Nitaifichaje hii aibu ili niweze kurudisha heshima yangu

Kwa wanywaji na walevi hilo hutokea sana na kesho hakuna anaekumbuka sababu tunajua ni mambo ya pombe, relax kaka...amini usiamini hakuna anaejali hilo kwa sasa sababu wanajua haukuwa wewe ni pombe.
 
πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Your browser is not able to display this video.
 
Mkiambiwa pombe sio chai hamuelewi
 
Nadhani weka juhudi kubwa kwenye kujizuia kuwaza mambo ya hovyo ili siku ukinywa tena usiropoke upuuzi. Na kama watu unawapenda waambie sio usubiri unywe kwanza pombe. Sisi wengine huwa tunazingatia sana anachoongea mlevi. Mlevi huwa hadanganyi
 
Anza kuwa busy na Ibada, iwe ni swala Tano ama Ibada za kawaida za wakristo.

Binadamu tumeumbiwa kusahau

Wakikuona umeanza ibada na kujutia lazima watasahau vivyo hivyo na heshima yako kurudi kama awali
 
Kila kichwa cha mtu kina uwezo tofauti wa kuhimili kilevi, kwanza tuanze kwa kufahamu hilo halafu ndiyo tuone ulichokifanya baada ya kulewa kuwa ni fedheha kweli ama ndiyo ulevi wenyewe!

Unajihisi kudhalilika baada ya kusimuliwa vituko ulivyovifanya baada ya kulewa, lakini vituko hivyo haujafanya na hauwezi kuvifanya ukiwa na akili timamu.

Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kuvijaji vitendo vya mlevi, bali huvipuuza na kuvidharau, kwa hiyo jiondoe kwenye eneo hilo la fedheha kama hukujisaidia hadharani watoto wakaona tupu zako, jiweke tu kwenye kundi la walevi na vurugu zao.

Kuna watu wanadhalilishwa na pombe kwa vituko vya ajabu kuliko ulivyovifanya wewe hadi kupelekea kuiacha, lakini hauwezi kusikia wamefedheheka.

Cha kufanya, jipime kama kichwa chako hakiwezi kuhimili kilevi, basi achana kabisa na pombe.

Kama unaipenda, basi kunywa kidogo kwa kujipimia kama dose ya dawa ili kuweza kuitawala.

Vituko ulivyovifanya siku ya tukio iwe ni fundisho lako la kucontrol pombe ama kuziacha.

Endelea na maisha yako ya kila siku bila wasi wasi wowote, hakuna mtu anaweza kuvitilia maanani vituko vya mtu anayefahamika kuwa kalewa pombe.
 
Pole sana mkuu, na wacha nikupe hizi njia mbili, zitakusaidia sana.

Njia namba uno: Itabidi uendelee kulewa ili hao uliowakosea uendelee kuwakosea hadi washangae kiasi cha kuona si jambo la kawaida bali inawezekana kuna jambo limekupata na hapo wataanza kukufuata kwa upole ili wakupe ushauri wa hapa na pale kwa lengo la kukusaidia uondokane na hiyo hali.

Na wewe utajifanya kuzingatia ushauri wao then utakaa Kaa baadae utaacha utaona wote uliowakosea wanakupa pole kwa changamoto zilizokupata na hapo heshima yako itakua haijaguswa ila wataanza kulaumiwa watu walioko katika ulimwengu wa giza ilihali wao wenyewe hawana taarifa zozote na tatizo lako. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜….

Njia ya pili jifanye haukumbuki chochote kilichotokea baada ya kulewa ila urudi uanze kuwaomba msamaha watu wote ambao walikua karibu na wewe wakati huo wa kulea uwaambie haujui kilichotokea baada ya kulewa ila kwakua unajijua wewe huwa pombe hazikufai kwa maana ukilewa huwa unaongea mambo mengi yasiyofaa(kuropoka, yaani unakua kiropo ropo), kwahiyo unawasiwasi inawezekana kuna jambo lolote la ajabu ulilifanya iwe la kukufedhehesha wewe au watu wengine kwa hali ya kutokujua basi unawataka wakuwieladhi kwa maana haikua dhamira yako, na isitoshe wanajua the really you ukoje.

Fanya hivyo kazini na kwa majirani zako hapo mtaani kwenu then acha yaliyopita yapite na maisha yaendelee kwa maana mwisho wa siku wewe ni binadamu tu na kimsingi hakuna mwanadamu aliyemkamilifu.
 
Jambo dogo sana Hilo kama nukta..... Kwanza hongera kwa kufungua mlango wa 7 ukitaka uishi amani na ujipate ishi maneno uliyoyaongea wakati umekunywa uliyemwambia unampenda mfuate mazima mwambie sio pombe nakupenda kweli ili asijue ni pombe au ukimwambia me
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…