peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
[emoji1623][emoji441] mpaka 2030 huwezi amini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1623][emoji441] mpaka 2030 huwezi amini
Kama wewe unalipa Kodi PAYE, afu mwisho wa SIku unasikia watu wamepiga pesa afu wanaishia kusutwa tu badala ya kurudisha hela inauma sana. Aiseee tunafanyia KAZI watu. Mishahara yetu inakatwa kodi ili watu wale badala ya kuleta maendeleoNdugu zangu, Uraisi siyo kazi ya kitoto. Urais siyo lelemama. Hata Nyerere alilitambua hilo hadi akasema mtu anayetumia nguvu au fedha kuingia ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma.
Tafasiri ya haraka haraka ni kwamba mpaka Dakika hii Samia nchi imeshamshinda, hakuna nchi ngumu kuongoza kama Tanzania ukizingatia ni Mzanzibar hata jiografia ya bara inampiga chenga.
Iko hivi, kuna maeneo watu wanajipigia bila uoga wala aibu kwa sababu wote ni wezi kuanzia TAKUKURU, Polisi hadi mawaziri Hakuna wa kumchunguza mwenzake. Huko kwenye halmashuri hali ya wizi ni mbaya sana.
Kikwete mwenyewe alishawahi kukiri. Nanukuu, "Nawaletea chuma hiki maana mlikuwa mnasema Mimi ni mpole, sasa anakuja mkali". Mwisho wa kunukuu.
Watanzania hawatakiwi kudekezwa utavuna mabua, nchi ilipokuwa imefikia kipindi cha kikwete Magufuli alikuwa hakwepeki that is why Hayati alipitishwa. Sawa?
Je, mlimsikia Mzee Makamba kipindi hicho? Nanukuu, "Huyu atawabatiza Kwa moto siyo maji tena" Walimtabua Kuwa alikuwa mtu sahihi kwa Watanzania.
Sasa nakuja kwa mama Samia ni hivi, Maza hana meno wahuni wa mjini wanamdhalilisha hajui afanye nini. Muda utafika wanachi hawatataka Hata kusikia jina lake.
Maana hawezi kubatiza Kwa moto wa siyo mkali, upole wake umezidi wa Kikwete. Kwa Mwenendo huu ubadhilifu wa kodi zetu kutumiwa na watu binafsi upo pale pale ndiyo maana kila kukichwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Kama wewe unalipa Kodi PAYE, afu mwisho wa SIku unasikia watu wamepiga pesa afu wanaishia kusutwa tu badala ya kurudisha hela inauma sana. Aiseee tunafanyia KAZI watu. Mishahara yetu inakatwa kodi ili watu wale badala ya kuleta maendeleo.
Busara ilikuwa ni kukamilisha miaka 10 ya Awamu ya tano akae pembeni kwa heshima Tofauti na hapo atapata tabu sana. Pia kama taifa tutakuwa tumepata hasara kubwa mno.
Nawasilisha.
Hakuna tofauti hapo sema tofauti ya kipindi cha Magufuri na Samia ,ni kwamba Samia ni mtu anaye ukubali ukweli hata kama unauma na ndio maana ameruhusu mdhibiti wa serikali kuuweka hadharani wizi huo ,maana alikuwa na uwezo wa kumzuia asiuweke wazi na ww usinge ujua.Umeelewa alicho sema.amesema ni bora kipindi cha JPM wizi ulikuwepo ndio ila sio kama wa kipindi hiki huu umezidi mzee
Samia Rais wangu 2025-2030.Akigombea ntamshangaa
Yaani mwizi anakuibia nyumbani kwako unamuona kisha unamuambia stupid wewe toka hapa tuache.Rais gani anamtukana mwizi stupid?. Huyo amalize aondoke asigombee Tena.
