Nakutakia kila la kheri kwenye utafiti wako wa miaka miwili
Kupata Muumini wa dini anaye thamini na kujua maana ya utafiti ni nadra, hongera sana
Haya ni baadhi ya makosa niliyoyaona kwenye hoja yako
Taafsiri ya neno Mungu kwa mujibu wa Einstein sio taafsiri ya sayansi kuhusu neno Mungu
Hiyo ilikua ni Personal belief ya Einstein nje kabisa ya kazi yake (Sayansi)
Mpaka sasa, hukuna concept ya Mungu mwenye mainstream science
Unapoanza kuweka sifa kwenye hoja yako ambazo kimsingi ni non falsifiable (hatuwezi kuzi disprove) basi automatically ushaiondoa hoja yako nje ya upembenuzi wa kisayansi
Sayansi imejengwa juu ya Karl Popper Philosophy, msingi wake ni kwamba kila siku sayansi ina jaribu ku disprove hypothesis na sio kuprove kama wengi wanavyoamini
Hypothesis inakua theory pale inapo pass vikwazo hivyo
Mungu haiwezi kuwa hypothesis kwa sababu ni ambiguities zilizopo kwenye taafsiri yake na jinsi gani ilivyo ngumu kui disprove
Sayansi inaweza disprove vipi Mungu asiyeonekana?
Pili, kutumia vitabu vya dini kujenga maana ya neno Mungu sio kosa
Kosa ni kuthibitisha yupo kupitia hicho hicho kitabu cha dini kinachosema yupo
"Biblia ni neno la Mungu, kwa sababu Mungu amesema, ndani ya biblia kuwa biblia ni neno la Mungu'
Hio hoja hapo juu, inazunguka tu hapo hapo (Circular reasoning)
Mi baada ya miaka miwili naamini nitakua hapa, nasubiri matokeo ya utafiti wako