Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Meno yananiuma nikila nyamaa hii imekaaje mkuu
Moja ya sababu ya meno kuuma
.Meno kutoboka
.Magonjwa ya fizi
Unaweza wasiliana nami kwa PM au WhatsApp, ili uweze kufika offisini kwetu uweze kupata huduma ya kinywa na meno
 
Kukaa kwenye AC au feni kunabadili joto la chumba hivyo kama ambavyo inazidi mwili huhisi baridi na kutetemeka hata meno hivyo hivyo, baridi ikizidi kuliko Ile hali ya kawaida ya kinywa meno yanatabia Moja yenyewe chochote kitacho enda kwake hakihisi baridi au joto kama ilivyo ngozi ila yakitokea mabadiriko ya hali ya hewa hasa baridi jino hutafsiri ni maumivu na hapa tunazungumzia Kwa yule mtu ambae meno yake yameanza kulika (abrasion) Kwa kupiga maswaki Kwa nguvu au yule anae fungulia vizibo meno. Hio hali haimpati Kila mtu

Unafanyaje muhimu kuchunguzwa kujua aina ya meno Yako Ili upewe tiba ya dawa ya maswaki au dawa ya kupaka kutokana na Tatizo
Upo SAHIHI 💯
 
Naomba kujua kwanini mara nyingi meno ya chini huwa na shida kwa maana ya kutoboka kuliko ya juu,kwa maana kwa asilimia kubwa ya watu huwa tunang'oa meno ya chini kuliko ya juu
 
Mimi ni mtaalamu wa afya ya kinywa na meno napatikana Magomeni - Dar es Salaam na Kibaha -pwani
Kama una swali au chochote kuhusu kinywa na meno niandikie hapa chini nitajitahidi kujibu kadri ya uwezo wangu.
  • Katika vituo hivyo vya kazi pia natoa huduma kwa gharama rafiki kabisa .
  • Elimu ya kinywa na meno
  • Kuziba meno yaliyotoboka
  • Kusafisha meno na kung'arisha meno
  • Kupanga meno (braces)
  • Kuweka meno bandia (meno bandia sehemu/kamili)
  • Huduma ya mzizi wa jino (root canal treatment)
  • Urembo wa meno
  • Veneers, blekning, taji na madaraja
Kinywa chenye afya, mwili wenye furaha.

View attachment 3117272
Meno yaliyovunjika (sio kutoboka) yana tiba yake?
.Na meno bandia sehemu kamili ndio ipoje?
 
Naomba maelezo ya hii picha
View attachment 3118117

Maelezo ya kitaalam kulingana na kinachoonekana hapo kisha toa ushauri.
Huyu mtu ana magonjwa ya Fizi ( Calculus ) Huo Utando mgumu Wa Njano umesababiswa na Kutosafisha Kinywa vizuri, Matumizi ya pombe na sigara NK ..Utatuzi wake anaweza Fika Kliniki ya Kinywa na Meno na Kufanyiwa Huduma ya Kusafisha Kuondoa hilo tabaka la Njano meno yatabaki imara na Atakuwa powa pia harufu mbaya mdomoni itaondoka
Karibu
 
Meno yaliyovunjika (sio kutoboka) yana tiba yake?
.Na meno bandia sehemu kamili ndio ipoje?
Ndyo yanatiba , kuna huduma ya kuvalisha kofia ya jino ( crowning)
Nimekuwekea Video Mjongeo uweze kuon
 
Attachments

  • 5a64316317be4ac0b9056758c60920fe.mp4
    1.5 MB
Ndyo yanatiba , kuna huduma ya kuvalisha kofia ya jino ( crowning)
Nimekuwekea Video Mjongeo uweze kuon
Je hii crowning ni imara kiasi gani kwa maana inadumu muda gani maana naona kama ni material nyepesi na inabandikwa tu?
 
Naomba kujua kwanini mara nyingi meno ya chini huwa na shida kwa maana ya kutoboka kuliko ya juu,kwa maana kwa asilimia kubwa ya watu huwa tunang'oa meno ya chini kuliko ya juu
Meno ya chini yana shape ya Concave section ambapo ni rahisi mabaki ya chakula kunata , hivyo yasiposafishwa vizuri hupelekea kuharibika mapema .
 
Ndyo yanatiba , kuna huduma ya kuvalisha kofia ya jino ( crowning)
Nimekuwekea Video Mjongeo uweze kuon
Hivyo hiyo kofia ni ya moja kwa moja au inatolewa?
.Na kuhusu jino lililokatika (kati fizi na jino) matibabu yanakuwaje?
 
Huyu mtu ana magonjwa ya Fizi ( Calculus ) Huo Utando mgumu Wa Njano umesababiswa na Kutosafisha Kinywa vizuri, Matumizi ya pombe na sigara NK ..Utatuzi wake anaweza Fika Kliniki ya Kinywa na Meno na Kufanyiwa Huduma ya Kusafisha Kuondoa hilo tabaka la Njano meno yatabaki imara na Atakuwa powa pia harufu mbaya mdomoni itaondoka
Karibu
Havuti sigara wala hanywi pombe ni mwanamke
Anapiga mswaki kila siku
 
Je hii crowning ni imara kiasi gani kwa maana inadumu muda gani maana naona kama ni material nyepesi na inabandikwa tu?
Ceramics crowns zinadumu zaidi ya miaka 25. Karibu sana mkuu
 
Hivyo hiyo kofia ni ya moja kwa moja au inatolewa?
.Na kuhusu jino lililokatika (kati fizi na jino) matibabu yanakuwaje?
Kofia ya jino ni ya kudumu .
Visiki vya jino huondolewa ili kuepuka majipu na usaha
 
Back
Top Bottom