Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

Hiki ndio kitu cha kushangaza kuhusu Mtu anayehisi imani yake ni sahihi wakati hata jinsi ya kujenga hoja za kawaida tu hawezi

Mimi au Mleta mada kutokua mahututi hospitali kuna thibitisha vipi uwepo wa Mungu unayemuamini?

Like serious?
Mimi kutokua mahututi mda huu ni uthibitisho kuwa Mungu yupo?

Vipi kuhusu Mtoto mdogo anayekufa kwa njaa mda huu somalia?

Vipi kuhusu mama anayekufa kwa kujifungua mda huu?
Vipi waliokufa kwa ajari leo?

Hao nao wasemeje? Kuwa hakuna Mungu kwa sababu angekuwepo wasingekua katika dhiki na shida walizo nazo

Kutokuwa na uwezo wa kutetea unachokiamini kwa hoja reasonable ni moja ya udhaifu mkubwa sana,

Ni wazi tu unaamini usichokijua

Hebu seriously, nipe hoja moja tu ya msingi inayokufanya uamini Mungu yupo

Twende na Abrahamic God, kwa sababu huyu ndiye anayeaminiwa na watu wengi humu

Kuna zaidi ya watu 5,000 wanafatilia huu mjadala,

Twende mimi na wewe, nipe hoja za msingi zinazothibitisha Mungu unayemuamini yupo

Then wafatiliaji ambao wapo open minded watajua hoja mbovu na nzuri

Acha hizi hoja za kitoto,cheap mno
 
Hata msimamo wa wanasayansi wengi hawapingi uwepo wa Mungu ila jinsi vitabu vya dini vinavyomuelezea Mungu huyu
Kimsingi huu utetezi umetumia premise yenye Logical fallacy "wanasayansi wengi"unataka kuweka implications ionekane kukiwa na kundi fulani la watu mashuhuri jambo hilo litakua kweli. Pasipo hata kuangalia kama njia iliyotumika kupata jibu imepitia process za kiutafiti mpaka kufikia hitimisho bali uwingi wao ndio kipimo cha kuonesha jambo nila kweli.

Fact ya kwamba wanasayansi wengi hawapingi uwepo wa mungu si sababu ya wewe na mimi kukubali kua kitu hicho ni kweli, Muhimu kufata ukweli na sio personal view ya mtu. Tunazo records za watu mashuhuri wakiwemo wanasayansi waliowahi kuamini vitu vingi vya uongo kua vi vya kweli

Kuna kipindi wanasayansi waliamini matuta ya kichwani yana indicates tabia ya mtu, kwa hiyo kua mwanasayansi hakukufanyi uwe karibu na ukweli kwa kila kitu unachokisema.

Hata kwenye sayansi wazo hua haliaminiki eti kwakua limetolewa na mwanasayansi nguli, hua lina aminika nakuhalalishwa kulingana na evidence iliyo wasilishwa na si vinginevyo

So hao wanasayansi wengi ambao hawapingi uwepo wa Mungu walishawahi kuthibitisha yupo?
 
Naweza nisiweze kukuthibitishia Uwepo wa Mungu kuridhisha akili yako lkn naweza kukudhihirishia Uwepo wa Mungu kwa Imani Yangu kwake.Ikiwa unaona hoja zangu hazina maana basi utanielewa kupitia misimamo yangu ya Kiimani.
 
We hujui hata jinsi ya kusoma na kujibu hoja...
Unajibu tu unavyoelewa wewe

Nimekuuliza kwanini Allah asingeteua katika Kila kabila na kila jamii ya watu, Asia, Ulaya, Africa, America etc mitume yake ambayo ingesambaza ujumbe kuhusu uislamu kwa wakati mmoja tena usiopingana

Njia hii ingekua na manufaa mengi Sana

Moja kusingekua na huu utitiri wa dini nyingi ambazo zinamfanya mtu kutokua kuwa na uhakika ipi ni sahihi

Pili kusingekua na madhehebu mengi katika dini moja kwa sababu wote tungehubiriwa kuhusu habari moja tena katika lugha tunayoifahamu

Tatu, kwa kuwa ingewafikia watu wote kwa pamoja, ingewapa watu wa zama zote fursa moja ya kusikia habari ya ukombozi

Wasioamini wasingekuwepo kabisa au wangekuwa wachache

Mungu muweza wa yote asingeshindwa kuleta dini yake kutumia hii njia, kwa sababu ina faida nyingi bila hasara

Nakuuliza kwanini Allah ameshindwa kutumia hii njia na badala yake akachagua jamii moja tu ya binadamu bila sababu yoyote ile (Racism) na kuanzisha dini yake pale?

Unanambia Mbona hata Yesu alikua muyahudi?
Hapa hujajibu swali kwanini Allah Alishindwa teua mitume kutoka kwenye kila jamii?

Nakuuliza kwanini umefanya jambo fulani, unanambia mbona fulani naye kafanya?
Hapo umejibu swali?

Unanambia pia Mungu hapangiwi cha kufanya, hapa sio kipi apangiwe

Hapa ni ipi ni njia bora zaidi?
Nambie ipi njia bora kati ya kuteua mitume kwa Kila jamii ya watu au kuchagua jamii moja bila Kuwa na sababu yoyote ile?

