Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mkuu Carina Ti inawaka taa ya ABS tatizo nini hapo, nimepeleka kwa fundi ikamshinda
Hilo ni tatizo la brake. Kama breki zako zinafanya kazi vizuri, basi huenda umezima (kwa bahati mbaya) anti-lock Brake system yako, au sensor ya speed iliyoko kwenye matairi imeharibika, au mafuta ya breki yamepungua kwenye master cylinder yako.
 
Kichuguu
Habari yako Mkuu!
Naomba ufafanuzi wa tatizo nimeliona katika gari yangu ni Toyota Crown Athlete, 4GR injini ya mwaka 2005 kama ifuatavyo:

1. Kuna muda kama mara mbili hv au tatu imekuwa ikitoa moshi mweupe kwa muda kidogo km sekunde 10 na unakata

2. Injini oil nimepima imepungua kutokana na kiwango kilichowekwa na kwa kile kipimo cha deep stick. Hakuna leakage yoyote na gari ina nguvu kama kawaida

Mabadiliko niliyowahi kufanya mara ya mwisho
Kwa kawaida huwa natumia injini oil aina ya Tota Quatz 5W40, lakini mara ya mwisho nilikuwa na changamoto ya msiba ambao ulikuwa mkoani hvy kutokana na ughafla wa jambo hili ilibidi nitoke na kwenda huko. Wakati huo tayari kilomita za kubadilisha oil zilikuwa zimefika hivyo ikawa sina budi kubadilisha oil lakini nilitumia aina nyingine ambayo ni Atlantic 5W30 kutokana na kukosa oil ya Total Quartz 5W40. Takribani gari imeshatembea kilomita 2400 ndiyo hali hiyo nimeiona. Tayari nimeshapanga kubadilisha oil, lakini niliomba kupata ufafanuzi wa suala hili

Note: kuna maelezo umetoa kwa mdau mmoja hv nadhan wa rav 4, juu ya suala la moshi na namna ya kupima nimefanya sioni dalili yyt ya maziwa maziwa wala povu ktk rejeta
Suspect mkubwa kwako ni kuwa valve zimeanza kuvuja; tafuta fundi akukagulia valve seals, nadhani zimeshapanuka sana zinaanza kuvujisha oil pole pole, baada ya muda injini itakuwa inatoa moshi sana
 
Ahsante nafanyia kazi ntaleta mrejesho
 
Hapana, hayuko sahihi. Inabidi utoe maelezo zaidi kujibu maswali yafuatayo ili kukupa information zinazaoweza kukusaidia.

(1) je Inakula oil sana? (2) Je inakula coolant sana? (3) Je injini ina nguvu au mpaka ukanyage accelerator hadi kwenye bati ndipo iende? (4) Je inakula mafuta sana?

Nikipata majibu ya maswali haya ninaweza kukupa informatio nzuri za kukusaidia.
Kuhusu kula oil sana hapana na kuhusu coolant sina uhakika maana nina muda sijaweka coolant.

Huwa ninaweka maji kwenye coolant.

Ila kuhusu nguvu hilo nakubali gari haina nguvu sana, kuna muda ilifika hata kimlima kidogo tu inashindwa kupanda mpaka nilivyobadirisha plugs ndio kidogo ikawa na nguvu.

Ila nikiwasha Ac inapoteza nguvu kabisa.

Pia inakula mafuta sana.
 
Na wewe valve seals zako zimekufa. Kuna mwingine naye nimemshauri hivyo leo. Mafundi wetu wengi huwa hawajui umuhimu wa valve seals, na ni wepesi wa kukimbilia engine overhaul badala ya kurekebisha jambo dogo kama hilo. Inawezekana hata ulipobadilisha piston rings mara ya kwanza ilikuwa siyo lazima kabisa
 
Kwahiyo mkuu, unamaanisha nikibadirisha valve seals hilo tatizo la moshi litaisha na nguvu itarudi kama mwanzo.
Au valve seals zitatatua changamoto ipi katika hizo.?
 
Tatizo lote: Injini kukosa nguvu nia kwa sababu pressure inavuja kupitia hizo valve seals, halafu injini kutoa moshi ni kwa sababu oil na maji yanaingia kwenye combustion chamber kupitia kwenye valve. Kwa tatizo lako ni lazima oil na coolant viwe vinapungua kwa kiasi fulani ingawa unasema hujaona kupungua kwa oil.
 
Mkuu nimetafuta oil ya Castrol 10w 30 nimekosa je naweza tumia namba gani nyingine??? Kuna 5w30,5w40 na 10w40.

Kwa upande wa 10w30 kuna oil ya atlantic ila sijajua bado ubora wake na sijawah itumia msaada mkuu Kichuguu
Hata ukipata Oil ya liquimoly 10w30 ni nzuri kuliko Castrol na ni ghali kuliko Castrol. Mimi nimeweka kwenye gari yangu, it is running like new
 
Tatizo lote: Injini kukosa nguvu nia kwa sababu pressure inavuja kupitia hizo valve seals, halafu injini kutoa moshi ni kwa sababu oil na maji yanaingia kwenye combustion chamber kupitia kwenye valve. Kwa tatizo lako ni lazima oil na coolant viwe vinapungua kwa kiasi fulani ingawa unasema hujaona kupungua kwa oil.
Ahsante Mkuu!
Ngoja nilifanyie kazi then nitakupa mrejesho.
 
