Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Asante saaana kwa nafas hiyo. Mimi naomba unishauri nitumie oil gani ya engine na gearbox ambapo gari ni Toyota Premio yenye cc 1490 ya mwaka 2005 na mpaka sasa imetembea jumla ya km 71,179 na hiyo oil nibadili kila baada ya km ngap kwan wapo wanaoshaur km 3000 na km5000!!

Pia naomba unijuze ipi oil nzur kati ya Total na Castrol ambapo mm ni mkaazi wa mkoani mbeya ambapo hali ya hewa huku n baridi.

Asante boss!
ATF (gear box oil) haishauriwi kuibadili mara kwa mara katika mazingira ya uendeshaji wa kawaida. Unless kama zitakuwepo sababu nyingine za msingi sana za kukulazimu kubadili. Naamini hata kwenye dip stick ya gear box utakutana na maandishi yakisoma "do not change ATF under normal driving conditions'...
Zingatia hayo...
Oil ya engine jina la kampuni halisaidii sana ila gredi ya oil husika ndio inasaidia. Kwa gari lako na mazingira ya Mbeya weka oil ya 5W30 fully synthetic... Hapo oil zenye hiyo specification ni kama Castrol, Atlantic, Puma na Total....

Mwenye thread yake atakuja na ufafanuzi zaidi
 
(1) Nafikiri nilishakujibu katika thread nyingine. Engine oil kwa nchi za joto tumia full Synthetic 5W-30 au 10W-30 ingawa. Nakushauri zaidi utumia 10W-30. Uchaguzi wa brand gani ya oil, sisi kiufundi hatuoni tofauti yoyote kabisa labda kampuni iandike 10W-30 kumbe siyo oil hiyo, lakini kama TBS inafanya kazi zake sawasawa, zote Castrol, Total, na oil zote zenye namba hizo zitakuwa ni sawa tu. Kuna watu wanakuwa washabiki wa brand fulani lakini kiufundi hakuna tofauti kabisa.

(2) Kuhusu ubadilishaji wa oil, usifuate urefu wa safari au urefu wa muda tangu umeweka oil tu. Ingawa magari mengi ya kijapani wanashauri kila baada km 8,000 au baada ya miezi 6, usiamani sana hizo namba. Fanya mambo mawili, kila wiki uwe unapima ile dipstick, na kuangalia rangi ya oil imebadiliakaje. Kwa vile wewe siyo fundi, swala la rangi ya oil labda halitakusaidia sana, lakini upime dipstick kila wiki na ukiona oil imeshapungua chini ya kiwango, basi mwaga oil yote ya zamani uweke mpya wala usiongezee tu; unapobadilisha oil ubadilishe pia oil filter. Ukifikisha miezi 6 au km 8,000 wakati oil iko level ile ile basi ubadilishe oil hiyo wakati huo. Wakati mwingine muungurumo wa injini unapobadilika basi ujue pia kuwa ni muda wa kubadili oili. Sijui kama maelezo hayo yamesaidia.

(3) Kuhusu mafuta ya Transmission (ATF) pia nilikueleza kuwa tumia mafuta halisi ya kulingana na ilivyoelezwa na mtengenezaji, sijui ilikuwa Type T-IV kama ninakumbuka. Acha gari lipoe, mwaga mafuta yote ya zamani, badilisha transmission oil filter, halafu weka mafuta mapya; usiongezee tu. Kuna magari mengine hayana plug ya kumwagia mafuta ya transmission, kwa hiyo utalazimika uonde transmission fluid sump na utatakiwa uweke na gasket mpya. Uzuri ni kuwa ukibadilisha transmission fluid, unarefusha maisha ya gearbox yako umbali wa km150,000 tena bila matatizo yoyote.
Je kwa gar manual yenye umr mrefu oil gan nzur.ofckoz recommended ni hizi 5w30 ila hii kwa engine yenye low milage.je kwa gar iliyotembea almost 200000? Na hio atf ni kila gari?
 
Kwenye dipstick ya gearbox ya gari yangu imeandikwa kwamba kwa uendeshaji wa kawaida wa gari, hakuna haja ya kubadilisha ATF. Hili limekaaje mkuu?
 
Ndiyo zipo. Sisi tunalipia kwa mwaka kuweza kusoma service manual ya gari yoyote online. Niambie model ya gari lako na mwaka wake kama nitaipata nitadownload na kukuwekea hapa
Mimi yangu ni Toyota Succeed.
Model code: NCP59G-FWPLK
Vin: NCP590003329
Product date: 2002/10

Nitafutie hiyo manual ya kiingereza. Halafu niambie niandae kiasi gani?
 
Kwenye dipstick ya gearbox ya gari yangu imeandikwa kwamba kwa uendeshaji wa kawaida wa gari, hakuna haja ya kubadilisha ATF. Hili limekaaje mkuu?
Kwa uendeshaji wa kawaida, ATF haibadilishwi ila baada ya muda mrefu ni lazima ibadilishwe kwa vile gearbox ina husiana na vyuma kusagiika na hivyo oil inakuwa na vipande vingi vya chuma. Baada ya km 250,000 itakulazimu ubadili ATF yako
 
Model gani hiyo inayosema uwekw kwenye P kwanza kabla ya kusimama ? Kuna transmission nyingiune hazihami position wakati injini iko off

