Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Mkuu Mimi ni mwanamke tarehe yangu ni
26/12
Me tarehe 11/12
Naomba nichambulie huyu mwanaume
 
Wawili nyie ni wenye kuendana na maarufu sana katika historia za kuendana kwa mahusiano haya wote mnakuwa mnashare ladha moja ya riwaya, kusafiri, kukutana na watu wapya,

kwa maana nyote wawaili ni watu msio tabirika. Mambo hayawezi kuwa laini siku zote lakini kwa suala la mapenzi kwa wawili nyie utakuta kila siku mambo yanaenda vema.

kwa maana yeye anakuwa anavutika sana na wewe kwa akili yako na tabia ya kuwa na furaha.

Kama wewe ukiwa sio mwenye kubadirika kwa kiasi fulani maana una katabia kako ka uzinzi wa kisiri siri ukiweza kukamudu hako. Japokuwa kwa yeye tabia hii anaijua ila haichukulii uzito sana kama watu wengine japo machoni hawezi kukuonyesha hilo.

Lakini yey ni moja kati ya watu anapokuwa na wewe anaweza kuonyesha tabia za wivu lakini ukimuondoka atasema muacheni akale maisha lakini kwangu atarudi.

Na nyinyi hata kama mahusiano yakifa basi mna uwezo mkubwa wa kuendelea kuwa marafiki na hata mara zingine ikitokea mtakuwa mnapasha kiporo.

Katika ndoa,

Nyote wawili mnakuwa ni wenye kufurahia ukaribu wa mwenzie zaidi ya ukaribu wa kimahaba

Rakims
Uko sahihi Kaka .... shukran

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aksnt sana mkuu , Endelea kutupa madini,.. Niunganishe nae nipte zangu nijue kama yaliyomo yamo au lah


Lakin pia unaweza nisaidia mtitiliko wa maisha yangu inbox mkuu
Gharama yake laki na 20.
 
Mimi me jina E tareh 19/06/1992
Yey ke Jina L tarehe 23/05 /

Nasubir mkuu
Kwa mtizamo unaonenyesha wewe ni maji ya moto na yeye ni mchanga wa fungu. huyu ndio mwenza wako mnaoendana kwa safari nzima ya maisha na anaweza kukukamilisha na kukufaa zaidi na ni perfect match wako kwa sababu;-
Yeye anaonekana ni mtu mwenye stamina na hamu na ana uwezo mzuri wa kukidhi mahitaji yako hasa mkiwa chumbani na mkiwa pamoja ni watu wenye kujiweza kuwasha na kuzima moto wenu wenyewe ni watu mnaweza kugombana dakika 1 kisha ya pili mkaelewana.
Lakini kipi ambacho kinaweza kuwa tatizo kwenu kwa masaa yaliyo baki mnaonekana;-
Kwanza kabisa nyote wawili ni wenye wivu wa kupindukia na viburi(wakaidi) tofauti yenu ni kwamba yeye ni mtu anaependa kummiliki mpenzi wake na kama mtu wa thamani sana, kama ilivyo kwa kitu cha thamani na wewe unakuwa ni mtu wa hisia sana.
Ingawa mnashiriki mshikamano mzuri kuhusu maswala ya pesa, wewe ni mfadhili na hudharau uvivu,
wakati yeye anapenda kutumia kwa kujiridhisha kama yeye na ni jambo lingine nyote wawili japokuwa ni watu mnaendana sana lakini ni sawa na fahari wawili kila mtu anataka awe zaidi na ikitokea mmoja hajakubali kuwa chini ya mwenzie basi ni sawa na nahodha wawili wanaogombania kuendesha meli vita vikizidi chombo kinazama.
Elewa kwa mtizamo huu ukishindwa kuishi na watu wenye mchanga wa fungo ambao wanaweza kukumudu wewe basi utaishia kuwa mpweke na kila mtoto kuwa na mama yake kama mlivyo na sifa hii wengi wenye maji ya moto
😃😃Ubishi Ubishi tumeachana siku ya 3 leo atuwasiliani afu Jambo ata halieleweki...mi gari lishawaka Ni swala la muda tu hatoamini macho ake..nimekubali kushika mengine


Kuhusu watoto mungu tu asaidie makeeeeeee🤐🤐nlikua sjapanga kabisa kuzaa watoto na mama tofauti Ila ndo hivyo tena... nothing guaranteed forever!
 
