Ukifuatilia Japanese cars, utagundua Nissan waliwahi kutumia technology mpya ya CVT kabla ya Toyota....sasa cvt za nissan zilipoingia mtaani,mafundi wa mwembeni wakaziponda na kuwaanisha watu ni mbovu, kumbe wao ndiyo wabovu...walizoea kuchokonoa Ordinary Automatic Transmission za Kwenye Corolla na Carina..
Nadhani wanaogopa CVT kwa sababu mbili kubwa...
1. Wabongo tunapenda vitu vya bei rahisi...mtu anataka kumwaga oil ya gear box asitumie zaidi ya 80k...
Kwa upande wa CVT lazima ujipange, oil peke yake maeneo mengi ya TZ haipungui 130k kwa gharama za chini, hapo bado hujamlipa fundi..
2. Elimu...Nimegundua wamiliki wengi wa magari hawana elimu ya kutosha juu ya magari wanayoyamiliki...mtu haelewi gari lake lina gear box ya mfumo gani, yeye anachojua ni kushift kutoka P na kwenda R au D...Mafundi nao hawana elimu ya kutosha....
Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wengi siku hizi wanaomiliki Toyota latest hawakawii kuua gear box...?
Unakuta Toyota imekuja na VCT gear box, siku ya service wanaweka cheap ATF kutoka PUMA Patrol station....Walishakariri Carina zinatumia ATF za pale Puma, basi wanaweka hizo hizo kwenye Passo, IST na nyinginezo....hawana taarifa kuwa hata hizi passo na ist zipo za CVT..
Conclusion
CVT ni transmission nzuri sana ukiweza kuitunza na kuipa fluid yake iliyopendekezwa kwa sababu inakupa smooth driving bila kusikia mshtuko wa kubadilika kwa gear.
Hivyo nimawaasa watu wawe waangalifu, CVT kwenye Nissan zimeshakuwa common, kwa sasa zinakuja kwa kasi kwenye baadhi ya Toyota, Mitsubish na Suzuki. Wale wamiliki wa Toyota wanaopenda cheap services kutoka Puma petrol station, mtaua gear box zenu kila siku.
Soma kwenye kweny deep stick ya oil ya gearbox uone umeambiwa uweke fluid ya aina gani, ufanye hivyo na si vinginevyo.
Nawasilisha.
Sent using
Jamii Forums mobile app