Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

mbona huyu wa maandiko yetu hana wivu huyu wala hana hasira
sisi waislamu na wakristo wote tunamtumikia vizuri tuu
Mbna ana declare atachoma watu sku ya mwisho sio kwasababu hawatendi mema
Ila kwa kutomfuata yani kutamka yesu au Mohammed ndio pona yako.. huo ni upendo?
Na inakuwaj kila dini inajitanabaisha kuwa ni bora kuliko nyingine?
Na inakutaka uifuate yenyew ili iwe salama yako.
au hawa wafia dini wanaoua kwa sababu ya dini huwaoni,
Hata huko ukristo roma limeua watu zaidi ya 50 milion kwa kutumia jina la Mungu.
Leo wote wadai dini zao na Mungu wao ni wa upendo
upendo upi?
 
achana na hao walioua sababu ya dini hao mazuzu
dini bora ni ile inayo mwabudu Mungu wa kweli na

wakristo wote na waislamu tunamwabudu mungu huyo huyo mmoja
ndo maana maandiko yetu hayatofautiani saaana labda kwa mitume wa mwishoni mwishoni huku

sasa wewe unafanya maovu alafu utegemee ukaribishwe vizuri lazma uungue
hakuna msamaha kwa watenda dhambi wasio tubu na kutorudia dhambi zao
 
Hamna sehem hata moja uliyoelezea roho zaidi ya story na Quote ambazo kila mtu anajua kuw roho haina mwili.
Mpaka hapo umekiri ya kuwa nimeelezea Roho ni nini.

Lakini,ku quote si kuelezea au huwezi kuelezea jambo kwa kuquote ? Kijana huu mjadala umekuzidi.

Kingine unacho takiwa ufanye wewe ni ukosoe hicho unacho dai nime quote na uweke kilicho sahihi na utupe na marejeo.
 
Hakuna kitu.. Chui kavaa Ngozi ya kondoo na Roho wa Bwana alinionyesha mapema Sana...
MUNGU NI MFALME, Anaitwa Mwenyezi, Anakaa kwenye kiti cha enzi (SIO KUKAA UNAKOFIKIRI WEWE Mwanadamu, KITI CHA ENZI KINAWAKILISHA Mamlaka na Umiliki Wake..)

Ahadi anazozitoa ni kwasababu AMEWAPA uhuru wa kuchagua Mtakalo, ila KWA WALE watakaomfuata Yeye Hakika watapewa Tuzo ya Ushindi.. Wale wampingao Stahiki yao ni Moto wa Jehanamuuuu...

Mungu wetu Hapendi Kuchanganywa na miungu mingine (KUISHI KWA UONGO)... Yaani mbele za watu unasema Lihimidiwe Jina Lake, Nyuma ya pazia unatumia waganga wakulinde na kukupa mali kwa njia ya kafara za kuzimu.. Mungu lazima awe na wivu, wivu wake ni kwasababu UNAMUHUSISHA na vitu ambavyo havipo sawa na uwezo wake, YAANI ni kumdhalilisha kupita maelezo..

Mungu Yupo.. amekuumba wewe, Ameniumba mimi, alimuumba JF Kennedy, akamuumba Hayati Peter Tosh, amemuumba JPM.
 
Usiniambie nikasome huu ni mjadala wa wazi. Wewe thibitisha kama energy ina hivyo vyote,ukiweza kufanya hivyo naacha kujadili huu mjadala.

Sasa kama ni scientifi proved unacho shindwa kuthibitisha hapa ni nini ? Thibitisha ya kuwa maji yana yajua yanacho kifanya,thibitisha ya kuwa maji yana malengo thibitisha ya kuwa maji yana sanifu jambo kadhalika thibitisha ya kuwa maji yana hekima.
 
unapofikiria kuhusu ulimwengu fikiria kuhusu single atom
Single Atom haya ni mawazo ya wanafalsafa tu ndiyo maana wakatofautiana walianza na mata wakaja na atomu ndiyo ikaja fizikia ya usasa. Hata hao Waatomia hawakuwa na uthibitisho juu ya mawazo yao. Usilete mawazo mfu kijana sisi tunajishughulisha na uhalisia.
unapofikiria kuhusu ulimwengu huu usiende mbali fikria kuhusu single atom.
Kila kitu kimerise huko hai sio, hai. kinaonekana, hakionekan.
Hili huwezi kuthibitisha mpaka unakufa,hizi waasisi wa nadharia hizi ni Wanafalsafa wa kigiriki kina Aristoto hawakuwa na Waatomia hawakuwa na ushahidi wowote zaidi ya nadharia.

Niambie Atomu inafanyaje mpaka ukapatikana wewe ? Hizi akili za kitoto kweli.
Vibration tu ndio inayotofautisha kitu kimoja na kingine.
Thibitisha.
Tukidissolve mwili wako hakuna sehem tutakuta kitu tofauti na atoms.
Hiyo intelligence na memory inaexist wap tofauti na kwenye atom.
Nacheka sana. Hivi unasoma unachokiandika ?
 
Huu uongo ulio semwa sana,bila kukanushwa niambie ulianza kusemwa lini ? Maana sisi tujuavyo tangu zama za mitume wapo watu walio kuwa wanakataa juu ya uwepo wa Mola,rejea habari za Firauni,sasa sijui mnaongelea muda gani ? Lakini Firauni mwisho wa siku alikuja kukiri ya kuwa Mola yupo.

