Taarifa ya awali inasema takriban billion 50 zimekusanywa katika wiki 4 za mwanzo kupitia tozo mpya ya kizalendo kwenye miamala ya simu.
Tumeambiwa kwamba tayari billion 15 na bilion 7 zimeshatolewa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya 150 pamoja na kufanya finishing ya maboma ya madarasa yapatayo 560, hivyo bado kuna salio la kama bilioni 25.
Naamini wiki 4 zinazofuata zinaweza zikavuna tozo sawa na hiyo au zaidi toka kwenye miamala ya simu.
Itakuwa ni furaha mno kwangu endapo 50 Billion za mwezi unaofuata zikaenda kuanza ujenzi wa flyover kwenye Mataa ya Morrocco.
Baada ya hapo Billion 50 za mwezi unaofuata tena,na baada ya hapo, tena? Na baada ya hapo tena? Itabidi tukajenge Zahanati za msaada hadi Rwanda na Burundi ili waTanzania watakaohamia huko wajisikie nyumbani [emoji23][emoji23]