Naombeni msaada viongozi..
Pikipiki aina ya Yamaha na tatizo la kuzima likiwa kwenye mwendo na baada ya injini kupoa ndio unaweza kuliwasha.
Linaweza kuwa ni tataizo gani ??
 
Kichuguu
Habari yako Mkuu!
Naomba ufafanuzi wa tatizo nimeliona katika gari yangu ni Toyota Crown Athlete, 4GR injini ya mwaka 2005 kama ifuatavyo:

1. Kuna muda kama mara mbili hv au tatu imekuwa ikitoa moshi mweupe kwa muda kidogo km sekunde 10 na unakata

2. Injini oil nimepima imepungua kutokana na kiwango kilichowekwa na kwa kile kipimo cha deep stick. Hakuna leakage yoyote na gari ina nguvu kama kawaida

Mabadiliko niliyowahi kufanya mara ya mwisho
Kwa kawaida huwa natumia injini oil aina ya Tota Quatz 5W40, lakini mara ya mwisho nilikuwa na changamoto ya msiba ambao ulikuwa mkoani hvy kutokana na ughafla wa jambo hili ilibidi nitoke na kwenda huko. Wakati huo tayari kilomita za kubadilisha oil zilikuwa zimefika hivyo ikawa sina budi kubadilisha oil lakini nilitumia aina nyingine ambayo ni Atlantic 5W30 kutokana na kukosa oil ya Total Quartz 5W40. Takribani gari imeshatembea kilomita 2400 ndiyo hali hiyo nimeiona. Tayari nimeshapanga kubadilisha oil, lakini niliomba kupata ufafanuzi wa suala hili

Note: kuna maelezo umetoa kwa mdau mmoja hv nadhan wa rav 4, juu ya suala la moshi na namna ya kupima nimefanya sioni dalili yyt ya maziwa maziwa wala povu ktk rejeta
@Kichuguu

Mrejesho wa tatizo nililoomba ushauri

Nilienda kwa mafundi wawili mmoja wa umeme na mwingine makenika na kuwaeleza na kuonyesha nilichoandika ktk uzi huu

Ushauri niliopewa kabla ya kuthibitisha suala la oil seals kwa pamoja waliona ni bora kwanza zisafishwe plugs zote kisha niitumie gari kwa japo siku tatu hk nikichunguza moshi kama utaendelea au laa. Zoezi hilo limefanyika leo, plug zilikuwa chafu sana na pia kua njia ya hewa (siijui vema kama ni sahihi maana nakiri si mtaalam wa mambo ya magari) nayo pia wakaisafisha ilikuwa chafu. Baada ya hapo vikafungwa vema kabisa

Matokeo niliyoyapata
1. Gari imekuwa nyepesi mnooo ktk kuongeza mwendo
2. Sijauona moshi kwa safari nilizofanya leo

Baada ya siku tatu, ntarudi tena kuwapa majibu japo niliambiwa kama tatizo litakuwa limeisha bhasi watafungua na tanki la mafuta walisafishe kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa gari
 
Basi kuna dalili nyingine hukuwa umeaziandika; kwa mfano injini kuunguruma vibaya, mtikisiko wa injini na sailensa mbaya.
 
Boss Man Kichuguu, Niko na BMW 5 series 5251 e60 ya 2014, Radio haifanyi ina blink tu, tatizo inaweza kuwa ni nn?

NB: msaada kwa yeyote anayejua pls si lazima awe Kichuguu tu
 
Nina vitz old model.
Imekua na tatizo lakutoa moshi mwingi sana hasa ninapoiwasha ikiwa imepaki mfano asubuhi au muda wowote.
Nilibadirisha ring lakini bado mabadiliko niliyaona kwa muda mfupi then tatizo limejirudia.

Nimeongea na fundi aliebadirisha ring anasema tatizo ni pistons zimekonda so natakiwa nibadirishe na pistons.

Je inaweza kuwa yupo sahihi...? Au ndio mwendelezo wa kunipiga maana mpaka dk hii ameshanipasua sana.
Achana na overhauling.. fundi huyo ajakushauri vizuri. Yawezekana cylinder walls zako zimeisha tanuka, au kaeka rongs ambazo nazo zimeisha choka na hazi tight vizuri against cylinder walls.. kiufupi overhauling haishii kwenye kubadili rings tu, lazima pia upime diameter kila cylinder bore ili ujue nini ufanye,, but all in all you better buy new engine... Pia jua umepata hiyo changamoto kwakua umekua either ukivusha muda wa oil au watunia poor quality oils kama Oryx, gp, lake oil au mogas, au oil with viscosity SAE40
 
Kichuguu
Habari yako Mkuu!
Naomba ufafanuzi wa tatizo nimeliona katika gari yangu ni Toyota Crown Athlete, 4GR injini ya mwaka 2005 kama ifuatavyo:

