AFL kama haitofutwa ( kuna tetesi kwamba wajumbe wamekataa CAFCC kufutwa ni bora ifutwe AFL) bado inabidi itete mashindano ya ndani, hivyo kutakuwa na mashindano mengi sana kushiriki hivyo kunahitajika uwiano uliokuwa sawa kati ya first eleven na wachezaji waliopo benchi. Kama wachezaji wanacheza timu kubwa ya Yanga lakini inafungwa na APR au Ihefu hawana maana.
Nkane, Faridi, Ngushi, Mauya, Sureboy, Metacha, Skudu, Mwamnyeto sijui ana shida ipi kwanza kujiamini kumepungua sana. Akipata mpira ni kubitua tu na akisema atoe pasi basi kachoma. Kwenye uwezo wa kukaba nako kapwaya kabisa kama sio kusababisha penati basi kashindwa ku win mpira. Nafasi ya Mwamnyeto inahitaji mtu.
Ma gap mengi kwa asilimia kubwa tunatakiwa tuyazibe kwa wachezaji wa ndani ukizingatia kuwa wachezaji wa nje ambao wanaostahili kupewa mkono wa baibai ni wachache sana binafsi naona ni Skudu na Lomalisa. Mzize ana tetewa ila ni moja ya wachezaji waliochangia kuichelewesha Yanga. Mechi dhidi ya Azam ilikuwa sio ya Yanga kupoteza ila kaipotezea Yanga. Mechi zote mbili dhidi ya Mamelodi Mzize kaikosesha Yanga nafasi ya nusu fainali hivyo kama ana bakishwa basi aje mtu wa kumpa changamoto hata akiwa usajili wa ndani maana Mzize sio wa kumtegemea kabisa.
Musonda mzee wa kazi huyu ukimpanga pembeni atakupa kinachostahili kwenye mechi ngumu yeyote. Anakaba na kufanya mashambulizi ni aina ya wachezaji wanaopendwa na Gamondi kama ilivyo kwa Max Nzengeli. Hivyo Musonda hastahili kuondoka.
Kazi kubwa inayofanywa na daktari bingwa wa upasuaji (Aucho) anatakiwa apate mtu wa kumsaidia kwasababu kuna kuumia na kadi na kuchoka kwa kutumika sana. Mkude alifanya kazi nzuri kwenye leg mbili za Mamelodi na ilikuwa ni sapraizi kwa wengi ila hili eneo linabidi liongezwe ingizo lingine kwavile sureboy kalishindwa hivyo imeshapunguza idadi ya viungo wenye ubora.
Yangu ni hayo