Pole sana mkuu, na wacha nikupe hizi njia mbili, zitakusaidia sana.
Njia namba uno: Itabidi uendelee kulewa ili hao uliowakosea uendelee kuwakosea hadi washangae kiasi cha kuona si jambo la kawaida bali inawezekana kuna jambo limekupata na hapo wataanza kukufuata kwa upole ili wakupe ushauri wa hapa na pale kwa lengo la kukusaidia uondokane na hiyo hali.
Na wewe utajifanya kuzingatia ushauri wao then utakaa Kaa baadae utaacha utaona wote uliowakosea wanakupa pole kwa changamoto zilizokupata na hapo heshima yako itakua haijaguswa ila wataanza kulaumiwa watu walioko katika ulimwengu wa giza ilihali wao wenyewe hawana taarifa zozote na tatizo lako. 😅😅😅.
Njia ya pili jifanye haukumbuki chochote kilichotokea baada ya kulewa ila urudi uanze kuwaomba msamaha watu wote ambao walikua karibu na wewe wakati huo wa kulea uwaambie haujui kilichotokea baada ya kulewa ila kwakua unajijua wewe huwa pombe hazikufai kwa maana ukilewa huwa unaongea mambo mengi yasiyofaa(kuropoka, yaani unakua kiropo ropo), kwahiyo unawasiwasi inawezekana kuna jambo lolote la ajabu ulilifanya iwe la kukufedhehesha wewe au watu wengine kwa hali ya kutokujua basi unawataka wakuwieladhi kwa maana haikua dhamira yako, na isitoshe wanajua the really you ukoje.
Fanya hivyo kazini na kwa majirani zako hapo mtaani kwenu then acha yaliyopita yapite na maisha yaendelee kwa maana mwisho wa siku wewe ni binadamu tu na kimsingi hakuna mwanadamu aliyemkamilifu.