chichi pilato
Senior Member
- May 26, 2019
- 132
- 97
Toa belt alafu washa usikie kma muungurumo umepungua. Ukipungua cheza na belingi za izo pulls.Mkuu Kichuguu asante sana kwa uzi huu.
Nina Nissan X-Trail ya mwaka 2002, nliinunua kwa mzee mmoja hivi. Ni namba B ila kiukweli mzee aliitunza vizuri sana. Sasa nlipoichukua nadhani nlii-abuse(maji ya Dawassa n.k), nikaitumia kama miezi mitatu ikaanza kuchemsha, nikaipeleka kwa washkaji wa uchochoroni wakaichokonoa mara kadhaa mpaka nlipojua nimeua injini...
Zikifa gar inamiss, inachekewa kuwaka, inazima zima ghafla na inatumia mafuta mengi. Pia mosh unaweza kuwa unatoka wenye harufu ya fuel.Ni zipi dalili za coil zile za kwenye Injini ya 4E kufu ?
Na je ni madhara gani yanaweza kutokeaa baada ya hizo coil kufa?
Nashukuru sana,Japo siye uliyeniuliza swali
Je, ni knock sensor inareport error au knock sensor ni mbovu?
Muhimu kujua pia mambo ya usomaji wa RPM yana uhusiano mkubwa na CRANKSHAFT POSITION SENSOR na KNOCK SENSOR kwapamoja.
Ni moja ya sensor muhimu sana maana inahusika na "timing" ya uchomaji wa mafuta (ignition timing) kwa kuhusishanisha na uelekeo wa piston. (Yaani piston ikiwa juu au top dead center ndo muda wa kuchoma mafuta)Nashukuru sana,
kwa jinsi fundi alivyoniambia ni kuwa knock sensor ndio ina shida!
Mkuu nisidie manua book ya carina T. INdiyo zipo. Sisi tunalipia kwa mwaka kuweza kusoma service manual ya gari yoyote online. Niambie model ya gari lako na mwaka wake kama nitaipata nitadownload na kukuwekea hapa
Nimeshatafutia watu wengi lakini mwishowe inashindikana; nina access na vitabu vya magari ya Kimarekani na Kanada tu. Kwa hiyo nimekuwa nashindwa napata vitabu vya magari mengi yaliyoko Tanzania ambayo siyo ya kimarekani. Kuna baadhi ya magari ya kijapani ambayo kuna model zilizoko Marekani pia kama vile Landcruiser V8 na Camry tunaweza kupata, lakini kwa magari mengi ni mbinde. Hata hivyo nitajaribu nikienda kwenye karakana yetuMkuu nisidie manua book ya carina T. I
Mkui nisaidie hata hizo pdf za magari hayoNimeshatafutia watu wengi lakini mwishowe inashindikana; nina access na vitabu vya magari ya Kimarekani na Kanada tu. Kwa hiyo nimekuwa nashindwa napata vitabu vya magari mengi yaliyoko Tanzania ambayo siyo ya kimarekani. Kuna baadhi ya magari ya kijapani ambayo kuna model zilizoko Marekani pia kama vile Landcruiser V8 na Camry tunaweza kupata, lakini kwa magari mengi ni mbinde. Hata hivyo nitajaribu nikienda kwenye karakana yetu
Nitashukuru sanasawa
Samahani, swali hili sikulion mapema.Habari mkuu,
Nilifanya diagnosis kuhusu gari yangu kuwa speed ndogo na odometer kusoma speed kuwa let's say unaona kabisa upo 70km/hr ila odometer itasoma 95 - 100km/hr.
Mtu wa diagnosis akaniambia strainer na "Knock sensor bank 1" ndio zina shida, je nikibadilisha gari yangu itakuwa poa? Maana hata kubadili gear haipo Safi kuna muda inaishia gear namba 3, gari yangu ni Rav4 kilitime automatic transmission.
Umejibu vizuri. Labda niongezee tu kuwa inawezekana knock sensor yenyewe kufa linaweza lisiwe tatizo kubwa sana, ila tatizo ni pale knock sensor inapeleka message kwenye computer kuwa injini inaunguza mafuta hovyo hovyo yaani kuna uncontrolled milipuko kwenye cylinder. Hilo ndilo jambo baya zaidiNi moja ya sensor muhimu sana maana inahusika na "timing" ya uchomaji wa mafuta (ignition timing) kwa kuhusishanisha na uelekeo wa piston. (Yaani piston ikiwa juu au top dead center ndo muda wa kuchoma mafuta)
Ikiharibika inasababisha gari kutumia mafuta mengi kutokana na mafuta kuchomwa bila mpangilio, kukosa nguvu unapokuwa na spidi au kubeba mzigo, na hata injini ku-knock hivyo ni muhimu sana kuirekebisha mapema
Tumsubiri mkuu Kichuguu atueleweshe zaidi
Most likely fuel pressure regulator yako au fuel pamp vimechoka. Hiyo miss inakuwa inasababishwa na mafuta kuingia kwenye injector yakiwa na pressure ndogo sana hivyo hayachomwi ipasavyo, na ndiyo maana gari inakosa nguvu. Sasa hivi gari litakuwa linakula mafuta sanaWakuu naomba msaada wenu natumia gari aina ya Toyota Raum.
Siku hizi mbili gari yangu imekua ikikosa nguvu haswa mlimani pamoja na kuchelewa kubadili gia pia imeandamwa na miss nyingi.
Injini 4E
Naomba msaada wa ushauri nn cha kufanya
Viongozi habari, nina prado 95, ina tatizo la kuyumba sana barabarani nikiwa spidi kuanzia 70 tu, nimebadilisha vitu vyote vya mbele kama boljoint, tyrod nk, nimepima wheel balancing /alignment, lakini bado, je tatizo linaweza kuwa nini?
Ignition coil zikifa, injini itapa misfire; na madhara yake ni kuwa zikifa zote, basi injini haiwaki. Na iwapo zitakufa baadhi halafu ukaendelea kuendesha gari na miss hizo basi utakuwa unaharibu main bearing za gari yote na unaweza kuua injini ikahitaji overhaul.Ni zipi dalili za coil zile za kwenye Injini ya 4E kufu ?
Na je ni madhara gani yanaweza kutokeaa baada ya hizo coil kufa?
Oxygen sensor na spark plugs hazikuwa na umuhimu wa kubadili labda kama kulikuwa na dalili nyingine lakini siyo hiyo ya coolant kuisha haraka. Jibu kamili la kukusaidia linahitaji ukaguzi wa sehemu kadhaa za injini yako. (1) Cylinder head gasket umesema umebadili, hilo linaweza kuwa ni jambo jema kwa sababu cylinder head gasket huweza kusababisha maji yavuje na kuingia kwenye cylinder, jambo ambalo siyo zuri kwa uhai wa injini. (2) Kuna jambo amabalo hukuliongelea ni hali ya oil wakati wa kubadilisha.Kichuguu
Gari yangu ina shida ifuatayo.
Mwanzo ilikuwa na shida ya coolant kuisha haraka.
Nikabadili radiator top cover na cylinder head gasket na oxygen sensor bank 1 na plugs zote...