Utaratibu wa kawaida ni huu :
(1) kanyaga breki ya pedal mpaka mwisho,
(2) Weka gear kwenye P,
(3) Weka Parking Brake (handbrake) ukiwa bado umekanyaga Breki ya pedal mpaka mwisho,
(4)Hakikisha madirisha yote yamefungwa
(5) Zima injini kikamilifu uipe kama dakika mbili iache kutikisika.
(6), Chomoa ufunguo kama gari yako inao,
(7) Lock milango yote,
(8) Toka nje ya gari
(9) Funga milango

Tembea kwa mguu uende ofisini mwako au uingie kwenye baa unayokwenda kupoozea kiu. Mambo kwisha.
Hiii imekaa vizuri
 
ATF (gear box oil) haishauriwi kuibadili mara kwa mara katika mazingira ya uendeshaji wa kawaida. Unless kama zitakuwepo sababu nyingine za msingi sana za kukulazimu kubadili. Naamini hata kwenye dip stick ya gear box utakutana na maandishi yakisoma "do not change ATF under normal driving conditions'...
Zingatia hayo...
Oil ya engine jina la kampuni halisaidii sana ila gredi ya oil husika ndio inasaidia. Kwa gari lako na mazingira ya Mbeya weka oil ya 5W30 fully synthetic... Hapo oil zenye hiyo specification ni kama Castrol, Atlantic, Puma na Total....

Mwenye thread yake atakuja na ufafanuzi zaidi
Baada ya maili 150000 au km 250,000 ni lazima ubadili ATF; huo ni umbali mrefu sana kwa waendeshaji wa Marekani na Japan, hivyo hawabadili ATF. Ila iwapo unaendesha Tanganyika hadi kufikia km 250k ni lazima ubadili hiyo ATF, na mimi nitakushauri ubadili ATF ukishafikia km200,000 tu.
 
Leo nimeimwaga rasmi Oil ya 20w50 kwenye baby walker yangu 1zzfe 1790 niliyoshauriwa kipindi choote na fundi wa chin ya muembe baada ya kusoma uzii huu mwanzo mwisho nimeweka total 5w30,,,nitawapa mrejesho chochote kitakachojili
 
Mimi yangu ni Toyota Succeed.
Model code: NCP59G-FWPLK
Vin: NCP590003329
Product date: 2002/10

Nitafutie hiyo manual ya kiingereza. Halafu niambie niandae kiasi gani?
Kichuguu, unasemaje juu ya manual ya gari hiyo hapo juu?
 
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler.

Nimepata license yangu hivi majuzi tu mwaka huu baada ya kuitafuta kwa muda kidogo through part-time activities kwani hiyo siyo kazi yangu kuu.

Certification hiyo inahitaji siyo tu kufaulu mtihani wake, lakini pia uwe na uzoefu wa kutosha kwenye auto-repair shop.

Nimekamilisha experience hiyo inayotakiwa mwaka huu na kupata license yangu.

Kwa vile injini nyingi za petroli zinafanana katika utendaji, jisikie free kuniuliza swali lolote kuhusu matatizo ya injini ya gari yako model yoyote inayotumia mafuta ya petroli.

Siahidi kuwa majibu yangu yote yatakuwa ni sahihi, lakini sehemu kubwa itakuwa ni sahihi, na hata yale ambayo hayatakuwa sahihi yanaweza kukusadia kujua wapi pa kuanzia.
Kuna shida ya oil kupungua kila nikipima dipstick. Hakuna leakage yoyote, hakuna moshi wala oil kwenye exhaust, isipokuwa kuna masizi (smoke) tu. Na asubuhi ninapowasha gari, kunatoka maji kwenye exhaust. Nguvu ya engine iko pale pale. Shida ni nini mkuu?
 
Kichuguu, unasemaje juu ya manual ya gari hiyo hapo juu?
Nikumbushe tena baada ya mwaka mpya kwa vile sasa hivi niko kwenye mithani, na nikimaliza mitahani sitakwenda kwenye karakaraka yetu kwani itakuwa imefungwa kwa ajili ya Krismas hadi tarehe 3 January.
 
Kuna shida ya oil kupungua kila nikipima dipstick. Hakuna leakage yoyote, hakuna moshi wala oil kwenye exhaust, isipokuwa kuna masizi (smoke) tu. Na asubuhi ninapowasha gari, kunatoka maji kwenye exhaust. Nguvu ya engine iko pale pale. Shida ni nini mkuu?
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha hilo litokeaa ila katiaka mazingira unayoeleza ni uwezekana mkubwa ni kwam injini yako inavuja oil ambayo inaingia kwenye colling system na kuyeyukia huko. Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha hali hiyo; vingienvyo huenda injini yako inachoma oild kwa kiwango kdiopgokdigo bila kutoa moshi lakini baada ya muda inakuwa imeshachoma oily nyingi sana; hali hiyo nayo husabababishwa na mambo kadhaa.

Cha kwanza kabisa anza na ukaguzi wa radiator yako kama utaikuta na oil ndani yake. Baada ya hapo ndipo tuambizane ni sababu gani zinazosababisha oil inngia kwenye cooling system
 
Gari yangu ina tatizo kama hili la oil kupungua,
Haina changamoto yoyote kwenye speed au nguvu.
Tatizo wakati wa kuiwasha asubh kama itakuwa imekaa siku bila kuiwasha inatoa moshi na pop sound.
 
Tatizo hili mafundi wamekula hela yangu sana na tatizo bado lipo, nimelikubal !
Ushaur wako mkuu
 
Back
Top Bottom