[emoji2][emoji2]Ubishi Ubishi tumeachana siku ya 3 leo atuwasiliani afu Jambo ata halieleweki...mi gari lishawaka Ni swala la muda tu hatoamini macho ake..nimekubali kushika mengine


Kuhusu watoto mungu tu asaidie makeeeeeee[emoji850][emoji850]nlikua sjapanga kabisa kuzaa watoto na mama tofauti Ila ndo hivyo tena... nothing guaranteed forever!
Pole sana
 
Mke tarehe 19 September
Mume tarehe 31 July

Tiririka hapo Mkuu Rakims.
Natanguliza shukrani nyingi.
Mahusiano haya ni ya watu wawili wasioendana sana hasa ukizingatia tabia ya majivuno na kujiona ya yeye ni machukio kwako na utajikuta hupendezewi na kutaka kwake kutukuzwa kwa kila jambo.

Wewe ni mwenye kujithamini na kujiwekea uzio na ubinafsi wenye manufaa yako binafsi utakuta ni fedheha kubwa kwake yeye mwenye kupenda kuwa juu na kutukuzwa pia ukimuignore kidogo tu hata akiwa anaongea basi gubu lake huta kuja kuamini.

Wewe ni mtu ambaye huna uwezo wa kulea mtu ambaye ni mwenye utukufu wa ndani ya roho yake.

Yes, yeye ni mtu mwenye ukubwa ndani ya roho yake yaani ana asili ya malikia kama ni mwanamke na kama ni mwanaume basi ana asili ya kifalme roho yake ni tajiri na sio tajiri wa kawaida ni tajiri fahari, kabla ya kuondokewa na uhai anatarajiwa kuwa tajiri.

Hivyo kwa wewe ambaye wakati huna hujulikani na wakati unachohujulikani itakuwa ngumu kuishi na falme hii maarufu.

Pia wewe huwezi kumfikia hadhi yake jinsi alivyojiweka hata kama mkikaa nae utaona anakuzidi mengi na vile vile wewe sio mtu wa kutoa sifa kwake yaani kumsifu sifu na yeye hakuna kitu kinamtia nyege kama kusifiwa ukimsifu sifu basi utaona unamlainisha kila kukicha lakini mtu akikwambua jua zamani lilikuwa linachomoza mashariki na kuzama magharibi siku hizi linazama mashariki kubali ila tabia ya mtu huwa haibadiriki.

Ndivyo hivyo hivyo kwako utaushi maisha ya maigizo hadi lini ipo siku gari itawakia namba 5 hapo hapo kila mtu ataangalia uelekeo wake.

Wote wawili ni wenye kujitegemea sana, sio wenye kupenda kutegemea watu

lakini yeye anaonyesha hii kwa njia ya hasira, yaani kujitegemea kwake au maendeleo yake utaona anatumia pesa nyingi hata kwa vitu visivyo na faida yeye haoni hasara kuwa fahari yupo radhi anunue kitu cha thamani kubwa au afanye jambo kubwa pasipo kujali atalala njaa.

wewe ni mchumi na mwenye kujibana sana.

Hivyo yeye hapendi watu wa hivyo na vile vile utakuwa unampotezea muda kama yeye anashindwa kukwambia mimi nakwambia yaliyopo kwake linapokuja katika suala la matumizi hakuna anachokuelewa sawa na kupigia mbuzi gitar labda akuskilize tu kisha akitoka hapo vimeyayuka ana roho ya kitajiri na ukimvumilia mtakuwa matajiri baadae.

Mahusiano yenu ni mafupi sana kuliko uhai wa mayfly.

Rakims
 
Mimi [emoji1485]Me 13/12 G
Yeye[emoji1485] Ke 20/12 R

Mkuu Rakims[emoji1488]
Mahusiano haya ni baina ya moto wa nyasi kwa moto wa nyasi moja kwa moja unaweza kusema ni mfano watoto mapacha yaani wenye kufanana sana.

Lakini hata hivyo ukirejea mwanzo nilishaelezea kuwa hata nyota zenye kufanana huwa zina mushkeli yake.

Baadhi ya wanajimu huamini kwamba mwenye kuweza kumtosheleza Mwenye nyota sawa na nyota hii yako ni pacha wake lakini kwa uzoefu na elimu pamoja na experience nilionayo katika unajimu hapana hii pekee haitoshi bila kuwa na marekebisho.

Imagine mnaishi na mtu mnafanana kila kitu?

Mapenzi yenu yatakuwa lakini lazima tu kuna migongano,

Moja kwa moja twende kwenye uchambuzi wako:

Nyote wawili mnaonekana ni wenye kupenda maendeleo na wenye kuendana sana mwanzoni karibu kila kitu chenu, wenye kupenda kutoka toka na kuroam, japo kuwa ni jambo zuri kwenu machafuko, uhusiano wa matukio yasiyotabirika wala kufikirika huja kwa kushangaza sana.

mnaonekana hata kwenye macho ya watu ni wenye kuendana na kupendezana sana.

