Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

choisir-un-dentifrice-HELVIDENT-1024x683.jpg
Dawa ya meno , ni kitu muhimu sana katika usafi wa kinywa na meno wa kila siku. Kwa kuwa zipo aina nyingi za dawa za meno, ni muhimu kuchagua dawa ambayo inaendana na mahitaji yako. Makala hii inaongelea aina tofauti tofauti za dawa za meno, kazi zake na jinsi ya kuzitumia kwaajili ya afya bora ya kinywa na meno yako.

1. Dawa ya kawaida
Faida: Inaimarisha meno na kuzuia yasitoboke/kuoza.
Watumiaji Hii inafaa kwa mtu yeyote na muhimu zaidi kwa wale ambao wapo kwenye hatari ya kuoza/kutoboka meno.

2. Dawa ya Kung'arisha meno
Faida: Kung'arisha meno.

3. Dawa ya meno kwaajili ya ganzi kwenye meno /Sensitivity Toothpaste
Faida: Inapunguza hali ya kupata ganzi kwenye meno hasa wakati wa kunywa au kula vitu baridi au vya moto.
Watumiaji: Watu ambao wanapata ganzi kwenye meno, mfano watu ambao meno yao yamelika kuta za pembeni au juu , wanaosaga meno usiku, na watu ambao fizi zao zimelika kiasi kwamba mizizi ya meno inaweza kuonekana .

4. Dawa ya meno ya watoto
Faida: Dawa hizi zinakuwa na kiwango cha madini ya floridi kinachofaa kwa watoto, lakini pia huwa na ladha na muonekano ambao huwavutia watoto kusafisha vinywa na meno yao. Kumbuka hauhitaji kiwango kikubwa cha dawa ya meno. Watu wazima na watoto kuanzia umri wa miaka

6: Saizi ya punje ya njegere.
Watoto wenye umri wa chini ya miaka 6 Saizi ya punje ya mchele.

Kuchagua dawa na kuitumia kiusahihi ni muhimu sana katika kulinda afya ya kinywa chako. Kutokana na kuwepo kwa dawa nyingi sokoni, hakikisha dawa yako ina madini ya floridi, na hakikisha imethibitishwa na shirika la viwango la Tanzania (TBS).

pia Iwe imeandikwa kiwango cha Fluoride 1450- 1500Ppm kwenye box lake.

Muone daktari wa afya ya kinywa na meno kwa msaada zaidi, ,iwapo Unachangamoto za kinywa na meno Unaweza wasiliana nami
 
healthy-pregnancy-side-view-pregnant-woman-with-big-belly-advanced-pregnancy-in-hands-banner.jpg
Wakati wa ujauzito ni wakati ambao mwili wa mjamzito unapata mabadiliko mengi sana ya kifiziolojia Afya ya mama katika kipindi hichi ni muhimu sana kwani ukuaji wa mtoto unategemea sana afya ya mama . Leo tutaangalia umuhimu wa afya ya kinywa na meno kwa mama mjamzito na jinsi inavyo husiana na afya ya mtoto.



Huenda umekutana / umewahi sikia watu wakisema mama mjamzito hatakiwi kwenda kwa daktari wa kinywa na meno na wanasema akiumwa jino au shida yoyote kinywani anatakiwa kusubiri mpaka ajifungue!



UKWELI NI UPI?

Afya ya kinywa na meno ni muhimu sana kwa mjamzito kwani inaweza kuathiri afya ya mama pamoja na mtoto ikiwa haitozingatiwa, mfano magonjwa ya fizi kwa mjamzito yanahusishwa na watoto kuzaliwa na uzito mdogo na mtoto kuzaliwa kabla ya wakati. Kutoboka kwa meno kunaweza kuleta maumivu makati sana, na wakati mwingine yanaweza kusababisha majipu katika taya. Yote haya yanaweza kuathiri ubora wa maisha ya mjamzito, hasa katika ulaji wa chakula.

Ni sawa kumuacha mjamzito na maumivu ya meno mpaka atakapojifungua?


MAGONJWA ANAYOWEZA KUPATA MAMA MJAMZITO

Wakati wa ujauzito kinga ya mwili ya mama huwa inashuka na hivyo kumfanya mjamzito kuwa na hatari ya kupata magonjwa mbalimbali.


Kowhai-Dental-Gingivitis1-500px.jpg

1. Magonjwa ya fizi - fizi kuvimba, kutoa damu na harufu mbaya, hii inatokananna mabadiliko mengi ya homoni.
2. Kutoboka/kuoza meno - wakati wa ujauzito mama anaweza kupenda vyakula/vinywaji vyenye sukari zaidi na hii inawezza kupelekea tatizo hili
3. Uvimbe kwenye fizi / (pregnancy tumours), baadhi ya wanawake hupata uvimbe kwenye fizi zao na vimbe hizi huisha zenyewe baada ya ujauzito.
4. Meno kupata ganzi - ikiwa mjamzito anatapika sana , matapishi huwa yana tindikali ambayo inaweza kusababsiha. Meno kufa ganzi.

VITU VYA KUZINGATIA KWA MJA MZITO

Kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno , kabla ya kuwa mjamzito ,lakini pia wakati wa ujauzito angalau mara mbili.
Usafi wa kinywa , piga mswaki mara mbili,tumia nyuzi kamba , tumia dawa ya mswaki yenye madini ya floridi
Kutapika : baada ya kutapika usipigwe mswaki hapo hapo, sukutua namaji vizuri
Kula mlo kamili : kula hatunda mboga mboga kwa bingi, kunywa maji mengi , punguza vyakula vyenye sukari nyingi
Usivute cigar na usinywe bombe
Usipige mswaki muda mfupi baada ya kutapika, sukutua na maji mengi kwanza!


MATIBABU GANI YANAWEZA KUFANYIKA WAKATI WA UJAUZITO

1.Kusafisha meno
2.Kuziba meno
3.Matibabu ya dharura - kung’oa jino, matibabu ya mzizi wa jino,upasuaji kama ikihitajika kulingana na daktari atakavyo amua.

Iwapo Utakuwa na changamoto ya kinywa na meno kama meno kutoboka, mapengo, ganzi kwenye meno, Mpangilio usio sahihi wa Meno unaweza Wasiliana Nami .
 
tatizo la sehem ya ndani ya kinywa kwq juu kuuma (au kuwa na vidonda vidogo vya njano) inasababishwa na nini na matibabu ni yapi
 
Hivi hii huduma ni salama..? Inawezekana kufanyika kwenye meno ya juu..?
Ndyo mkuu ni salama , pia inawezekana kufanyika kwenye meno yote juu na chini iwapo tu kuna dalili na vigezo vya kufanya huduma ya mzizi wa jino
 
Back
Top Bottom