1. Kuna muda kama mara mbili hv au tatu imekuwa ikitoa moshi mweupe kwa muda kidogo km sekunde 10 na unakata

2. Injini oil nimepima imepungua kutokana na kiwango kilichowekwa na kwa kile kipimo cha deep stick. Hakuna leakage yoyote na gari ina nguvu kama kawaida

Mabadiliko niliyowahi kufanya mara ya mwisho
Kwa kawaida huwa natumia injini oil aina ya Tota Quatz 5W40, lakini mara ya mwisho nilikuwa na changamoto ya msiba ambao ulikuwa mkoani hvy kutokana na ughafla wa jambo hili ilibidi nitoke na kwenda huko. Wakati huo tayari kilomita za kubadilisha oil zilikuwa zimefika hivyo ikawa sina budi kubadilisha oil lakini nilitumia aina nyingine ambayo ni Atlantic 5W30 kutokana na kukosa oil ya Total Quartz 5W40. Takribani gari imeshatembea kilomita 2400 ndiyo hali hiyo nimeiona. Tayari nimeshapanga kubadilisha oil, lakini niliomba kupata ufafanuzi wa suala hili

Note: kuna maelezo umetoa kwa mdau mmoja hv nadhan wa rav 4, juu ya suala la moshi na namna ya kupima nimefanya sioni dalili yyt ya maziwa maziwa wala povu ktk rejeta
Sijajua moahi wako ni wa mamna ganl, kuna ule moshi fulan hivi ambao engine impowashwa unaatoka kama mvuke ukiambatana na maji maji pale engine inapowaka from cold stsrt that is just normal... Kuna moshi mweusi huu unatokana na oil kuingia kwenye combustion chamber na kuchomwa, so exhaust gases zitakazo toka kwenye tail pipe zinakua zina ambatana na moshi mweusi... Gari yenye shida hii pia utakuta inakula oil(kama gari yako inavokula oil), no ukiingiza kidole kwenye tail pipe kwa nyuma utakuta kuna kama masizi meusi yaliyo gandia kwenye end edges za exhaust pipe... nini chanzo-(excessive carbon builds up kwenye njia zinazo drain oil kwenye piston ambayo uchangiwa na kucheleweshwa kwa umwagaji oil kwa wakati, kutumia oil low quality ziziso na detergents za kuzuia excessive carbons formation, lakini pia inaweza sababishwa na rings zilizo anza kuchoka.. (but kama rings zimeanza kuchoka mara nyingi utaona gari inatoa moshi mwanzoni alafu enjini ikisha chemka pistons hu-expand because of heat na kufanya pia rings zitanuke pia hii ufanya rings zi-tight vizuri kwenye cylinder walls na moshi upotea muda mchache baada ya injini kuwaka na kufikia operating temperature.. so nadhan kwa maelezo yako tatizo limaweza kua hapa.. jaribu ku upgrade oil viscosity from 5w-30 to 10w-40 or 10w-30 fully synthetic oil one results kama itapunguza tatizo lako pia tumia oil detergents siku unamwaga oil ili kupunguza carbon builds..

Test nyingine kujua uzima wa engine yako fanya hivi, washa gari mpaka engine ifike kwenye appropriate operating temperature,, then fungua bonet, chomoa deep stick ya oil huku injini ina unguruma, ukiona oil inaruka sana nje mpaka nje kunaloa kabisa na pia kuna moshi, basi ujue you have excessive blow-by.. maana yake rings zimeanza kuchoka.. test hii waweza ifanya hata kwa kutoa mfuniko wa kuingizia oil kwenye injini, ukipata the same results ujue you engine is telling you bye bye
 
Nina vitz old model.
Imekua na tatizo lakutoa moshi mwingi sana hasa ninapoiwasha ikiwa imepaki mfano asubuhi au muda wowote.
Nilibadirisha ring lakini bado mabadiliko niliyaona kwa muda mfupi then tatizo limejirudia.

Nimeongea na fundi aliebadirisha ring anasema tatizo ni pistons zimekonda so natakiwa nibadirishe na pistons.

Je inaweza kuwa yupo sahihi...? Au ndio mwendelezo wa kunipiga maana mpaka dk hii ameshanipasua sana.
Washa gari, subiri injini ichemke to operating temperature, chomoa deepstick ya oil, ukiona oil inaruka mpaka engine bay components zina lowana ujue hamna injini hapo.. na utakuta hata compression ni ndogo na inakula oil kama haina akili nziri na inatoa moshi mweupe.. go buy new engine mswaki... kama engine ni 1sz andaa 1m, kama ni 2sz andaa laki7, kama ni 2nz andaa 1m hakuna namna.. garama za overhaul na ubora wa engine baada ya overhaul bora ununue injini mpya.
 
Naombeni msaada viongozi..
Pikipiki aina ya Yamaha na tatizo la kuzima likiwa kwenye mwendo na baada ya injini kupoa ndio unaweza kuliwasha.
Linaweza kuwa ni tataizo gani ??
An intermittent problem to this motorcycle... Check injini ikisha kua ya moto je plug inaleta moto? Je, ingnation coil inatoa umeme?
 
Back
Top Bottom