Lakini ni kawaida sana kwenu kila mmoja wenu kumletea majanga mwenzie, Kila mmoja kati yenu anakuwa sio mwenye kujitolea kwa mwenzie kwa udhati na mnakuwa nyote wawili ni wenye kupenda kuchakatia nje,

Pair yenu huwa inaokolewa sana na imani ya dini hasa ukizingatia nyota yenu inatawala sana elimu ya dini na vilevile akili ya kiimani zaidi lakini kwa Sagitarians ambao hawana dini katika nyoyo zao utakuta mwanaume anachakatia huku na mwanamke kule.

Mkikutana kila mmoja anaweza kumlia mwenzie yamini kwamba hana hayo mambo lakini pale zinapoanza kuingia mimba za ghafla na kuletewa watoto usio wajua ndio unakumbuka kumbe naishi na jini mwenye miguu miwili.

Wote kati yenu mnatabia ya kumsukuma mwenzie katika kufanya mambo maovu mnapokuwa mnakwazana anaweza kukuboost na kukwambia katembeze nje sibabaiki na wewe ukajaa kweli,

Ni nyota moja ya mahusiano ikiwa na msimamo na imani basi dunia nzima huona kama ya kwao lakini otherwise ni wachezaji wazuri tu wa nje furaha ikiisha ndani.

Rakims
 
Rakims
Mimi ni MWANAMKE
J 24/9 ME
F 5/5 KE
wewe unaonyesha ni mtu mwenye asili ya upepo wa juu na pia yeye anaonekana ni mtu mwenye asili ya udongo mwekundu;
Ni mtu ambaye mnashare nae sayari lakini ni mtu ambaye hamuendani sana kwa kuwa ni mtu ambaye upo nae kwenye ndoa nitakupa maelekezo mengi hapa lakini mngekuwa kwenye mahusiano tu ningekwambia achana nae atakuharibia maisha kama ninavyowajibu wengine lakini ndoa ina uzito wake hivyo nitazidisha hekima katika kukujibu na ukizingatia maelezo uliyoyatoa kwenye PM na hapa sawa kwanza kabisa elewa mtizamo unaonyesha kama kuendana wewe na yeye ni kuwa;-

Mnaendana kwa asilimia 25% tu ambapo tukianzia kwenye upande wa sayari kwa kuwa tu mnashare sayari moja na siku moja mtizamo unakuwa ;-

Nyote wawili mnashare mapenzi katika kupenda mziki na sanaa ndicho kitu mnachofanana, zaidi ya hapo yeye ni mtu wa kupenda kuwa nyumbani yaani kujiweka weka ndani mfano chumbani sio mtu wa kutoka toka na ndio kitu cha kwanza huanza kuwa kero kwako kwa maana wewe ni mtu unapenda kujichanganya na jamii na mambo ya kijamii.

Mwenye kupenda kutumia pesa katika mambo ya starehe na anasa, wakati yeye ni mtu wa kujibana bana na mwenye asili ya ubahili. Unakuwa ni mtu mwenye kukosa subira kwa tabia yake ya kuopenda kukutawala na mfano wa kauli yake ya you have to deal with it no matter what, yeye akisema ndio anataka awe kasema na mjuaji zaidi kwenye mahusiano. Tabia zake za misimamo mikali mfano wa mfia dini akilitaka lake kwa njia lake ni lake ndicho kitu kingine ambacho hakikuvutii.

Ni mtu mwenye wivu kwako kwa kila kitu hata kwa vitu vyako mwenyewe na zaidi mnavutia kwenye tendo la ndoa sasa pale inapofikia kukinaiana ndio balaa huanza kwa maana kati yenu hakuna mapenzi zaidi ya tendo la ndoa ndio kitu pekee kinachowaonyesha mnamapenzi ziada kama kuzungumza vizuri kuelewana kupenda zaidi ya tendo hakuna. Kama unahitaji sex partiner sawa zaidi ya hapo hamna maisha.
nikiamua kuwaweka kwenye asilimia inakuwa hivi;

TENDO LA NDOA - 30

UAMINIFU - 20

MAELEWANO - 5

HISIA -25

THAMANI - 40

USHIRIKIANO - 65

Sasa unapokuwa na ndoa na mtu ambaye yote hayo yanakuwa hayapo zaidi ya thamani tu ambayo unaweza kuipata kwa mtu yoyote na ushirikiano ambao unaweza kuupata hata kwa mtu usiyemjua yoyote tu hizo sifa 2 hazibebi ndoa. ndoa kitu cha kwanza kabisa kinachoibeba ni maelewano ambapo hapo hakuna.

Look somewhere else utapasuka roho hapo.

