Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini shughuli ndio imeishia hapa kwa Yanga

Southern Highland

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
14,938
Reaction score
25,405
Mtu yoyote anayesema bingwa keshapatikana naamini bado haujui mpira vizuri, ninaamini bado hajauona ubora wa Yanga. Zipo dakika 90 nyingine za kutetea hiki kilichotokea jana uwanja wa Mkapa.

Njoo nikejeli, nitukane ila Jumamosi utakuja kusema nilitabiri. Naandika hivi nikifahamu vyema home ground ina advantage kubwa lakini siyo kikwazo kwa Yanga kwenda kufanya kitu huko huko Algeria. Kama wao wameshinda ugenini kwa nini Yanga asishinde huko Algeria? INAWEZEKANA? Jibu ni NDIO
 
Kuna watu wamejaa chuki, Jana walipata fursa ya kuonesha chuki zao hadharani.

Sasa ole wao Yanga irudi na kombe hapa watahama nchi wenyewe.
 
Imeisha hiyo, kunyanyua kombe mbele ya waarabu? Siyo rahisi sana!
 
Jipe moyo
 
Naelewa mnayoyapitia bado hamjaamini baada ya siku mbili ndiyo mtaamini kuwa ndiyo tyr imeisha hiyo
 
Ukitoka wewe mm ndio wa mwisho wenu
 
Aisee Yanga kutoboa kule ni kitu kisichowezekana kabisa. Kama USM Alger aliweza kutoka suhulu mugenini kwa Asec Mimose na kumtungua 2 kavu nyumbani basi sio timu ya mchezo. Kumbuka Asec ni timu inayoongoza ligi ya Ivory Coast.

Ndio maana Muarabu kaondoka hapa huku anashangilia sana maana anaona biashara imekwisha. Na kuna hatari tukapigwa 5
 
Na usisahau tayari Yanga INA medali na Mayele ndio mfungaji bora ana kiatu cha dhahabu tayari cha CAF.
hahaha. Aisee, kwa hiyo domo lote ulikuwa unapuyanga siku za nyuma sasa unajipoza na kiatu cha manywele?
 
hahaha. Aisee, kwa hiyo domo lote ulikuwa unapuyanga siku za nyuma sasa unajipoza na kiatu cha manywele?
Yanga IPO mashindanoni mpaka mwisho wa mashindano, endeleeni kuteseka, na mtaangalia Yanga wakivaa medali na nyinyi mtuoneshe za kwenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…