Kichuguu
Habari yako Mkuu!
Naomba ufafanuzi wa tatizo nimeliona katika gari yangu ni Toyota Crown Athlete, 4GR injini ya mwaka 2005 kama ifuatavyo:
1. Kuna muda kama mara mbili hv au tatu imekuwa ikitoa moshi mweupe kwa muda kidogo km sekunde 10 na unakata
2. Injini oil nimepima imepungua kutokana na kiwango kilichowekwa na kwa kile kipimo cha deep stick. Hakuna leakage yoyote na gari ina nguvu kama kawaida
Mabadiliko niliyowahi kufanya mara ya mwisho
Kwa kawaida huwa natumia injini oil aina ya Tota Quatz 5W40, lakini mara ya mwisho nilikuwa na changamoto ya msiba ambao ulikuwa mkoani hvy kutokana na ughafla wa jambo hili ilibidi nitoke na kwenda huko. Wakati huo tayari kilomita za kubadilisha oil zilikuwa zimefika hivyo ikawa sina budi kubadilisha oil lakini nilitumia aina nyingine ambayo ni Atlantic 5W30 kutokana na kukosa oil ya Total Quartz 5W40. Takribani gari imeshatembea kilomita 2400 ndiyo hali hiyo nimeiona. Tayari nimeshapanga kubadilisha oil, lakini niliomba kupata ufafanuzi wa suala hili
Note: kuna maelezo umetoa kwa mdau mmoja hv nadhan wa rav 4, juu ya suala la moshi na namna ya kupima nimefanya sioni dalili yyt ya maziwa maziwa wala povu ktk rejeta