Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

ATF (gear box oil) haishauriwi kuibadili mara kwa mara katika mazingira ya uendeshaji wa kawaida. Unless kama zitakuwepo sababu nyingine za msingi sana za kukulazimu kubadili. Naamini hata kwenye dip stick ya gear box utakutana na maandishi yakisoma "do not change ATF under normal driving conditions'...
Zingatia hayo...
Oil ya engine jina la kampuni halisaidii sana ila gredi ya oil husika ndio inasaidia. Kwa gari lako na mazingira ya Mbeya weka oil ya 5W30 fully synthetic... Hapo oil zenye hiyo specification ni kama Castrol, Atlantic, Puma na Total....

Mwenye thread yake atakuja na ufafanuzi zaidi
 
Je kwa gar manual yenye umr mrefu oil gan nzur.ofckoz recommended ni hizi 5w30 ila hii kwa engine yenye low milage.je kwa gar iliyotembea almost 200000? Na hio atf ni kila gari?
 
Kwenye dipstick ya gearbox ya gari yangu imeandikwa kwamba kwa uendeshaji wa kawaida wa gari, hakuna haja ya kubadilisha ATF. Hili limekaaje mkuu?
 
Ndiyo zipo. Sisi tunalipia kwa mwaka kuweza kusoma service manual ya gari yoyote online. Niambie model ya gari lako na mwaka wake kama nitaipata nitadownload na kukuwekea hapa
Mimi yangu ni Toyota Succeed.
Model code: NCP59G-FWPLK
Vin: NCP590003329
Product date: 2002/10

Nitafutie hiyo manual ya kiingereza. Halafu niambie niandae kiasi gani?
 
Kwenye dipstick ya gearbox ya gari yangu imeandikwa kwamba kwa uendeshaji wa kawaida wa gari, hakuna haja ya kubadilisha ATF. Hili limekaaje mkuu?
Kwa uendeshaji wa kawaida, ATF haibadilishwi ila baada ya muda mrefu ni lazima ibadilishwe kwa vile gearbox ina husiana na vyuma kusagiika na hivyo oil inakuwa na vipande vingi vya chuma. Baada ya km 250,000 itakulazimu ubadili ATF yako
 
Hiii imekaa vizuri
 
Baada ya maili 150000 au km 250,000 ni lazima ubadili ATF; huo ni umbali mrefu sana kwa waendeshaji wa Marekani na Japan, hivyo hawabadili ATF. Ila iwapo unaendesha Tanganyika hadi kufikia km 250k ni lazima ubadili hiyo ATF, na mimi nitakushauri ubadili ATF ukishafikia km200,000 tu.
 
Leo nimeimwaga rasmi Oil ya 20w50 kwenye baby walker yangu 1zzfe 1790 niliyoshauriwa kipindi choote na fundi wa chin ya muembe baada ya kusoma uzii huu mwanzo mwisho nimeweka total 5w30,,,nitawapa mrejesho chochote kitakachojili
 
Mimi yangu ni Toyota Succeed.
Model code: NCP59G-FWPLK
Vin: NCP590003329
Product date: 2002/10

Nitafutie hiyo manual ya kiingereza. Halafu niambie niandae kiasi gani?
Kichuguu, unasemaje juu ya manual ya gari hiyo hapo juu?
 
Kuna shida ya oil kupungua kila nikipima dipstick. Hakuna leakage yoyote, hakuna moshi wala oil kwenye exhaust, isipokuwa kuna masizi (smoke) tu. Na asubuhi ninapowasha gari, kunatoka maji kwenye exhaust. Nguvu ya engine iko pale pale. Shida ni nini mkuu?
 
Kichuguu, unasemaje juu ya manual ya gari hiyo hapo juu?
Nikumbushe tena baada ya mwaka mpya kwa vile sasa hivi niko kwenye mithani, na nikimaliza mitahani sitakwenda kwenye karakaraka yetu kwani itakuwa imefungwa kwa ajili ya Krismas hadi tarehe 3 January.
 
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha hilo litokeaa ila katiaka mazingira unayoeleza ni uwezekana mkubwa ni kwam injini yako inavuja oil ambayo inaingia kwenye colling system na kuyeyukia huko. Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha hali hiyo; vingienvyo huenda injini yako inachoma oild kwa kiwango kdiopgokdigo bila kutoa moshi lakini baada ya muda inakuwa imeshachoma oily nyingi sana; hali hiyo nayo husabababishwa na mambo kadhaa.

Cha kwanza kabisa anza na ukaguzi wa radiator yako kama utaikuta na oil ndani yake. Baada ya hapo ndipo tuambizane ni sababu gani zinazosababisha oil inngia kwenye cooling system
 
Gari yangu ina tatizo kama hili la oil kupungua,
Haina changamoto yoyote kwenye speed au nguvu.
Tatizo wakati wa kuiwasha asubh kama itakuwa imekaa siku bila kuiwasha inatoa moshi na pop sound.
 
Gari yangu ina tatizo kama hili la oil kupungua,
Haina changamoto yoyote kwenye speed au nguvu.
Tatizo wakati wa kuiwasha asubh kama itakuwa imekaa siku bila kuiwasha inatoa moshi na pop sound.
Tatizo hili mafundi wamekula hela yangu sana na tatizo bado lipo, nimelikubal !
Ushaur wako mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…