Hili ni tatizo la kutokuwa makini na kile ulicho kiukiza. Swali lako nimejibu tena kwa kutoa mfano nabii Isa,swali lako la kitoto na lina baki kuwa la kitoto kwa maana uliegemea kwa mtume Muhammad ukasahau kwamba njia hii imetumika kwa mitume wengine.
Mola hapangiwi jambo bali anafanya kile ambacho ni bora.
Nilikwambia huko awali ya kuwa si kweli Uislamu umetangaa kwa jihadi pekee,jihadi ni ibada kama ibada nyingine,jihadi ni ibada ambayo imekuja baadae.
Allah anasema katika Qur'aan ya kuwa.
36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha. (an-Nahl :36)
Katika kila umma aliwatuma manabii maana yake hata huku kwetu walitumwa manabii japokuwa hawajatajwa kwa majina. Lakini manabii na mitume wote walikuwa dini moja.
Mola hapangiwi ndiyo maana kila kitu kimewekwa wazi,leo katika dini yetu kuna hukumu ya mtu ambaye aliishi hapa duniani lakini hakufikiwa na ujumbe,ili ujue ya kuwa hakuna mwanya wa kutokea katika ujumbe na Mola wetu anafanya kilicho kuwa bora.
Hapa tunaangalia elimu na uhalisia,hizo busara nafasi sababu njia zote zimefanyiwa kazi.
Naoma unarudia kitu ambacho kilishafanyiwa kazi na kipo.
Mjinga asiye soma ndiyo ataona kuna "comfusion" kati ya shia na suni,mashia wako mbali ma uislamu kwa sababu hawaufati.
Kila kitu kipo wazi,mtume wetu anasema ametuacha katika hali ambayo mchana wake ni sawa na usiku wake,hatopotea humo ila mwenye kutaka apotee. Kwahiyo hizi zako zinabaki kuwa stori tu.
Hii si hoja,ndiyo maana hata wale ambao hawakufikiwa na ujumbe wana hukumu yao,bali mpaka watoto walio kufa kabla ya kunalehe wana hukumu yao. Ili ujue ya kuwa akili yako ni ndogo sana kufikiria mambo haya kwa kudhani tu walio angaliwa hapa ni watu fulani tu.
Kwanza kabisa Uislamu haujawahi kutokuwepo katika uso wa ardhi hii. Nakupa mfano watazame Wanafalsafa wa kale wa magharibi,hawa waliishi kipindi ambacho hapakuwa na mtume lakini mafundisho ya mitume walio pita yalikuwepo na kuna watu walikuwa wanayatumia mafundisho hayo.
Tukirudi kwa watu ambao wameishi mpaka wanakufa hawakufikiwa na ujumbe watu ambao mpaka leo hii wapo,hawa hukumu yao ipo,watapewq mtihani siku ya malipo watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli watalipwa moto.
We hujui hata jinsi ya kusoma na kujibu hoja...
Unajibu tu unavyoelewa wewe
Nimekuuliza kwanini Allah asingeteua katika Kila kabila na kila jamii ya watu, Asia, Ulaya, Africa, America etc mitume yake ambayo ingesambaza ujumbe kuhusu uislamu kwa wakati mmoja tena usiopingana
Njia hii ingekua na manufaa mengi Sana
Moja kusingekua na huu utitiri wa dini nyingi ambazo zinamfanya mtu kutokua kuwa na uhakika ipi ni sahihi
Pili kusingekua na madhehebu mengi katika dini moja kwa sababu wote tungehubiriwa kuhusu habari moja tena katika lugha tunayoifahamu
Tatu, kwa kuwa ingewafikia watu wote kwa pamoja, ingewapa watu wa zama zote fursa moja ya kusikia habari ya ukombozi
Wasioamini wasingekuwepo kabisa au wangekuwa wachache
Mungu muweza wa yote asingeshindwa kuleta dini yake kutumia hii njia, kwa sababu ina faida nyingi bila hasara
Nakuuliza kwanini Allah ameshindwa kutumia hii njia na badala yake akachagua jamii moja tu ya binadamu bila sababu yoyote ile (Racism) na kuanzisha dini yake pale?
Unanambia Mbona hata Yesu alikua muyahudi?
Hapa hujajibu swali kwanini Allah Alishindwa teua mitume kutoka kwenye kila jamii?
Nakuuliza kwanini umefanya jambo fulani, unanambia mbona fulani naye kafanya?
Hapo umejibu swali?
Unanambia pia Mungu hapangiwi cha kufanya, hapa sio kipi apangiwe
Hapa ni ipi ni njia bora zaidi?
Nambie ipi njia bora kati ya kuteua mitume kwa Kila jamii ya watu au kuchagua jamii moja bila Kuwa na sababu yoyote ile?
Halafu hujui hata Historia, Uislamu haukuwepo tangu kuwepo Kwa binadamu
Ni imani ya hivi karibuni, Ukristo tu ulikuwepo kabla yake
Kuna imani na dini kongwe kuliko uislamu
Sasa ukija na utetezi wa kitoto kuwa kila binadam anazaliwa Akiwa muislam utachekesha watu humu
Nakuuliza tena, kwanini Allah hakuchagua mitume kutoka kwenye kila jamii ya watu na kuwapa ujumbe wake?
Badala yake akachagua jamii ya kiarabu bila sababu yoyote?
Dini yoyote ile ni zao au chimbuko la eneo fulani,inaanzishwa na watu wa eneo hilo na mara zote inabeba tamaduni za eneo hilo