Nitajieni biashara nyingine inayotoa faida kama mikopo ya kausha damu!

kama riba zao ni 30% -40% mbona kwa mtaji wa 1,000,000 FAIDA SIO 4,000,000 KAMA UNAVYOSEMA ?! Hesabu ulisoma wapi ndugu yangu yani 30% ya million moja ni million nne ?!
 
Kunywa bia popote ulipo .
Ukifika Mbeya mijini , tafadhali njoo Airport ya zamani karibu na gari ziendazo Tunduma utaikuta ofisi ya mikopo sitaji jina ila iko wazi utaiona , wambie wakupe milioni boss wao kasema maana una akili sana .
 
Kwa nondo kama hizi kwanini nisikuheshimu mtani wangu .

Basi tu ni vile hautaki kunipa pumzi toka upate [emoji110]
 
Kausha damu ziendelee
 

Samahani mkuu.

Kausha damu ni sawa na loan sharking?

Na ni halali kabisa kwa sheria za bongo yetu?
 
Kama Riba ni kubwa kakope bank! Kwann uje kukopa kwangu si ni shida zako kwani Umelazimishwa Mkuu.

Binafsi nafanya hii biashara mwaka wa 8 huu riba yangu ilikua 20% kwa mwezi nimeshusha imekua 15% kwa mwezi.

Wabongo bwana yaani unaumia watu kukopeshwa.

Kwa mtu yoyote anaetaka kufanya hii biashara, ni biashara nzuri sana kikubwa uwe na wateja wazuri na uandae mikataba kisheria iliyokaa na ujisajili BOT
 

Mkuu Heshima yako[emoji1545]
 
Tatizo umasikini mkuu. Ukishaona njia ya kupata hela na una shida hauwezi kukumbuka hayo mengine.
 
Pesa haramu hizo...
Zinasafishwa.
 
Kausha damu wamewezaje ?
Wapo wakopaji wababaishaji na wengi wao ni wanawake. We unafikiri hao kausha damu wanakula faida tu kila siku? Nina ndugu mwanamke wa makamo tu ni mwaka wa 5 sasa hivi kesi na hao jamaa wa kausha damu haziishi. Kila tukimsaidia kulipa baada ya muda wanaibuka tena wengine wanaomdai wanampokonya simu au chochote chenye thamani.
 
CCM ndio kausha damu wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…