Mkama Shapu huyu alikua ni askari polisi aliewahi kufanya kazi mitaa ya Temeke na baadae kituo cha Msimbazi kama sikosei,huyu alikua ni mdau mkubwa wa mziki wa mchiriku kwa wakati huo na bendi ya mwanzo maarufu kuipa saport ni bendi ya Night Star iliyokuwa chini ya Haidari Kesi.Mkama Shapu mdau mkubwa wa mchuliku.. Kile kikundi chake cha Mchiliku kilitwaje?
Hisani ngoma ilikiwa na mwimbaji wake wa kike, Aligongwa na gari asubuhi mitaa ya Faya, Kutokana na ile ajali wakatunga nyimbo uke mwimbo nimeusahau jina.. Unaitwaje? Kama uko nao tuwekee hapa...
Hussein Mwinyi sasa Rais Zanzibar alikuwa mdau mkubwa wa Hisani ngoma (Mchiliku) unakumbuka aliwahi kutungiwa nyimbo? Mbali na ule ya aliyotungiwa Baba yake Mzee Mwinyi kipindi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Mkuu huu mziki ni full masela.. Old is Nile..
Yeah ni kweli mdau,lakini kiuhalisia yatupasa sote tuupende mziki huu na kuufuatilia ili urudi kwenye peak,sababu ni mziki halisi kabisa wa Kitanzania uliobuniwa hapahapa nchini kwetu.Na isitoshe umesheheni mashairi murua na mazito yenye kuigusa jamii nzima ya Kitanzania,kilichouharibia mziki huu ni kundi la mashabiki vijana waliojawa na mihemko ya kiuni tuwewe kweli ni shabiki wa mchiriku
Chaukucha family #Watoto wadogo waliokomaa vichwa( maskani ya Mwananyamala kwa Kopa) ni moja kati ya bendi zilizomaarufu sana kwenye tune ya mziki wa Kinondoni.Huku mwishoni kuna kundi la wasanii nguli na wakongwe walimeguka kutoka Jagwa Music kutokana na malumbano ya mgongano wa kimaslahi na kwenda kujiunga na Chaukucha(wengine walikulia humo kimuziki) na hatimaye kuzuka tungo tata na vijembe kwenye nyimbo zao.Mimi ni mpz mkubwa wa Jagwa,ila jana usiku E FM walikuwa wanapiga ngoma za Chaukucha family kumbe nao ni wakali aisee,kuna ngoma moja wanasema dogo Jack Simela kuwa anafanya mchezo wa kurudi nyuma,iko pow sana,sijui inaitwaje
Mkuu usijali maana niko mbioni kufanya kitu kama na wabobezi wenzangu wa tasnia ya mchiriku,itakayoambatana na Mchiriku Summit kitaifa.Mkuu huwezi tengeneza link tukazipata hizi ngoma aisee...you tube zipo kwa uchache uchachee Sana...
Binafsi nimeahiriki Sana minara ya 7 survivor na Jagwaa enzi hizo wakati nikiwa Naishi Alimaua Campona Camp.
Yaani zile harakati fulani za kihuni ambazo zilitafsiriwa kama ndio ujanja kwa maisha ya levelMkuu Namichiga umenikumbusha mbali Sana. Mwaka 1996 mitaa ya Tandika Azimio,Dmaeks,Mashine ya Maji, Sandali nk.
Nashukuru kuishi kwenye haya mazingira na kutoka salama bila kuvuta sigara wala bangi au kukaba na mchana kupiga ndole ROAD..
Nashukuru basics za Karate zilinifanya niogopwe na kuwa huru kwenye mitaa ya kibishi ya Tandika.
Mkuu @namachinga mpaka hivi Sasa kila Jumamos jagwa hua wanapiga hayo maeneo??Jagwa Music,chini ya utawala wa marehemu baba J ndio ilipoanza kupata umaarufu mkubwa na hatimaye kuwa mrithi wa Hisani Gari kubwa pale Mwananyamala.Kila j'mosi watu wanaruka pale CCM Mwin'juma.
Yaah hao ni Atomic Music chini ya mafundi kama akina Omary Omary,Saidi Ndiga,Mwamkoto Ngoma,Nanga boy Simela(Wema Said Nanga) na wengineo.Hiyo Kipaka nyimbo inaitwa Kipaka Memory,wakati hiyo baba Asha in muendelezo kuanzia baba Asha no.1,2,3 na 4.
Hakuna wasanii namba moja kwa umasikini kama wasanii wa mnandaNimeona hizi nyimbo zipo Apple music sijajua Kama wasanii waliopo wa Jagwa wananufaikaa nazo as Kuna malipo yanaingia kwa wanaosikilizaaView attachment 1790384
Hao ni Hisani Gari kubwa( Meli ya sumu).'...Sifa za uzuri wake e e Mwanaidi,
zafanana na tabia yake ee Mwanaidi,
Kwani kaumbika vema aah Mwanaidiii,
Tumsifu Aliyemuumba aah Mwanaidi,
Yaani kwa utaratibu uuh Mwanaidiii,
Kwa jinsi Alivyompamba aah Mwanaidiii..!
Ooh! Mwanaidiii yoooh Mwanaidiii!
Body lako linayumbayumbaa... Mwanaidi, waumiza roho za vijanaaa Mwanaidi
Malkia wa warembo Mwanaidi...
Nasikitika sikumbuki kundi wala mwamba aliyetiririka hiyo mistari.
Mnanda ilikuwa burudani ya kweli!
Manager Gola ndo aliesema hivyoo kua bado wanapiga.Hapana,Jagwa hawana Tena huo utamaduni wa kupiga kila juma mosi pale Mwinjuma.Sababu minanda hapa kati ilishuka trend
Enz hizo maeneo ya TAA NYEKUNDU hadi SANDALI njoo farmer gusta hatari tupuUmenikumbusha temeke mikoroshini