Halafu hujui hata Historia, Uislamu haukuwepo tangu kuwepo Kwa binadamu

Ni imani ya hivi karibuni, Ukristo tu ulikuwepo kabla yake
Kuna imani na dini kongwe kuliko uislamu

Sasa ukija na utetezi wa kitoto kuwa kila binadam anazaliwa Akiwa muislam utachekesha watu humu

Nakuuliza tena, kwanini Allah hakuchagua mitume kutoka kwenye kila jamii ya watu na kuwapa ujumbe wake?

Badala yake akachagua jamii ya kiarabu bila sababu yoyote?

Dini yoyote ile ni zao au chimbuko la eneo fulani,inaanzishwa na watu wa eneo hilo na mara zote inabeba tamaduni za eneo hilo
 
Naweza nisiweze kukuthibitishia Uwepo wa Mungu kuridhisha akili yako lkn naweza kukudhihirishia Uwepo wa Mungu kwa Imani Yangu kwake.Ikiwa unaona hoja zangu hazina maana basi utanielewa kupitia misimamo yangu ya Kiimani.
Sio unaweza usiweze
Huwezi

Kama unaweza thibitisha kwa hoja hapa

Nambie kwa Premises hizi na hizi zinatoa conclusion hii (kuwa Mungu niliyem define yupo)
 
huo haukuw msingi wa hoja yangu wala sijatumia wingi wao kuhalalisha hoja yangu
ila kujaribu kueleza mtazamo wa baadhi yao
 
Mungu yupi sasa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Nikuulize swali moja mkuu, je wewe binafsi unaamini uwepo wa uchawi duniani, na kama unaamini sayansi inalithibitishaje hili? Na kama hauamini mbona matendo yanafanyika na mm naweza kuwa shuhuda wa hayo na watu zaidi ya mm wanaushuhuda pia. Nisaidie kuhusu hii energy nisiyo ijua kiini chake kimetoka wapi.
 
Kwanini umemtaja Mungu, na kujikita kwemye hoja hiyo, nilidhani kama mtu haamini katika Mungu hakuna sababu hata ya kumtaja maana ni kitu kisichokuwepo.
 
Ukiona simu, gari, meza, nyumba, kuna mtu/watu nyuma ya hivyo vitu walioviunda.

Ni ajabu ukiamua kufumba ufahamu wako kukataa kwamba vitu kama bahari, ardhi, mimea, na sisi binadamu hakuna aliyenyuma ya uwepo wake.
 
Hata mawazo kwamba hakuna Mungu nayo ni ya kibinadamu. Kwa hiyo si lazima yawe sahihi. Tena hayo ndiyo hayana mantiki kabisa, maana yanadhani kukosa ushahidi wa kitu ndio ushahidi kwamba kitu hicho hakipo.
You nailed it. Kukosa ushahidi wa kitu haimaanishi hicho kitu hakipo.
 
huo haukuw msingi wa hoja yangu wala sijatumia wingi wao kuhalalisha hoja yangu
ila kujaribu kueleza mtazamo wa baadhi yao
Ishu ya mtazamo nayo nimeiongelea kua sio kigezo cha kufanya kitu kiwe kweli, kinacho angaliwa ni uthibitisho ulio tolewa kuonesha uhalisia wa kitu

Je hiyo mitazamo ya hao wanasayansi imeambatana na uthibitisho kuonesha Mungu yupo au ni claims/ assumptions ambazo hazijathibitishwa?
 
Kwanini umemtaja Mungu, na kujikita kwemye hoja hiyo, nilidhani kama mtu haamini katika Mungu hakuna sababu hata ya kumtaja maana ni kitu kisichokuwepo.
Wewe una amini miungu ya kigiriki?

Mbona unaitaja kila siku?
 
Ukiona simu, gari, meza, nyumba, kuna mtu/watu nyuma ya hivyo vitu walioviunda.

Ni ajabu ukiamua kufumba ufahamu wako kukataa kwamba vitu kama bahari, ardhi, mimea, na sisi binadamu hakuna aliyenyuma ya uwepo wake.
Kwa hiyo una maanisha yule anayesema kuna aliye nyuma ya chanzo cha binadamu atakua kaufumba ufahamu wake endapo atasema huyo aliye nyuma ya chanzo cha binadamu hakuna kilicho nyuma yake kilichomsababisha awepo?
 
Mbona unanilisha maneno, wapi nimesema hayo uliyoandika.
kwani we hutumii kalenda?

Kwasababu kwenye kalenda january ni mungu wa kigiriki "janus" na "March" ambaye ni mungu wa "mars"

Na kama ni mkristo basi nakupa na hii nyingine kama ulikua huelewi, kua hata ile Easter mnayo sherekea imetokana na sherehe za Mungu wa "ishtar" huyu ni mungu wa ngono waki Babylon Eostre, Astarte, au Ishtar,

For the same reason kwa namna moja au nyingine utakua unaabudu hiyo miungu na kuikubali kua ipo na ni ya kweli kwasababu umekua ukiitaja kupitia kalenda ambayo imepewa majina yao, au easter ambayoi ni sherehe ya kikristo iliyotumia jina la mungu mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…