Kuhusu kuthibitisha ya kuwa Mola ametupa pumzi ni rahisi sana,tunarejea katika vitabu alivyo wafunulia mitume wake na mananbii.

Lakini kama huu ni uongo inakuwaje mnashindwa mpaka leo hii kuubatilisha ? Mnaishia kulia lia ?
 
Mimi sipo hapa kukushawishi usimuamin Mungu wako...
Hajatoa uhuru angetoa uhuru asingewaadhibu watu wasipo mfuata.
Ukweli ni nin??
Mungu wako anaukweli upi?
 
Mimi sipo hapa kukushawishi usimuamin Mungu wako...
Hajatoa uhuru angetoa uhuru asingewaadhibu watu wasipo mfuata.
Ukweli ni nin??
Mungu wako anaukweli upi?
SIO WEWE HATA wataliban hawawezi KUNISHAWISHI NISIMUAMINI MUNGU... ALIKONITOA MBALI, ALIYONIFANYIA NI MAKUU SANA Hakuna mfano wake..

Zaburi 25:10
"Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli,
Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake."

Kweli ni njia zote za Bwana, Kwamaana Mungu hasemi na Hajawai kusema Uongo.

Msalimie Mzee Universal conscious.. Mwambie Mungu aliye hai anamsalimia.
 
Na wew niambie Mungu aliufanyaj udongo mpaka ukapatikana wewe?
Mungu hajawahi pingana na sayansi.
Kitu kimoja nina uhakika kuhusu wewe ni kuwa unacombination ya many atoms sio zaid.
ukomplex wako haukufanyi uwe sio atoms.
Law zote yeye ndio creator sasa atapingana vipi nazo.
Tuach kutumia Mungu kama kivuli cha kuficha upuuzi uliopo kwenye dini zetu
msikilize imam.
 
Kila siku nime tamani kuingia katika jukwaa la haya mambo ya dini nimefurahi kuona hii kitu
 
Nimekuambia ukasome nikijua hutaenda kusom
kwasabu you have a blind faith unaamini bila kuhoji imani yako.
kama principle ni kuamini bila kuhoji kila mtu yuko sahihi kwa anacho amini.
lakini sio kila anachoamini mtu kinakuwa kweli.
Mimi iman yangu inaniambia ni utafte ukweli katika kila jambo wewe imani yako inakwambia inamiliki
ukweli wote so huna haja ya kutafta wala kuskiliza chochote nje ya dini yako.
Umezoea school feeding ukimezeshw kila kitu open your mind uexpose what lie beyond your religion.
 
Nimeona kiwete akitembea, mwenye mapepo akifunguliwa hiyo inatosha kuamini katika MUNGU muumba mbingu na ardhi.

Hata kabla ya dini za mashariki ya kati kusambaa duniani bado wamatumbi tulikuwa tunaabudu katika MUNGU, wahindi wekundu wa Amerika walikuwa wakiabudu hivyo hivyo kwa wa Asia halafu leo hii mpuuzi mmoja anakuja na hoja kwamba hofu ya binadamu ndio imepelekea kutengeneza dhana ya 'Umungu'!

Kitu pekee naweza kubaliana na nyinyi huenda dini zikawa hazipo sahihi lakini MUNGU wa kweli muumba mbingu na ardhi yupo alikuwepo na atakuwepo.
 
Twende taratibu jibu maswali ninayo kuuliza kwanza.
 
Kama hali iko hivyi ili ujue nasoma au sisomi jibu hoja zangu hili rahisi sana.
 
Kabada sijacomment chochote nimehitaji kumfaham zaidi mleta mada. Nimeheshim ukomavu wako wa akili kupitia hoja zako kadhaa uliokwisha zileta hapa. Unajua unachokiongea. Kwa faida zaidi naomba kujua uelewa wako kuhusu SHETANI. vipi unaelewa nini likitajwa hilo jina na je yupo?
 
Mmmh dah no comment mkuu.
 
Mtu anayetumia nguvu kuaminisha hakuna MUNGU ni mpuuzi kwa sababu hajui ni kwann watu walio wengi walichagua kuamini uwepo wa MUNGU na haijui dunia isiyo amini katika uwepo wake inafananaje ila anajiona yeye ni exceptional sana na wengine ni wapumbavu. Hapo ndipo upuuzi wake unapokuja.

USHAURI: Hufahamu siri za kaburi, kwa udhaifu huo kwann watu waamini mawazo ya ubongo wako dhaifu ambao pia utaoza?

Kifo kinakuja, kila siku unasogelea siku ambayo utaingia kaburini. Kuwa na subira acha kutumia nguvu kuigeuza dunia kwenye kitu ambacho hukijui.

Umeikuta dunia ikiwa inaamini juu ya uwepo wake, heshimu hilo sidhani kama kuna la kupoteza ewe kiumbe dhaifu.
 
Unaongelea Mungu yupi?
Kama ni wa kwenye bible au Quran tumemuani si zaid ya miak 150 iliyopita.
Waafrika walikuw wamepungukiwa na nin miaka 150 iliyopita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…