Njia gani nzuri ya kutatua changamoto kama hii kazini kwangu?

Njia gani nzuri ya kutatua changamoto kama hii kazini kwangu?

1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Nenda kwny maombi mambo mengne ni spiritual issues
 
Waswahili wanasema "Akufukuzae hakwambii toka" Fanya mpango upate ajira nyingine hapo uachane napo.
 
nishajaribu kumuuliza kuwa Kuna shida gani mpka inakuwa hivi,sema anaishia kunichekea na kusema hamna shida,,,awamu hii ntaongea naye kwa kina
Usiongee nae kwa kina, mpige biti mpaka aogope kukufuta kazi.
 
Pole sanaa mkuu kwa changamoto, ni hali ya kawaida kukutana na hali hiyo ukiwa mwajiriwa, pia hata kwenye mahusiano n.k

Lakini kabla ya kulaumu, fanya utafiti wakina kujua sababu zinazokufanya ukumbane na changamoto hiyo, Pia angalie wafanyakazi wenzako wanavyoishi then relate mahusiano yao na Boss wako. Hii itakusaidia kujua boss wako ni mtu wa aina gani,anapenda kipi/hapendi kipi, anapenda/hapendi watu wa aina fulani.

Pia kumbuka hakuna boss anaependa aonekane kuwa chini ya wafanyakazi wake, kama umemzidi elimu,akili,muonekano(smart) au kama unakubalika sanaa na wafanyakazi wako kuliko yeye atatafuta sababu ya kukushusha hadhi yako. NB: sio wote wana roho hiyo ya kuchukia wafanyakazi,pia Wapo maboss wanaopenda wafanyakazi wanaokuwa smart kwenye kazi (Kuna kabila/jamii huwa wanatabia hiyo.. wakipanda cheo lazima mtaona chamoto, ni nature yao kwahiyo ishi nao kwa akili)

Lakini kunasababu zinazoweza kusababisha boss kukuchukia:

●Kutotimiza wajibu wako. Hakuna boss anayependa kuwa na mfanyakazi ambaye hatimizi wajibu wake, Yaani kilakitu lazima uambiwe,ukumbushwe kila kitu unakuwa wa mwisho. Kama una hiyo tabia acha mara moja.

●Kuwa na uwezo mdogo wa kujenga hoja. Fahamu deeply taaluma yako, pata ujuzi mpya kila siku, ikitokea kuna tatizo ofisini usikae kimya toa msaada wa mawazo ya kuimarisha ofisi.

●Kuto jali muda. Hakuna kitu muhimu kwenye taasisi yoyote kama muda, Jali muda wa kuingia kazini na kutoka, muda wa kuanza kazi na kumaliza, Jali muda mkihaidiana mfano kikao,kutoa repoti,n.k

●Kutoshirikiana na wafanyakazi wenzako. Kuna muda wa kazi, na muda wa kupumzika, hivyo kuwa social, zungumza na wenzako usijitenge sanaa, na usiwazoee sanaa.

●Acha mazoea na boss wako kwenye mambo ya kipuuzi, hapa kuna kuna seheme tofauti kama kwenye media,whatsapp the way unavyochat na watu wanakuchukulia boya tu, so yanakushusha hadhi, acha upuuzi.

●Usiwe mropokaji wa ovyo ovyo, Yaani Chochote unacho zungumza kiwe na manufaa,Kama wenzako wanajadili upuuzi usitoe maoni stay cool,Sometimes to be silent is better

●Epuka kutoa siri za maisha yako kwa kila mtu, watu wasijue kilakitu ulichonacho, au unachokipitia au tabia zako nje ya kazi. Kama unapiga gambe sanaa punguza.

●Kuwa Ruler 📏 kama YES iwe YES, NO iwe NO. Usiwe mtu wa kuyumbishwa tu na watu, Watu wajue unamsimamo. Hata boss akijua una msimamo ata kuheshimu, hawezi kuja kichwakichwa.

Maisha hayana njia moja, sio lazima njia uliyonayo ndiyo utakayo tokea.

● Mwisho : Usiache imani ya Mungu wako. Kwenye ofisi zetu za kibongo kuna mambo mengi sana kama ushirikina,waenda kwa waganga kukupiga tukio n.k (Hii wanaita kukupaka mavi ,kama kuna mtu kakufanyia hilo, hapo hutoboi hadi utafukuzwa kazi) namna ya kutoka fuata kanunu za kiimani, asubuhi kabla ya job Pray, ukiwa kazini Pray, ukitoka Pray, eneo la kazi Pray, Pray daily. Then urudi utupe mrejesho.

Asante
Nimeipenda hii expert wangu
 
Kwenye kutafuta ridhiki kuna changamoto nyingi sana, endelea kufanya kazi ukiwa unatafuta kazi sehemu nyingine, usiache kazi kabla ya kupata kazi sehemu nyingine.
 
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Ni nani mwenye elimu kubwa kuzidi mwenzake?
Pia, ana umri gani kwa makadirio na wewe una umri gani?
 
Ukiona hivyo ujue anakuona Zoba.
Una Roho ya kukandamizwa

Huna utisho. Wenzako wanaendaga kwa Sangoma kudai utisho.
Wengine wamezaliwa nao. Wengine wanapewa na Muumba
 
Kwenye kutafuta ridhiki kuna changamoto nyingi sana, endelea kufanya kazi ukiwa unatafuta kazi sehemu nyingine, usiache kazi kabla ya kupata kazi sehemu nyingine.
Shukrani Sana Asante
 
Ukiona hivyo ujue anakuona Zoba.
Una Roho ya kukandamizwa

Huna utisho. Wenzako wanaendaga kwa Sangoma kudai utisho.
Wengine wamezaliwa nao. Wengine wanapewa na Muumba
Duhhh hivyo suluhisho ni Nini kwa hili swala langu?
 
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Wewe fanya kazi kama mkataba unavosema....ingia kwa wakat na toka kwa wakati ofisini.
Kama anafoka na anakulipa mshahara basi ww fanya yako huku unapambana utoke hapo
 
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Mloge
 
Boss wangu alikua ana nikopa hela afu arudishi kwa wakati sikuwa mnyonge tukiwa wawili ofisini tuna kabana mashati tukitoka njee ana foka kama kawaida
 
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Daaah pole mkuu... hakika hapa utapata msaada mzuri wa mawazo. Umeandika in so touching way....
 
Back
Top Bottom