Niwe mmoja wa WanaJF mwenye nyumba kali

Kuna miji nilikuwa nafanyia kazi masuala ya upimaji wa viwanja. Nikakuta mpaka 300sqm. Kuwahoji inakuwaje wakanijibu simple tu, mwongozo wa wizara unaruhusu. Nikawa mpole. Hakika niliona sisi wabongo ni vituko, hatujifunzi kabisa
Duu aisee
Ila wenye nyumba za uhakika ni Moshi mkuu
Yaani unakuta nyumba ina ardhi kubwa haswa hadi unasema hawa wanajua maisha na hawataki tabu

Unatembea hata mile nzima unakuta nyumba Tatu tu au 4
 
Kwenye ujenzi hatukadirii kwa macho.
Huwa tunatumia miongozo ifuatayo;
1. Ku study floor plan na vipimo vyake
2. Cross section inaoonyesha kuanzia kina cha msingi na urefu wa jengo kwenda juu kwa vipimo.
3. Structural ...hii huonyesha layout ambayo huonyesha size za chuma
Idadi ya chuma na mfumo wa usukaji.

Kwa hayo na mengineyo ndipo waweza kkadiria material na gharama ya ujenzi mkuu.

Kupitia vitu hivyo slhesabu yako itakuwa 100% na sio kutumia macho
 
Mkuu

Upo sahihi kabisa

Kenya tu hapo nenda Muthaiga,Karen,etc viwanja ni 5 acres mzee na wana ardhi ndogo kama nchi

Bongo pia tabia zetu kama individuals ni za kipumbavu sana yaani,unakuta mtu humo humo eti anafuga ng'ombe,amejenga upumbavu wa wapangaji chungu nzima na hapo nje kaweka mafremu chungu nzima..na yeye familia yake inakaa hapo hapo...

Yaani kiwanja kilichopimwa still humo humo ndani ya kiwanja owner anageuza squater humo humo ndani kwa kufanya upumbavu wote huu

Zote hizi ni NJAA na mindset za kimasikini kabisa

Hua nashangaa hivi mtu kwenye nyumba yako ya kuishi na familia na mahali pa kulea watoto wako unajenga maduka na baa hapo hapo sijui hizo akili mbovu hivyo zinatoka wapi?I really do not understand this stupidity

Kama ni baa,nunua eneo maalumu,kama ni maduka nunua eneo maalumu,kama ni wapangaji nunua eneo maalumu ufanye yote hayo..

Sio mahali unalelea wanao ndio unafanya ukumamayo wote huo!
 
Nafikiri Kenya na Afrika kusini wametupiga gap kubwa sana
 
Yote hayo unayakuta Tz tu maana hata Burundi wanatuzidi
Mtu unajenga nyumba unaifanya kila kitu under one roof ni ujinga sana

Watz akili zinatufaa sisi tu yaani hatubadiliki kwa kila kitu na wanaona aibu kuiga, wakati kuiga ndio maendeleo

Hebu imagine hata dual citizenship wamegoma kisa woga wa kijinga
Mjadala wa muungano utashangaa ujinga wanaoingea so called wasomi

Ni nchi ambayo hata baada ya miaka 100 watakuwa hivyo hivyo
Utasema vijana watabadili nchi kumbe nao ndio wale wale
Ardhi ya tz leo kungekuwa na miji iliyotanuka na maridadi ila ushamba mwingi sana

Wachaga tu ndio wanajielewa nafikiri maana mpaka nje ya mji ndio wamejenga haswa utasema uko nchi nyingine kabisa
 
Nafikiri kuanzia 70m
Na kama umri umesogea, nyumba ya chini kubwa ni nzuri zaidi

Ili usije kuhangaika kupanda na kushuka
Uzee na gorofa hapana
Maana baadae utalazimika uwe unaishia chini tu [emoji1]
70M labda nyumba ya kawaida yenye finishing ya kawaida.
Mfuko wa cement sasa hv kuna sehemu mpaka 16k mfuko mmoja.
 
Asante mkuu. Ukifuatilia mjadala humu. Huu mjengo hauwezi kufika hiyo amount kwa sababu nimeeleza sio ghorofa.
Hii ni sawa na mtu mwenye watoto 7, akupigie ukiwa mnadani umletee nguo ya mtoto nawe ukanunua hata bila kujua urefu wa mtoto🤣🤣🤣🤣🤣
 
Asante mkuu. Ukifuatilia mjadala humu. Huu mjengo hauwezi kufika hiyo amount kwa sababu nimeeleza sio ghorofa.
Nimeelewa vizuri kuwa ni one storey ila labda uchakachue ila ukiitende haki iwe na hadhi kama.kwa hiyo picha hasa kwenye finishing inafika amin mkuu.
Hapo kuezeka tu ukichukua bati/vigae quality kama.za ALAF na mbao uchukue zile za dawa kweli sio zile feki za bugurun hiyo roofing tu peke.yake 40M inakwenda mkuu.
Material.zimepanda juu sana
 
Kuna watu wana asili ya ubishi hata kama hawajafanya tafiti.

Kuna nyumba najenga hapo Mjini, ni ya ground tu lakini nimeshatumia 135M hadi sasa.

Isingekuwa kujenga kwa awamu nisingeweza kutoboa
Muache adanganywe aishie kati libaki pagala.
Namwambia 250M inaisha anakataa.
 
Una jina la gari niipendayo sana Jeep rubicon
Why isiwe 300m?
Au isiwe 150m?

Kukadiria kwa macho bila kujua;
Ukubwa wa nyumba
Matirio zitakazotumika
Huku ni kutoutendea haki ujenzi.

Ujenzi ni sawa na afya ya mtu ambayo huwezi kumwambia anaumwa kitu gani hadi apitie vipimo.

Unajua uzi huu unapitiwa na watu wengi hivyo kukadiria kwa macho kunaweza kuwaingiza wengine mkenge kuona ujenzi kumbe gharama kubwa au mwingine akaona ni rahisi kutokana na kukadiria bei ndogo au ya juu vyote vina madhara.
 
Mkuu hiyo ni mansion.
Bila hata ya kujua vipimo najua Haiwezi kuwa na udogo wa kujengwa kwa cost chini ya 250M.
Akilazimisha gharama zishushe atajenga ila atakua amejenga kitu kingine.
Najua ninachoongea mkuu sikurupuki.
Why not 150M simply because hiyo ni mansion,sio nyumba ya kawaida.Hilo ni hekalu huitaj vipimo kujua ni jumba kubwa.
Why not 350M or 700M inategemea na mbwembwe zake hasa kwenye finishing.
Kuna watu kwenye finishing wanaagiza container la material Dubai,Italy au Spain ila hizo ni mbwembwe tu lakini hata akijenga kawaida tu 250M inafika.

Hicho anachokiita ki canopy cha kupungia upepo kwa standard nzuri za usalama lazima hela ya maana iingie kwenye hiyo slab itakayomwagwa hapo.Huwez kukijenga kiwnywji enyeji tu kije kiuwe watu
 
Hujasoma ukanielewa.
My concern sio hiyo 250m uliyoitaja kuwa haitafika...but umetumia kigezo gani kuzipata?
 
Hongera kwa kurudishiwa ID yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…