Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

1. kiziba jino kwa kutumia mercury kuna madhara yoyote kiafya?
2. huduma ya kisafisha meno yenye rangi" kahawia" a.k.a meno ya arusha na kuyafanya yawe meupe hayana madhara kwa meno hayo? kuna mtu alifanyiwa hii huduma meno yakaanza kupata ganzi
 
Meno ya Kahawia (Fluorosis) hutokea mtoto anapopata kiwango kikubwa cha fluoride akiwa tumboni au katika miaka ya mwanzo ya maisha.

Meno huanza kutengenezwa kati ya wiki ya 3 hadi 6 ya ujauzito.

Ikiwa mama anapata maji au vyakula vyenye fluoride nyingi, meno ya mtoto yanayokua yanaweza kuathirika, na kusababisha madoa meupe au rangi ya kahawia kwenye meno baada ya kutokeza.

Matibabu ya meno ya kahawia

1. Kupiga mswaki na polishing – Kusafisha sehemu za juu za meno ili kupunguza madoa mepesi.

2. Bleaching – Njia ya kusafisha kitaalam kwa kutumia kemikali ili kupunguza rangi ya meno.

3. Veneers– Viboreshaji vidogo vya porcelaini au composite vinawekwa kufunika meno yaliyoathirika.

4. Crowns – Kofia za meno zinavaliwa kwenye meno yaliyoathirika sana ili kuboresha muonekano na uimara.

Kujua matibabu yapi hutegemea kiwango cha fluorosis. Kwa taarifa zaidi fika offisini kwetu ,Uweze kupata Elimu , Matibabu

Kibaha - Pwani, Magomeni- Dar es Salaam
kama una tatizo hili karibia PM tuweze kulitatua na ufafanuzi zaidi.
IMG_20241005_093645_877.jpg
IMG_20241005_093645_914.jpg
 
1. kiziba jino kwa kutumia mercury kuna madhara yoyote kiafya?
2. huduma ya kisafisha meno yenye rangi" kahawia" a.k.a meno ya arusha na kuyafanya yawe meupe hayana madhara kwa meno hayo? kuna mtu alifanyiwa hii huduma meno yakaanza kupata ganzi
1. Ndyo kuna kiasi kidogo japo sahizi tumehama kutumia Mercury ( Amalgam Restorative materials) kwa sasa kuna dawa mbadala inaitwa Cention N Restorative Materials hii ni zaidi ya Amalgam ina Release Flolaidi , ni tooth coloured, Effectiveness yake ni kubwa. Na ni strong kuliko Amalgam.
2.Kuna njia zaidi ya Nne Za Kusafisha Meno ya Arusha Hivyo Unaweza Pitia uzi Niliopandisha mda sio mrefu kujifunza zaidi .
Karibu
 
Ipo wapi na inatoa huduma hiyo tu?
Hapana tunatoa huduma zaidi ya 8 za kinywa na Meno Ikiwepo
.meno bandia ya aina zote
.Kusafisha meno
.kung'arisha meno
.Kuondoa maumivu ya meno
.Kurekebisha mpangilio wa meno yaliyokaa vibaya
Na huduma nyingine karibu PM au WhatsApp 0658 950 085 uweze kupata Maelekezo zaidi na namna ya kufika offisini Kwetu
 
Jino jipya ukifika muda wake wa kuchipua huchipua popote...hivyo ya zamani kama hayajatolewa hapo ni full kupandana
 
Asante sana mkuu, nadhani mm naweza kuwa nimesababishiwa na moja wapo ya ulivyo orodhesha. Tuje kwenye njia za utatuzi kama unaweza kuziorodhesha sambamba na faida na hasara zake ili nifanye maamuzi kabla sijafika magomeni
Mkuu swali hili tafadhari
 
Mkuu swali hili tafadhari
Zipo njia zaidi ya 8 za kurekebisha mpangilio wa meno hivyo tukiona tatizo lako ndyo tutajua njia ipi inakufaa unaweza nitumia picha PM nikaona meno yalivyo .ili nijue njia gani itafaa
 
Zari mama Tifa Dangote alikuwaga na meno yamekaa vibaya mnoo akawa hacheki...ila kwa sasa yamekaa vzr mnoo
 
Back
Top Bottom