Katika kupunguza unene na uzito wa mwili,wengi wametumia njia mbalimbali bila mafanikio! Mfano kunywa maji vuguvugu yenye limao,kufanya mazoezi,kufunga kibana tumbo nk,njia hizo zimeshindwa kuwa na ufanisi na wanazidi kunenepeana tu.
Leo ninakuletea njia lishe (formula) ya kupunguza unene na uzito (kilo tano) kwa siku saba tu.
Siku ya 1: Asubuhi kula matunda,mchana chemsa kabichi weka chumvi kidogo na nyanya chemsha na upate supu; kula mchanganyiko huo na utajisikia umeshiba kabisa.Jioni kula tikitimaji na mbogamboga au kabichi kama ulivyotengeneza mchana.
Siku ya 2:Kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).Mchana kula kabichi iliyochemshwa tengeneza na kachumbari,katika kabichi weka chumvi,pilipili na mafuta ya olive.Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana,lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.
Siku ya 3:Kula mboga za majani na matunda,unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja.
Siku ya 4:Kula ndizi moja na unywe maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi.Mchana kula kabichi kama ulivyotengeneza siku ya kwanza,usiku rudia mlo wa mchana.
Siku ya 5:Kula nyanya nne pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi.Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya.Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.
Siku ya 6:Unaweza kula chakula cha protini na mboga za majani,anza kwa kula kachumbari asubuhi.Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki.Usiku tengeneza supu ya kabichi.
Siku ya 7: Anza kwa matunda na juisi.Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
KUMBUKA:
Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku.
Unapomaliza dayati ya kwanza,unapaswa kupumzika wiki moja huku ukitumia vyakula ambavyo havikuongezei tena uzito.
Utaendelea tena na dayati hiyo wiki tatu mpaka pale utakapofikia uzito unaouhitaji.
Wasalaam!!