Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Ila yote mchiriku Na mnanda ndo zao la singeli waimba singeli wamwanzo kabsa wametokea huko huko kwenye mchiriku na mnanda.
 
Yeah! Yeah
walikuuwa na kibwagizo chao
Maswala kudensa ooh
Maswala kubembea ooh


Kwaa jinsi familia yangu ya upande wa mama ikivyokua inaishi ningeendelea kuishi MWANANYAMALA hakika ningepotea mabinti nilichoza nao na washkaji asilimia kubwa wamepoteza kabisaa
 
Mwenyewe ni mhanga wa hii, ilikua keko magurumbasi, nimesimama mbele ya mlango naangalia vitu, kurudi ndani wameshapita na radio
Kwanza wanapokaribia kufanya uhalifu wanaongea kwa code,waimbaji na wapigaji watapiga mziki mtamu sana unaopendwa na wengi huku stage show mmoja mahili atakua ananengua,mfano Vanndame(Atomic)au Saidi Kitinike(Seven) hivyo watu lazima mkusanyike kwenda kushangaa!.Basi utasikia anaitwa "Saidi mwana wa Pembe,kasole ubwele",basi jua viwalo ndani vinaibiwa huko.Hadi mlinzi ukirudi lindoni baada ya kushangaa miondoko unakuta hakuna kitu!.
 
Ila yote mchiriku Na mnanda ndo zao la singeli waimba singeli wamwanzo kabsa wametokea huko huko kwenye mchiriku na mnanda.
Singeli ni zao la KIGODOLO virtua DJ ndo ilihasisi SINGELI
Madogo walianza kwa kuzikimbiza taarabu wanapandisha pinch taarabu inaenda mperampela huku wanaingiza vionjo vyao na virtuar dj baadae wakawa wanaingiza mashaili yao
Sasa kukiwa na kigodolo mtaani mtu anachukuaa mic anatambaa na biti zao walizotengeneza kibingwa na fluityloops
Mwisho sasa watu wakaanza kurecody nyimbo full kabisa na FL studio
Kiuhalisia waimba singeli wa mwanzo hawakutokea kabisa kwenye mnanda

Msaga sumu ndo alikuwa mdau mkubwa aneyejulikana kwa kutia vionjo nyimbo nyingi za taarab

Km wewe mtoto wa kishua huwezi elewa hii coment ila watoto poli watakuwa wamenielewa
 
Ila yote mchiriku Na mnanda ndo zao la singeli waimba singeli wamwanzo kabsa wametokea huko huko kwenye mchiriku na mnanda.
Singeli ni cycle (mzunguko ule ule wa mnanda.Mziki huu hapo mwanzo ulikua ukiitwa chakacha na upigaji wake uliambatana na magita,bendi maarufu zilikua kama Dar Nyota na Night Star ya akina Haidary Kessy.

Baadae mziki ukaporwa na watoto wa kihuni kutoka uswahilini na kuufanyia maboresho uwe wa kuchezeka na ndipo ukahama kutoka Chakacha kuja mchiriku miaka ya 90,na bendi iliyotamba sana wakati huo ni Hisani Gari kubwa (Meli ya sumu.

Kadiri muda ulivyokua unasonga ndivyo makundi mengi yakaanza kutapakaa ndani ya jiji la Dar na kila moja likibuni miondoko ya kuvutia mashabiki,na hapo ndio ilipoibuka miondoko mipya ya "Limba" kwa maana ya kupiga sana kinanda tena kiufundi baada ya kumaliza kuimba,anga hizi fundi alikua Omary Omary (Atomic Music)na hasimu wake ni Hassan Chuna (Kombora Music) na kwa mbali vibendi vidogo kama vile New Kiwembe(Mwina).

Baadae ukavuka kuja stage ya "Kitapa",hapa jamii ilishakua na uwelewa wa kutosha kuhusu mnanda na hivyo ili uwashike watu ni lazima ufundi utimie kuanzia Ngoma(dumbaki),kinanda(Njia)na vionjo(kurap).Hapa ndipo inapoibuka bend kama Seven Survivor iliyokuja kuleta mageuzi makubwa na kuwakamata watu kwa kuuteka mziki wote wa Temeke.
 
Ukiwa unacheza mnanda kamaa GITA limefungwa mtaani Goma likikolea wakitia kibwagizo
"mikono juu mikono juu" usinyooshe
ile kususha chini kama men mfukoni washapita navyo kitambo ukijisachi hamna kitu
 

Mkuu ni kweli miaka ya 90 mnanda ndio ulikuwa kwenye chati sikumbuki vikuti vya enzi zile sana ila nyimbo zao nazikumbuka sana nakumbuka kuna Super Topaz au AJAX...Ebu tupia minanda ya 90s.
 
Singeli ni chakacha iliyoboreshwa tu kwa kunogeshwa na punch za kukiimbiza ili kuleta miondoko ya uchezaji,lakini bado wako kwenye mzunguko wa mchiriku.Kwani huku mwishoni hukuwaona watu Kama akina Omary Omary,Dogo Mfaume,Lupozi mwenyewe walikua wana wanapiga chakacha?.

Hivyo mwisho wa siku utasikia watu wa singeli wanatafuta vifaa ili wapige live na hapo ndio mnanda utakua umerufi kwa mlango wa nyuma lakini tofauti ni miondoko tu.
 
Mkuu ni kweli miaka ya 90 mnanda ndio ulikuwa kwenye chati sikumbuki vikuti vya enzi zile sana ila nyimbo zao nazikumbuka sana nakumbuka kuna Super Topaz au AJAX...Ebu tupia minanda ya 90s.
Yaah,wajanja wa Temeke hao,wakati huo Omary Omary ndio anachipukia.Kikubwa kinachonigomba ni tecnolgia,kwani nyimbo nyingi ninazo kwenye maflashi na tape za redio cassete,sasa namna ya kuzihamisha kuja kuwatupia ndio mbinde,na kama mjuavyo kwa sie wajanja wa kitambo,elimu sio kivile wana[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mkuu ukienda K/koo wapo wataalamu wa kutoa/convert nyimbo za kwenye Tape kwenda Mp3.
 
Mungu alipanga kukunusuru sister,mida hii ungekua aidha ushakufa au uko tikitiki kwa unga,bange au gongo na udangaji wa kiboya!.
 
Bwana kicheko sina ubaya nae
Bwana sidibe sina ubaya naye
Bwana mfaume sina ubaya
 
hahahaahahahh hapo Farmer Gusta enzi hizoo palikua na kibustani cha michongoma kabisaa pale ambapo leo hii pana jumba la kutupia taka
wanikumbusha watoto wa Mzee Mangusiroo, kina Kabwe na nduguye Kipaka,
enzi za Double Ommy na Atomic music
mikoroshini ilikua motooooo
 
Palikua panavuta ganja yakutosha..
 
Hapo Tops kulikua na wahuni wakutosha na ndio ilisababisha zile maskani ( garden ) kupigwa marufuku maana ilikua ganja ganjani unga ngada kwa kwenda mbele.kulikua na vile vikundi vya komando yosso kama wale panya road.Usisahau wale wahuni wa pale mwembeyanga Farmer Gusta
 
Walikua ni wahuni haswa lakini matusi kwenye nyimbo zao ilikua ni mwiko kabisa mkuu tofauti na hawa mashololo wa siku izi nyimbo zao matusi mwanzo mwisho.mtu kama akina Juma nature ndio wametokea huku ndio maana kwenye mistari yao kulikua na maneno mengi sana ya kiswahili ambapo mtindo wao ilikua ni rap katuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…