Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

IMG-20241002-WA0316.jpg
Afya ya kinywa ni muhimu sana katika maisha yetu, japo wengi wetu huchukulia poa, mpaka pale tunapo pata tatizo. Kusikia ganzi kwenye meno / tooth sensitivity ni moja kati ya changamoto ambazo wengi wetu tunazo hasa tunapokunywa vinywaji vya baridi.

Kama umewahi kupata ganzi/ maumivu makali kwenye meno baada ya kunywa kinywaji baridi haupo pekee yako. Makala hii itaangazia sababu za tatizo la ganzi kwenye meno na namna ya kulidhibiti.

SAYANSI INASEMAJE?
Hali ya meno kusikia ganzi hutokea pale ambapo tabaka la juu ya jino linapopata shida, mfano kuchubuka au kutoboka. Meno huwa yana matabaka matatu na haya matabaka hulinda kiini cha ndani ya jino ambacho kina mishipa ya fahamu na mishipa ya damu ambayo huleta virutubisho kwenye jino.

Kwahiyo inapotokea mchubuko au kutoboka kwa matabaka haya kile kiini cha jino kinakosa ulinzi na kusababisha ule ubaridi wa vinywaji kwenda moja kwa moja kwenye kiini cha jino.

Lakini pia ikitokea fizi zimelika sehemu ya mzizi wa jino inakosa ulinzi na kufanya ule ubaridi uende moja kwa moja kwenye mzizi wa jino hali ambayo hupelekea maumivu au ganzi

SABABU ZINAZOPLEKEA GANZI/ MAUMIVU
1.Kutoboka kwa meno.

2.Kuchubuka/ kulika kwa fizi (kupiga mswaki kwa nguvu).

Kuchubuka kwa tabaka la juu la jino (Vyakula vyenye tindikali, Kupiga mswaki kwa nguvu).

3.Kusaga meno (hasa wale wanaosaga wakila wamelala).

4.Matibabu ya meno kama vile whitening (kufanya yawe meupe) hufanya meno yapata ganzi kwa muda.

UFANYE NINI KUZUIA TATIZO HILI
Kama tayari unasumbuliwa na hali hii, kuna vitu unavoweza kufanya ili kuondokana na tatizo.


1.Kutumia dawa ya meno maalumu kwa kuzuia ganzi (Desensitizing Toothpaste) - Hizi dawa zinakuwa na madini maalumu ambayo huzuia ule ubaridi usifikie kwenye kiini cha jino.

2.Punguza matumizi ya vyakula/vinywaji vyenye tindikali - mfano malimao, ndimu, soda N.K

3. Piga mswaki kwa namna nzuri - Usitumie nguvu nyingi kupiga mswaki, na tumia mswaki laini na safisha katikakati ya meno kwa kutumia kamba nyuzi (dental floss)

4.Kwa wanaosaga meno (bruxism) hakikisha unavaa mouthguard - Hii husaidia kupunguza msuguano kati ya meno na kulinda tabaka la juu la jino.

5.Fanya uchunguzi wa kinywa na meno - Uchunguzi angalau mara mbili kwa mwaka husaidia kugundua matatizo yakiwa katika hatua za mwanzo.

Hali ya kupata maumivu wakati wa kula/kunywa vitu vya baridi inatutukumbusha umuhimu wa afya ya kinywa na meno na namna ambayo inaweza kuathiri ubora wa miasha ya kila siku. kwa kuzingatia mambo tuliyoongelea hapo juu unaweza kuendelea kuburudika na vyakula/ vinywaji vya baridi pasipo kupata maumivu.

Ukiwa na Tatizo hilo au changamoto za kinywa na meno Usisite kuja PM au nipigie / WhatsApp: 0658 950 085

Tunatoa huduma za kinywa na meno Tunapatikana Kibaha - Pwani , Magomeni- Dar es Salaam

Karibuni sana
 
Meno ni viungo mhimu katika mwili wa binadamu mana tabasamu lolote huanzia kinywani

Meno bandia ni viungo
ambavyo huweka kinywani kuziba nafasi ya jino Lililondolewa ili uweze kutafuna chakula vizuri

Zipo aina mbili za meno bandia
1. Meno ya kuvaa na Kuvua (Removable Partial Denture)
2. Meno ya Kudumu ya moja kwa moja ( Full Denture)


Meno bandia yanatengenezwa kwa materials ya aina tatu
Acyrilic materials
Chuma ( Ceramics )
Zinconia

FAIDA ZA MENO BANDIA
Uweze Kutafuna Chakula vizuri
Muonekano
Matamshi
Kulinda Meno mengine yasiharibike

Je wewe ni mhanga wa mapengo , au tatizo hilo wasiliana na Daktari kwa namba hizi: 0658 950 085
Screenshot_20241007_013726_Instagram.jpg
Screenshot_20241007_013713_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom