Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Hapana kusafisha meno kuna aina nyingi ikiwa ni kuondoa uchafu wa kawaida ( Utando wa njano ) hakuna kemikali inayotumika .
 
Je meno yenye rangi ya kahawia kama waliyonayo watu wa baadhi ya maeneo nchini, ni kweli yameoza? Je nini kifanyike kama.Meno yangu ni ya kahawia na hayajatoboka ila nataka yawe meupe kama Meno ya watu wengine?
Samahani kwa Kuchelewa kujibu hili fatilia kuna uzi nimeweka juu ya matibabu ya Meno ya Kahawia
 
Meno bandia yapo ya Aina Tatu
.Meno bandia ya Kuvaa na Kuvua ( Removable partial Denture ) haya kutengenezewa mtu ambaye kinywa kina nafasi kubwa ili aweze kuongea, kutafuna , na muonekano gharama zake ni tsh 40,000/= kwa jino

.Meno ya Kudumu ( hapa kuna Acyrilic, Ceramics na Zinconia )

Haya huwekwa kwa Kutumia baadhi ya meno kinywani kama nguzo ya kushikiria yasitoke

Pia gharama
Acyrilic crowns tsh 100,000
Ceramics ( chuma ) tsh 350,000/=
Zinconia tsh 400,000 kwa jino

Ceramics na zinconia ni imara zaidi , yanadumu zaidi ya miaka 25
 
Kwa mtu ambae ana mpangilio mbaya wa meno yani yaacha nafasi na kutengenezea ueazi wa mabaki ya chakula kubaki na kusumbua kutoka hata kwa toothpick, njia ya kumsaidia ni kuyapanga kwa hzo braces pekee au kuna njia nyingine tofauti?

Kama ni hizo braces je, side effect zake ni zipi kwa mtu wa rika kati ya miaka 25-30?
 
Sijaelewa yani 400,000 kwa ajili ya jino moja?
 
Kwa nini mpaka leo hakuna tiba ya meno zaidi ya kung'oa?
Mkuu unaposema zaidi ya, ni kwamba umeiweka hiyo kuwa tiba. Kung'oa jino sio tiba ni suluhu ya tatizo tu
 
Huduma za kuweka meno ya bandia unafanya meno ya chuma au plastic? Na ni ya kuweka na kutoa au ya moja kwa moja? Unaweza kufafanua pia, tofauti ya hayo ya plastic na ya chuma na pia faida na hasara zake
 
Kuna njia mbalimbali ya kupanga meno ili yakae kwenye mpangilio ulio sahihi . Njia ya Braces ni salama iwapo mtu ana meno imara, hana magonjwa ya fizi NK ..kuna Uzi nitaupandisha kuhusu mpangilio mbaya wa meno ukipata mda utaupitia
 
Huduma za kuweka meno ya bandia unafanya meno ya chuma au plastic? Na ni ya kuweka na kutoa au ya moja kwa moja? Unaweza kufafanua pia, tofauti ya hayo ya plastic na ya chuma na pia faida na hasara zake
Huduma za kuweka meno bandia ipo , yapo meno bandia (Acyrilic tsh 40,000) kwa jino haya mtu anaweza yatumia kwa kula na kutafunia.
Kuna meno bandia ya Kudumu ( Ceramics na Zinconia )
Haya hapa tunaweka moja kwa moja kwa kutumia Nguzo za baadhi ya meno mengine kushikilia gharama zake ni tsh 350,000 kwa jino la Ceramics, na Zinconia tsh 400,000/=

Faida ya Meno bandia
.Ili Uweze kutafunia chakula Vizuri
.Matamshi
.Kulinda Meno Mengine Yasiharibike
.Muonekano
.Kuepukana na Magonjwa ya Taya ( TMJ)
Nimeambatanisha na Picha za Meno ya Chuma ( Ceramics )
Kwa Ufafanuzi zaidi Karibu PM , Uweze Kupata Maelekezo ya Ziada
Huduma za kuweka meno ya bandia unafanya meno ya chuma au plastic? Na ni ya kuweka na kutoa au ya moja kwa moja? Unaweza kufafanua pia, tofauti ya hayo ya plastic na ya chuma na pia faida na hasara zake
 
Mkuu unaposema zaidi ya, ni kwamba umeiweka hiyo kuwa tiba. Kung'oa jino sio tiba ni suluhu ya tatizo tu
Kungoa jino ni Suluhisho la kuondoa maumivu iwapo jino limeharibika sana hakuna njia nyingine ya matibabu ya kuweza kutatua ndipo tunaondoa jino
 
Kuna njia mbalimbali ya kupanga meno ili yakae kwenye mpangilio ulio sahihi . Njia ya Braces ni salama iwapo mtu ana meno imara, hana magonjwa ya fizi NK ..kuna Uzi nitaupandisha kuhusu mpangilio mbaya wa meno ukipata mda utaupitia
Sawa usisahau kunitag utakapo upandisha
 
Ceramic inadumu zaidi ya miaka 25. Pia sahizi kuna dawa mpya ya kuzibia meno inaitwa Cention N Restorative Materials ni mbadala wa Amalgam ( mercury) . Rangi yake inafanana na meno yalivyo yani Shade ya A2 iko strong na effectively kuliko Amalgam na Glass ionomer Cements.
 
Kuziba pengo mkuu inachukua siku ngapi, kuanzia maandalizi mpaka kuwa tayari kwenye mdomo?
Nataka nije nitengeneze na kuziba baadhi
 
Mpangilio mzuri wa meno siyo kwaajili ya muonekano au tabasamu zuri pekee yake, mpangilio mzuri wa meno unawezesha kuwa ana afya bora ya kinywa na meno, ikiwa ni pamoja na kuwezesha utafunaji mzuri wa chakula na kuweza kutamka matamshi /kuongea vizuri.

Kwa bahati mbaya watu wengi wana changamoto ya kuwa na mpangilio mbaya wa meno, hali ambayo isipotibiwa inaweza kuleta matatizo mengine ya meno mfano kuoza meno. Nini kinasababisha mpangilio mbaya wa meno?

katika mada hii tutazunguzia vitu vinavyopelekea mtu kuwa na mpangilio mbaya wa meno, ili ikusaidie namna ya kujikinga/ kuwakinga watu wengine wasipate tatizo hili na kama limeshatokea ujue ni nini unaweza fanya kutibu.

1. Kurithi kutoka kwa wazazi
Mtoto anarithi vitu vingi kutoka kwa wazazi, hivyo inawezekana akarithi mpangilio wa meno kutoka kwa wazazi wake. Siyo jambo la kushangaza kwani vinasaba vinarithiwa kizazi mpaka kizazi.

2.Kupoteza/ kung'oa meno ya utotoni kabla ya wakati wake.
Inawezekana umewahi kumpeleka mtoto kwenye kliniki ya meno ili akang'oe jino na kisha daktari akakwambia hawezi kuling'oa kwani muda wake bado. Binadamu ana seti mbili za meno ( ya utotoni na ya ukubwani) kwenye meno ya utotoni, kila jino linamuda wake maalumu wa kuota na kung'oka ili kupisha lile la ukubwani.

Ikitokea jino la utotoni limeng'olewa kabla ya wakati wake ile nafasi yake inaweza kuzibwa na jino lingine ambalo liko mdomoni na kuziba lile jino la ukubwani ambalo linakuwa bado halijaanza kuonekana mdomoni.

3.Tabia ya kunyonya vidole kwa muda mrefu
Watoto huwa na kawaida ya kunyonya vidole, tabia hii ikiendelea kwa muda mrefu mfano ikiwa mtoto ataendelea kunyonya vidole hata anapofikia umri wa zaidi ya miaka minne (4) anakuwa na hatari zaidi ya kupata mpangilio mbaya. Tabia hii hufanya taya la juu kuwa jembamba na hivyo kufanya meno ya juu na chini yasikutane


4.Magonjwa ya fizi
Magonjwa fizi ya muda mrefu yanaweza kupeleka meno kujipanga vibaya ikiwa hayatotibiwa, yamkini umekutana na mtu anakwambia sikuwahi kuwa na mwanya lakini siku zinavozidi kwenda napata mwanya na meno yameanza kuelekea upande lakini pia yanalegea.

5.Tabia ya kutumia mdomo kupumua
Kutumia mdomo badala ya pua kupumua inaweza kusababisha mpangilio mbaya wa meno kwani huathiri upana wa mataya. Kupumua kwa mdomo kunaweza kusababishwa na kuzibwa kwa njia ya pua kwasababu mbali mbali ikiwemo uvimbe kwenye tezi zilizopo kooni N.K , lakini pia inaweza kuwa ni tabia ya mtu tu (habitual mouth breathing)

UFANYE NINI KAMA TAYARI UNA TATIZO HILI?
Unatakiwa kumuona daktari wa kinywa na meno aliyekaribu na wewe, na kama upo Dar es salaam/ Pwani na Maeneo Jirani

unaweza kuwasiliana na daktari kwa namba hizi: 0658 950 085
Kupata suluhisho la tatizo hilo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…