Njia gani nzuri ya kutatua changamoto kama hii kazini kwangu?


Shukrani Sana, ntafanya hivyo maana hili swala Lina athiri afya yangu ya kiakili
 
Yawezekana akawa na inferiority complex

Yaani kuna watu ambao huwa wanapata relief wanapomtukana mtu na kumfokea.

Njia ya kuishi nao ni kuwa positive tu akiona anafoka then wewe upo Una smile ataanza kubadilika mwenyewe.
 
Nyie si ndo mnaokandiaga wafanyakazi wa serekali??
Sirikali kugombezana ni 😁😁😁
Nilitaka kusema hii kitu. Kila leo humu kukandia kazi zs Serikali na watumishi wa umma, ila huo ujinga wa kufokeana kama watoto na kugombezana Serikalini haupo, niliwahi kufanya kazi kampuni binafsi yq mawasiliano, miaka minne niliiona kama karne, japo nililipwa vizuri ila sio kwa manyanyaso yale.
 
  • Kwa kuwa upo sekta binafsi, ni sawa na jina lako kuandikwa kwa penseli, muda wowote linaweza kufutwa.​
  • Kama huna taasisi nyingine ya kufanya kazi, nakushauri vumilia kwanza na chukulia malalamiko yake kama fursa ya kukujenga.​
  • Mfanye awe rafiki yako,muombe akuelekeze kazi ata kama unajua zaidi.​
  • Pia usiwe siriazi sana kazini, jitahidi uwe ni mtu wa kuwafanya wengine wawe na furaha pale wakuonapo.​
 
Kama utaamua kuacha, basi hakikisha unampiga siku unaacha kazi hapo. Hii itapunguza maumivu ya manyanyaso aliyokufanyia pia itamfanya abadilike atakapopata mfanyakazi mwingine
Umemuuliza lakini mleta mada kama ngumi zinatoka..Asijekuwa ni mwepesi akaishia tena kudundwa mbali na manyanyaso aliyopokea.

Maumivu yataongezeka maradufu.
 
Unapitia changamoto kama yangu!Huenda umemzidi elimu anakuona kama kikwazo kwake 2Ni mtu asiyependavwatu wa chini yake inawezekana alipatia malezi ya kupigwapigwa.Fanya ujasiri siku Moja ukiwa kwenye mood nzuri mueleze ukweli kwamba hujisikii vizuri kufokewafokewa na ikibidi,awepo mtu unayemuamini,Cha msingi kama ni mtu wa Dini muombe sana Mungu kwenye Hilo.
 
Nipe namba zake, kazi ndogo hiyo.
Kawaida huyo Boss lazima atakuwa anawakaripia watu wengine mtaani na nyumbam kwake pia.
Nikimpigia nitampa onyo kuwa aache kufokea watu mtaani, nyumban na kazini, na nitamuambia iwapo atarudia nitajua na sitakuwa na msahama naye. Hivyo ajitune na nakuhakikishia atajitune mara moja.
 
Fanya kwa muda upate mtaji wa kujiajiri na kujistiri. Baada ya hapo acha kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…