Nitawashangaa sana Yanga kama watamlipa Mayele milioni 50

Yani ukija JF kila mtu anajua kila kitu na ana taarifa zote. Hiyo 50M ya Mayele ndio naisikia leo mara ya mwisho ilikua 35M ikapanda mpaka 40M sasa ishafika 50. Yan mtu anjiropokea mara mwingine anasema Musonda ni bora kuliko Mayele. Nimesoma mwingine eti coach Gamondi ana mipango na Musonda zaidi ya Mayele🤣🤣

UKiwa huelewi na wewe unabebwa juu kwa juu kama fikra zao. Yan kwamba kina Eng Hersi hawajui opportunity cost ya aidha kumbakiza Mayele au kumuachia. Tupunguze ujuaji
 
Musonda huyu huyu acha kujifariji wewe!
 
Musonda kawa bora dhidi ya Mayele ni kichekesho design kama watu wanajiandaa kisaikolojia.
 
N
Ndivyo ilivyo
Ila maisha ya mpira ni mafupi, Mchezaji anatakiwa achangamke wakati yupo kwenye peak ,maana akishashuka kupanda tena ni vigumu na wala klabu haitamuonea huruma kua tumlipe mshahara mkubwa kama kipindi kile
Yaliyomkuta Ngassa na jamii ya aina hiyo iwe funzo kwa wachezaji wazawa
Kazi na ushabiki haviendi pamoja
 
MUSONDA NI HATARI ZAIDI YA MAYELE


Mayele keshanusa hatari iliyoko mbele yake na ndiyo maana sasa hivi ameanza vituko,Gamondi anakuja kumpaisha MUSONDA na kila mtu atabaki anashangaa.

Uza Mayele chukua pesa saijili forward mwingine
Mpira ni mchezo wa hadharani ndio Sababu hata wanunuzi wamemuona Mayele.

Wewe utakuwa una makengeza au huwa unafuatilia mpira redioni kupitia TBC.
 
Ngasa ni upuuzi wake binafsi, alivyokwenda kujaribiwa Uingereza Zola alimwambia arudi Tanzania arekebishe vitu muhimu ana Mipango naye, cha kushangaza Ngasa ariporudi Bongo akaja kuongeza mke wa Pili, sasa utasema kichwani kuna mtu hapo?
 
Naomba kuuliza... anayelipa mishahara wachezaji pale yanga kwa sasa ni nani?! Si ni GSM au?! 🤔🤔🤔
 
Ngasa ni upuuzi wake binafsi, alivyokwenda kujaribiwa Uingereza Zola alimwambia arudi Tanzania arekebishe vitu muhimu ana Mipango naye, cha kushangaza Ngasa ariporudi Bongo akaja kuongea mke wa Pili, sasa utasema kichwani kuna mtu hapo?
Ngassa naskia alishindwa kumla kuku mzima.

Ukatokea ubishi kati ya management ya timu na wakala wa mchezaji.

Management ikasema mpira wa huku Ulaya nguvu zinahitajika sana sasa mchezaykama anashindwa kumaliza kuku, hata awe anapiga chenga kiasi gani ila bila stamina atakuwa anapigwa push na kutolewa kwenye reli.

Kuna wachimbaji kule Chunya walipoisikia hii habari walimuona Ngassa mjinga.

Jamaa mmoja alisema ningekuwa mimi kwanza huyo kuku ningempiga na matonge kadhaa
 
N
Ndivyo ilivyo
Ila maisha ya mpira ni mafupi, Mchezaji anatakiwa achangamke wakati yupo kwenye peak ,maana akishashuka kupanda tena ni vigumu na wala klabu haitamuonea huruma kua tumlipe mshahara mkubwa kama kipindi kile
Yaliyomkuta Ngassa na jamii ya aina hiyo iwe funzo kwa wachezaji wazawa
Kazi na ushabiki haviendi pamoja
 
Kuna jamaa yangu anafanya kazi Kilimanjaro hotel alikuwa New Africa hotel pia anakwambia walivyokuja team ya Taifa ya Ivory wale kina Drogba wanafuta hadi Kuku Wawili mchezaji mmoja, na wote wanacheza mpira ulaya.
 
ushauri mzuri wa kutengeneza timu za watoto ila nilichoshuhudia kwenye mashindano ya under 20 Bado Wana safari ndefu
 
Ushauri wako uzingatiwe
 
Mpira ni biashara, kama ni 1.5 b basi wakunje pesa, washambuliaji wamejaa.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…