Rakims
 
Me: 10 Aprily Jina E

Ke: 6 sept Jina F
Katika mahusiano haya ni baina ya Moto wa jaha na mchanga wa fungu,

Kitaalamu nyie ni baina ya moto na ardhi vitu ambavyo haviendani yaani wewe ni moto na yeye ni udongo,

Mahusiano yenu yapo hivi:

Kwanza kabisa ujasiri ulionao mara nyingi humpelekea kuwa na aibu yeye ambaye mara nyingi kitaalamu tunamuita binti maringo haijarishi jinsia yake,

Nyote wawili ni wenye mawazo tofauti yaani kila mmoja na nguvu zake tofauti linapokuja katika suala la mawazo na utendaji vile vile, hasa linapokuja suala la chumbani bila shaka hili ndio kubwa hubeba na kuharibu mahusiano mengi, kila mmoja kati yenu utakuta ni mwenye mawazo tofauti na mwenzie katika kitanda jinsi ya utendaji na jinsi ya kufurahia tendo zima sote tunafahamu kwamba katika tendo la ndoa kwa upande wako ni kama vile uwanja wa vita tukirejea kwake yeye chumbani ni kama vile uwanja wa maonyesho, haiishii hapo tofauti yenu pia inatoka hadi nje ya kitanda kwenda kwenye maisha ya kila siku.

Mapenzi na mihemko yako wewe imejaa msukumo na moja kwa moja bila kupinda wala ubabaishaji.

Kwake yeye ngono zaidi ni suala gumu sana kugawa hata pia huchukua muda kuweza kumvulia nguo mwanaume au mwanamke.

Kwenye maeneo mengine utakuta wewe ni mwenye shauku na mipango mipya na mawazo mapya. Na vile vile ni mwenye kulazimisha kuwa boss wa mahusiano hata kama utaficha mwanzoni.

Tukija kwa bi maringo nimekwambia haijarishi jinsia yake utakuta ni mtu mwenye kukosoa na kusumbua, na hupenda mambo yaende jinsi yeye anavyotaka.

Huyu hawezi kuheshimu au kukubaliana na matakwa yako haijarishi atakuigizia vipi mwanzo.

Na yeye atakutoa kasoro kila siku zinavyoenda hadi utajihisi zuzu.

Na wewe utamuona ni mwenye mgomo baridi na asiyewezekana kufurahisha.

Niamini wawili nyie mwisho wa siku ni wenye kufanya vita sio mapenzi.

Rakims
 
Aksnt sana mkuu , Endelea kutupa madini,.. Niunganishe nae nipte zangu nijue kama yaliyomo yamo au lah


Lakin pia unaweza nisaidia mtitiliko wa maisha yangu inbox mkuu
Nilikujibu mkuu
 
Ke - 04 Jan jina N

Me- 01/Feb jina M

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika mahusiano haya mnaonekana ni wawili msioendana hasa ukizingatia kwamba wewe ni mchanga wa bahari na yeye ni Upepo wa kimbunga;

Unaonaje dhoruba ikitokea kando ya bahari?

Hayo ndio mahusiano yenu yalivyo mkiunganisha roho,

Wewe utajikuta unamuona yeye ni mtu usiyeweza kumtabiri, na yeye atajikuta ni mtu ambaye anashindwa kwenda na wewe kirahisi hadi atumie nguvu nyingi,

Mbinu zako za kawaida tu za kumuendea hata katika kuomba mchezo utakuta kwake ni kero kubwa sana na atakuona kama vile muda wote wewe ni mwenye kumtibua tu mwanzoni utaona kama anakuvumilia lakini baadae sura kamili ya dhoruba itaonekana.

Yeye hujiamini katika kujieleza kimtizamo wake bila maneno.

Na wewe hujiamini katika kujiheshimu bila mipaka, mawasiliano yenu kila mmoja atajikuta haeleweki kwa mwenzie na pia ataona kama anaaibika na kudhalilika kwa mwenzie.

Yeye utakuta ni mtu wa kupenda mitoko na wewe utakuta ni mtu wa kupenda mtu mwenye kumaintain maisha ya nyumbani huyu ni mtu mtafutaji wewe utafurahishwa kwa utafutaji wake mwanzo kwa kufuata mkumbo lakini baadae itakuwa too much hata kama atakuletea maigizo sasa hivi lakini baadae visafari vya kwa ndugu jamaa na marafiki huwa havikatiki.

Yeye alivyompenda uhuru safari ya mapenzi yenu itakuwa ngumu sana na uvumilivu wake kwako ni mdogo huyu anataka mtu mwenye nyota ya moto wa mkaa ambaye yeye akimletea habari za kutoka anakuwa kama kamtia ny*ge. Hakika kipenzi chako hiki ni chenye kupenda kutoka sasa ukimfungia ndani kwa maisha yako ya siasa kali kimbunga kitazunguka kisha vumbi lako litapeperuka na kubaki umechafuka tu.

Nyie mnapendeza zaidi kuwa ni wenye urafiki tu na hata mapenzi yenu mara nyingi huishia kirafiki tu.

Rakims
 
Back
Top Bottom