Sasa mimi ni mpenzi mkubwa wa Nissan, tema Murano. Ninaimiliki ila imenitesa sana sio kidogo ila imekuja kutulia hadi nashangaa.
Ipo hv, nilipoinunua hii gari sikupata shida. Siku moja nikampa fundi anifanyie service ya oil ya gear box na Engine. Fundi akanunua oil ya Puma(manjis Arusha) badala ya Matic J(Murano inatumia matic). Akaweka hiyo oil na mimi sikujua. Baada ya kama mwezi mmoja tu gia ya rivers ikaanza kuwa haikubali gari ikipata moto. Yani ilianza kelele hapo. Mimi sikujua shida ni nini. Gari ilinisumbua sana kama miezi 4-6 nateseka tu. Mara ikaanza kuwa inazima tu yenyewe, mara inaua coil, mara betri inakufa kwa muda mfupi. Nimetembeza karibu garage zote Arusha, niliwasiliana na mafundi wa dar nao vilaza tu. Diagnosis machine nazo zinataja codes ambazo hata uki Google inaeleza vingine. Nikibadilisha control box, coil zote, pulgs zote bila muafaka. Hadi pump ya mafuta niliweka mpya ila gari hamna kitu. Nilitokea kuichukia sana. Nilibadili hadi camshaft sensor, crankshaft sensor, oxygen sensor ila bado hamna kitu.
Katika kutafuta msaada nikakutana na fundi mmoja akaniambia hii gari imeua sensor kwenye gia box na imewekwa oil ambayo sio yake. Akaniambia tatizo hapo ni gear box tu hmhamna kingine, nilishindwa kumuamini ila mwisho wa siku ilibidi nimuamini. Akaniambia nimpe hizo sensor zote coil na vifaa vya zamani avirudishie vyote halafu tuagize gear box nyingine(alinishauri kuwa gear box haifai kutengeneza) wakuu nialiagiza gear box, akafunga, akarudisha vile vifaa vyake vya zamani vyote. Hadi lei gari imetulia na sikuamini kama ni ile Murano iliyokuwa inawasha taa zote ukianzia na check engine.
Conclusion ni kuwa magari ya Nissan sio mabaya bali mafundi wetu elimu chenga. Na bei za vifaa mafundi ndio wanapandisha.
Nissan murano ni gari comfortable sana na ni nzuri ukiitunza na kuipa vitu vyake original