Niulize chochote kuhusu Taifa la Burundi

 
Haya twende kazi nieleweshe maana jamaa kala bhndq hajataka hata kunijibu
Hii ni mwaka 1886(jiulize miaka mingapi imepita)!!! Wazungu walivyojua kugawa mipaka, Rwanda ilibaki na jina lake. Burundi ikaitwa “Urundi”. Maana yake ni another. Walikuwa wakisema “Urundi Rwanda”. Nchi mbili zinaunganishwa na kuwa moja!!! Katika utawala wa wakoloni hao, ukanda wa Rwanda na Burundi ulikuwa na mahikamano. Wakaona kuwatawala ni ngumu. Ndipo likaja wazo la kuwagawa makundi sasa. Walianza kupima watu ulefu na upana wa pua. Na uchumi wako. Pua ndefu, uembamba, na ng’ombe nadhani kuanzia 10(hii idadi labda niihakiki), waliitwa watutsi. Na wakapewa mamlaka ya kutawala makabila mengine. Mfupi, mnene, mwenye kujaza kifua, mkulima. Hawa waliitwa wahutu. Wao walikuwa wa kufanya kazi za nguvu, kulima na kadhalika. Likawepo kundi lingine la waiokuwa nacho, walikuwa tu wa kuwinda na kutengeneza yombo vya majumbani(kupikia, kusombea maji)kwa kutumia udongo mfinyanzi, ndo wakaitwa watwa. Watutsi walipendelewa na wazungu, hata kusoma ndo walipewa kipaumbele. Kadri siku zilivyozidi kwenda, wahutu wakaona kwa nini tunyanyaswe, na sisi haya tunaweza! Hapo, ilikuwa ukifuga kufika idadi ya ng’ombe wa kuitwa mtutsi, una upendeleo usio wa kihutu wala wa kitutsi. Ila ulikuwa unaweza kuzaa na mwanamke wa kitutsi. Ndo watu wakaanza sasa kuwa na mchanganyiko wa maumbile. Zile sifa za watutsi, kwa wahutu zikaanza kupatikana. Za wahutu, kwa watutsi pia zikaanza.

Nivuke kidogo. Ukiangalia wanawake wa 1994 kurudi nyuma, sijui Mungu alifanya nini(kama kweli yupo).
Huu ujinga uliendelea sasa, ndo wahutu wakaamua wachukue madaraka. Rwanda mfalme alikimbizwa(alikuwa Mtutsi). Burundi ikawa hivo hivo. Watutsi nao wakaona haiwezekani. Ndo unasikia Burundi maraisi waliopinduliwa na kuuwawa. Juzi tu, mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD alisema haitawahi kutokea nchi ikarudi mikononi mwa kabila hilo. Rwanda na ko 1994, madaraka ya kihutu yakaisha. Waliokimbizwa, ndo hao unaowasikia FDLR. Mpaka leo, wanahitaji utawala wa kihutu. Je, linawezekana? Haya. Serikali ya Burundi inaongozwa na mhutu. Ya Rwanda inaongozwa na mtutsi. 1994, kuna warundi walikuwa wakimbizi nchini Rwanda, ambao ni wahutu. Waliuwa watu Rwanda. Vita vilipoanza, walirudi kwao. Mpaka leo, serikali ya Rwanda inalalamika Burundi haijawahikuwafikisha mahakamani. Na Burundi haijali kwa sababu waliuwa watutsi. Hapa ndo ujue kisa cha uhasama wa Burundi na Rwanda, mpaka huko Congo jeshi la Burundi linasagwa kama siafu.


Kwa sasa nichie hapa, ni stori ndefu sana tena sana. Ila kama una maswali uliza, ntakujibu.
 
Kwenu ni wapi huko Burundi japo unajiita Ngara? Je Burundi bado ni taifa au mkusanyiko wa maskini wa kawaida?
 
Unatuzuia kuwaza ngono huoni kama unavunja haki za binadamu? Tumeshindwa kutoa inventor hata mmoja sahivi taifa zima tunamtegemea masudi kipanya katengeneza gari kaifungia matairi ya bajaji sasa hata kwenye ngono tufeli?
😄😄😄😄😄😄 Mwanangu seriously mi comments Zako huwa nainjoi tuu (nacheka sana)

Sijui kwanini au kwa kuwa hata kwenye id yako haupo serious. Is lucha again it's lucha again kutetea ngono 😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄
 
Vipi kuhusu intermarriage? Wahutu na watusi wanaoana au bado wanabaguana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…