Kama wewe unalipa Kodi PAYE, afu mwisho wa SIku unasikia watu wamepiga pesa afu wanaishia kusutwa tu badala ya kurudisha hela inauma sana. Aiseee tunafanyia KAZI watu. Mishahara yetu inakatwa kodi ili watu wale badala ya kuleta maendeleo
[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]
Hiki kipengele kimenifikirisha sana
Kipindi cha jiwe ndio alikuwa akiiba hadi akashindwa kuajiri wafanyakazi na kuongeza mishaharaMbona kuna mengi tu yamefichwa ambayo yakiachiwa nchi itapasuka. Kuna pesa nyingi mno huyu mama ka,itoa nje ya utaratibu wa bunge na bajeti.
Mfano aliwalipa dowans billion 360 bila hata bunge kujua, amempa January Makamba trillion moja wanazosema wanaboresha mitambo ya tanesco ambapo Januari alisema zinatakiwa trilioni 4 ili kukamilisha zoezi.
Kuna pesa ambazo Nape alikiri wamewapa wenye maduka ya kubadilisha fedha kama kifuta machozi.
Kuna billions of shillings zimepigwa wakati wa zoezi la anuani ya makazi na hakuna chochote cha maana zaidi ya kuchukua mitipori na kupachika.
Huko NHIF alipo Makinda wamepotea ripoti sababu Makinda alimsifia sana Magu kiasi cha kuwabeza wanaomsema vibaya Magu ndio maana file lake limeachiwa.
Ndugu kila kitu kikiwekwa wazi tutakimbiana. Ikumbukwe mpaka sasa mama ameshakopa zaidi ya trilioni 20 ndani ya miaka miwili na mpaka sasa thamani ya vitu alivyofanya haifiki hata trilioni 7.
Habari imejikita zaidi kwa Samia we unajikita na jiwe.....akili za wapi hizi?Hakuna kipindi ambacho hii nchi haijawahi kuibiwa, huyo jiwe mnaye sema sijui kipindi chake hakukuwa na wizi ndo kipindi akina makonda walimiliki majumba na magari kifahari yenye thamani ya mabilion ya pesa wakati wanapokea mshahara wa million 6 tu kwa mwezi.
Pia kipindi hicho cha jiwe ndo profesa Asad alifichua ubadhirifu wa trion 1.5 lakini jiwe akamshukia kama mwewe.
Miaka 6 ya jiwe hatukuwahi kuona fisadi yeyote akihukumiwa kwenda jera hali ya kuwa mafisadi yanajulikana.
Jiwe kitu ambacho alikifanya mpaka nikamkubali ni kukomesha tabia za uzembe makazini na kuanzisha baadhi ya miradi mikubwa ya kimkakati lakini kuja kunambia eti alidhibiti wizi hilo nakukatalia mpaka nakufa.
Kipindi cha jiwe 1.5 trilioni ilionekana kuibwa, wizi gani umefikia 1.5 t awamu hii?Umeelewa alicho sema.amesema ni bora kipindi cha JPM wizi ulikuwepo ndio ila sio kama wa kipindi hiki huu umezidi mzee
Tatizo lake ni elimuHabari imejikita zaidi kwa Samia we unajikita na jiwe.....akili za wapi hizi?
Deep State ya Tz ingekuwa imelala ungekuta hadi leo nchi hii watu wanatekwa na miili yao kuokotwaDeep state ya Tanzania sijui ni akina Nani, ila mataifa yaliyomakini angestep down Kwa maslahi mapana ya taifa. kama Trump alivyofanyiwa USA.
Magufuli aliwahi kumfunga nani kwenye wizi wa ripoti ya CAG? Au ripoti kipindi hicho kila kitu kilikuwa safi? 😂😂Yaani mwizi anakuibia nyumbani kwako unamuona kisha unamuambia stupid wewe toka hapa tuache.
Lakini yeye haanzishi mradi mkubwaKipindi cha jiwe ndio alikuwa akiiba hadi akashindwa kuajiri wafanyakazi na kuongeza mishahara
Samia anaajiri na kuongeza mishahara bado miradi ya jiwe aliyoianzisha kwa pupa